15 Aug 2023 in National Assembly:
Wananchi wanategemea mashirika ya kiserikali kuwasaidia kwa sababu hawana uwezo wa kuchunguza vile chakula kimetolewa shambani. Hiyo ni kazi ya mashirika ya kiserikali. Lakini kwa sababu hawashughuliki, na kwa sababu ufisadi umekuwa mwingi, mwananchi anapata chakula kisicho salama kinachosababisha ugonjwa wa saratani na magonjwa mengine. Kwa mfano, kuku wa gredi hupewa dawa fulani, na inabidi wakae siku saba kabla ya kuchinjwa. Lakini kwa sababu hakuna mtu anayechunguza jambo hilo, wale kuku wanachinjwa na kuletwa sokoni ilhali ile sumu bado iko kwenye nyama hiyo, na watu wanakuja wanaitumia.
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Mboga zinanyunyizwa dawa na kabla muda wa kuuzwa kufika, mtu anazivuna na kuzipeleka sokoni kwa sababu hakuna mtu anayeshughulikia jambo hilo. Taifa ambalo liko na chakula bora hupata watalii kwa maana chakula kikiwa bora, wageni watatoka sehemu tofauti kuja katika taifa letu kwa sababu wako na imani kwamba chakula chetu ni bora na salama.
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Lakini leo kama walivyosema wazungumzaji wengine, mtu akishamaliza kunywa chai, anaona kwenye runinga kwamba kuna sukari ya sumu ambayo imeingia nchini. Hicho ni kitu cha kustaajabisha. Watu wetu wanapata shida kwa kula sumu baridi. Watu wetu ni wagonjwa. Wewe ingia kwenye matatu, kama hujaingia siku nyingi, uone mtu anatoka kule tumbo languruma utafikiri kwapigwa ngoma ndani. Hii ni kwa sababu chakula ambacho amekula sio salama. Wale wanaotaka kutengeneza ofisi hii wawe ni watu ambao watajitolea. Sisi tunakubali ofisi hii iundwe, lakini wale watakaotekeleza kazi zao ndio hatujui.
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Sasa, miraa na muguka zinapigwa dawa na kuletwa sokoni. Vijana wetu wengi sasa ni wenda wazimu kwa sababu ya dawa za sumu ambazo wanatumia kila siku.
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Mheshimiwa Spika wa muda, ninakomea hapo ili nitoe nafasi kwa wenzangu kuchangia Mswada huu.
view
15 Aug 2023 in National Assembly:
Ninaunga mkono.
view
9 Aug 2023 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika.
view
9 Aug 2023 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la ziada. Waziri wa Masuala ya Ndani na Utawala wa Taifa, tunayo imani na wewe. Tunayo imani utaleta mabadiliko. Umesema usajili wa wanajeshi uko huru, lakini kuna Wakenya ambao wanakatazwa kujiunga na jeshi kwa sababu ya kimo chao na siyo eti ni wagonjwa. Wanavaa viatu na suruali, na wana afya njema lakini wanakataliwa kwa sababu ni wafupi. Ni Mungu amewaumba hivyo. Kwa nini mnawanyima fursa ya kujiunga na jeshi? Kama mnawaona ni wafupi, wanaweza kumfikia adui bila kuonekana.
view
9 Aug 2023 in National Assembly:
Wachina ni wafupi Zaidi, lakini ni wanajeshi. Kwa nini tunawanyima Wakenya fursa ya kulinda taifa lao? Mhe. Waziri, hili jambo tunafaa tuliangalie kwa makini sana na tusiseme usajili ni huru kama hao tumewaweka nje. Ahsante sana.
view
5 Jul 2023 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika wa Muda.
view