5 Jul 2023 in National Assembly:
Nashukuru, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi kuuliza swali la ziada. Masuala ya ardhi katika Kisauni ni tatizo sugu. Je, Wizara ina mikakati gani kuyakomboa mashamba ili wananchi waishi kwa amani? Kuna tatizo katika shamba la Ugatuzi, shamba la Kashani na mashamba yaliyoko Junda. Je, mna mikakati gani ya kukomboa ardhi hizo?
view
5 Jul 2023 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, nilikuwa nikieleza swali langu lakini ikawa unazungumza na Mhe. Junet. Sijui kama Waziri alipata swali langu. Waziri, masuala ya ardhi ni sugu Kisauni. Je, Wizara ina mikakati gani ya kukomboa mashamba ili wananchi waishi kwa amani? Shamba la Ugatuzi, shamba la Kashani na mashamba yaliyoko Junda yako na tatizo.
view
5 Jul 2023 in National Assembly:
On a point of order, Hon. Temporary Speaker.
view
5 Jul 2023 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, Waziri hakujibu swali la mikakati walionayo kama Wizara ya kuyakomboa mashamba katika Eneo Bunge la Kisauni. Hakujibu swali hilo, ingawa halikuwa limeandikwa. Akiomba muda ni sawa. Bora nipate jawabu.
view
4 Jul 2023 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kupenyeza sauti yangu.
view
4 Jul 2023 in National Assembly:
Nimesimama kuunga mkono Ripoti hii. Taifa bora ni lile linalolinda mazingira yake. Mazingira ndio chanzo cha matatizo mengi. Mataifa mengi yanarudi nyuma wakati mazingira yanakuwa mabaya. Mazingira yanapokuwa mabaya, maradhi yanagubika taifa hilo. Na badala ya kwenda mbele, linarudi nyuma. Siyo vyema watu katika mataifa mengine ambayo ni ya kitajiri kutupa takataka zao sehemu zetu. Au hata mabaki ambayo wanaona hayawafai na kusema sasa yanakuja kama msaada na kumbe yana madhara.
view
4 Jul 2023 in National Assembly:
Bahari yetu imechafuliwa sana na mataifa yanayojiita ya kitajiri. Licha ya kuwa tuna umaskini, hao ndio wametusababishia umaskini huo kwa njia kama hii ya kutuletea uchafu ambao ni sumu. Tabia hiyo yao inaturudisha nyuma na wao wanatuambia kuwa wanakuja kutupa misaada. Maradhi ya saratani hayakuwa hapa Afrika hapo zamani. Sasa yamezidi mpaka mtoto mdogo anazaliwa na hayo maradhi kwa sababu ya ule uchafu wanaotubwagia. Kule kwao, wanajifanya wanasafisha bahari zao, lakini kwetu ndio wanatumia kama dumping grounds na kusema ni msaada. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can ...
view
4 Jul 2023 in National Assembly:
Taifa linaloheshimika ni lile ambalo linahakikisha kwamba watu wake wanaishi salama. Kuishi salama ni kutokubali kabisa kumwagiwa vitu usivyovijua. Wanatuletea vifaa, kama wanavyosema, vinakuja kama msaada lakini baada ya wiki mbili vinaharibika na tayari vilishatoa miale fulani kwa wale watoto kama ni vya shule. Ni vyema twende na hali yetu wenyewe. Tusijaribu kuomba misaada ambayo itakuja kutudhuru. Hata sisi katika taifa letu, ikiwa ni takataka ambazo ziko katika sehemu ya mji mwingine, zisihamishwe kupelekwa mji mwingine. Zikae pale pale na kama zina madhara, basi zikabiliwe pale na zisiambukize sehemu nyingine.
view
4 Jul 2023 in National Assembly:
Nimesimama kuunga mkono Ripoti hili. Tusikubali hilo licha ya umaskini wetu. Mungu ndiye atakuwa ametupa sisi na ana njia ya kutuhifadhi. Tusikubali kuletewa uchafu kutoka mataifa ya ulaya ama ya kitajiri. Kwa hayo machache, nashukuru na kuipongeza Kamati iliyounda Ripoti hii.
view