18 Oct 2023 in National Assembly:
majengo mengi. Haya mambo hayakuanza leo; yalianza wakati wa manispaa kabla ya serikali za ugatuzi. Ugawanyaji wa ardhi hauwezi kupita bila kuonyesha public utility ni zipi. Kwa kuwa mpangaji atapangisha wananchi, hawatatoka juu mbinguni wakianguka chini. ni muhimu wawe na barabara ya kutoka nje na kurudi ndani. Ni muhimu wawe na sehemu maalum ya taka ambayo si ya mpangaji bali mali ya umma. Wale wanaoenda kanisani na muskitini lazima wawe na sehemu ya kuabudu. Wale wanaoabudu Jumamosi pia wawe na sehemu yao ya kuabudu. Ikiwezekana, ardhi za umma zifanyiwe auditing kuanzia wakati manispaa zilipokuweko, ili kama ardhi hizo zingalipo zirudi ...
view
11 Oct 2023 in National Assembly:
Nilikua ninataka kuzungumzia kuhusu mihadarati kwa sababu imeniathiri sana katika eneo Bunge la Kisauni lakini sikupata nafasi. Si neno lakini wacha nizungumzie sukari vile imezungumzwa na Mhe. Salasya. Ningependa kusema kwamba Serikali iwe angalifu kwa kulinda viwanda vyetu. Ikiwa viwanda vyetu vinatoa bidhaa ya kutosha, hakuna haja ya kuagiza kutoka mataifa ya nje. Mnapoagiza kutoka mataifa ya nje, mnafanya vijana wetu wengi wakae bila ajira. Ni vyema sana tuvikuze viwanda vyetu ndio tuwe na ajira na nguvu ya kiuchumi ya nchi yetu kindani. Wakulima wetu wanalima sukari na bidhaa zingine, lakini wanashindwa mahali pa kuuzia kwa sababu vitu vingi vingi ...
view
11 Oct 2023 in National Assembly:
Nilikua ninataka kuzungumzia kuhusu mihadarati kwa sababu imeniathiri sana katika eneo Bunge la Kisauni lakini sikupata nafasi. Si neno lakini wacha nizungumzie sukari vile imezungumzwa na Mhe. Salasya. Ningependa kusema kwamba Serikali iwe angalifu kwa kulinda viwanda vyetu. Ikiwa viwanda vyetu vinatoa bidhaa ya kutosha, hakuna haja ya kuagiza kutoka mataifa ya nje. Mnapoagiza kutoka mataifa ya nje, mnafanya vijana wetu wengi wakae bila ajira. Ni vyema sana tuvikuze viwanda vyetu ndio tuwe na ajira na nguvu ya kiuchumi ya nchi yetu kindani. Wakulima wetu wanalima sukari na bidhaa zingine, lakini wanashindwa mahali pa kuuzia kwa sababu vitu vingi vingi ...
view
23 Aug 2023 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kutupatia nafasi ya kusema pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Mhe. Ndzai. Ninaomba utupatie nafasi tutoe rambirambi zetu.
view
23 Aug 2023 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika. Pia mimi ninasema pole.
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Asante sana Mheshimiwa Spika wa Muda…
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Mhe Spika wa Muda, ninakushukuru kwa mwongozo huo. Nitaenda kwa haraka ili wenzangu pia wapate muda na fursa ya kuchangia. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu niko na imani kwamba umetoka kwa Wizara mbili muhimu – Wizara ya Afya, na Wizara ya Kilimo – ambazo zilikaa chini zikakubaliana. Kwa hivyo, niko na imani kuwa hili ni jambo muhimu ambalo litasaidia taifa. Ubora wa chakula ni jambo muhimu sana. Pia, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu utahusisha serikali za ugatuzi katika jitihada za kuboresha chakula kabla ya kukipeleka kwenye masoko yetu. Tuko na imani kuwa wakihusishwa, mambo mengi pia yatakwenda sawa. ...
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Wananchi wanategemea mashirika ya kiserikali kuwasaidia kwa sababu hawana uwezo wa kuchunguza vile chakula kimetolewa shambani. Hiyo ni kazi ya mashirika ya kiserikali. Lakini kwa sababu hawashughuliki, na kwa sababu ufisadi umekuwa mwingi, mwananchi anapata chakula kisicho salama kinachosababisha ugonjwa wa saratani na magonjwa mengine. Kwa mfano, kuku wa gredi hupewa dawa fulani, na inabidi wakae siku saba kabla ya kuchinjwa. Lakini kwa sababu hakuna mtu anayechunguza jambo hilo, wale kuku wanachinjwa na kuletwa sokoni ilhali ile sumu bado iko kwenye nyama hiyo, na watu wanakuja wanaitumia.
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Mboga zinanyunyizwa dawa na kabla muda wa kuuzwa kufika, mtu anazivuna na kuzipeleka sokoni kwa sababu hakuna mtu anayeshughulikia jambo hilo. Taifa ambalo liko na chakula bora hupata watalii kwa maana chakula kikiwa bora, wageni watatoka sehemu tofauti kuja katika taifa letu kwa sababu wako na imani kwamba chakula chetu ni bora na salama.
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Lakini leo kama walivyosema wazungumzaji wengine, mtu akishamaliza kunywa chai, anaona kwenye runinga kwamba kuna sukari ya sumu ambayo imeingia nchini. Hicho ni kitu cha kustaajabisha. Watu wetu wanapata shida kwa kula sumu baridi. Watu wetu ni wagonjwa. Wewe ingia kwenye matatu, kama hujaingia siku nyingi, uone mtu anatoka kule tumbo languruma utafikiri kwapigwa ngoma ndani. Hii ni kwa sababu chakula ambacho amekula sio salama. Wale wanaotaka kutengeneza ofisi hii wawe ni watu ambao watajitolea. Sisi tunakubali ofisi hii iundwe, lakini wale watakaotekeleza kazi zao ndio hatujui.
view