Ali Menza Mbogo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 151 to 160 of 295.

  • 6 Jun 2023 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili niweze kupenyeza sauti yangu. Kwanza, naunga mkono Ripoti hii ya Mhandisi wa Fedha. Pia, naitilia mkazo kwamba… view
  • 6 Jun 2023 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kutia sauti yangu haswa kwa miradi ya NG-CDF. Ile miradi inayopatikana na inayoonekana katika maeneo yetu sana ni ya NG-CDF. La kusikitisha zaidi ni kwamba hivi sasa, tunakaribia mwaka mwingine na hatujapata hata robo ya pesa. Ni hatari sana kwa sababu hizi ndizo fedha ambazo zilikuwa zinasaidia maskini asiyejiweza. Lakini sasa hana la kufanya kwa sababu ofisi zetu hazina fedha. Hata sisi tumepeana bursaries lakini mpaka sasa, hatujamaliza kupeana za sekondari na vyuo vikuu kwa sababu hakuna fedha. view
  • 6 Jun 2023 in National Assembly: Mhe. Spika wa Muda, mijengo mingi ya shule imeanguka. Vyoo vimefurika. Kila siku, ukiuliza unaambiwa shida ni hazina. Tunaenda mwaka mwingine. Sasa tutakua tena kwa view
  • 6 Jun 2023 in National Assembly: ama namna gani? Hii ni hatari kubwa sana ambayo Wakenya wanapitia. Hali ni ngumu. Ukiangalia shule sasa hivi, vyoo vimefurika. Kipindupindu sasa kinaanza kuingia katika shule zetu na huku unaambiwa ni hazina tunangoja. Lazima watueleze shida iko wapi kwa sababu fedha ziko. Kwa nini haziachiliwi na hii ndiyo miradi ambayo inasaidia wananchi? Nitakupatia mifano katika shule za Kisauni. Kuna Shule ya Msingi ya Kashani ambapo watoto wanasoma mpaka mlangoni. Wanakaa chini. Hata dawati hakuna. Watoto wanapata funza. Zile sakafu zimevunjika na huku ukiitisha fedha, unaaambiwa ungoje hazina. Kinachoendelea ni kitu cha kusikitisha sana. Ukiangalia sasa hivi wakati wa mvua, kuta ... view
  • 19 Apr 2023 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia hii fursa ili kupenyeza sauti yangu kwenye Mswada huu. view
  • 19 Apr 2023 in National Assembly: ni usafiri muhimu sana unaotumika katika Taifa nzima. Hakuna mji au kijiji utaenda na kukosa kuona waendeshaji bodaboda katika shughuli zao. Vile vile, bodaboda zimepunguza hali ya uhalifu nchini. Vijana wengine wanatumia bodaboda kutafuta riziki. Pia, zimesaidia kupunguza ukosefu wa ajira. Ingelikuwa hakuna bodaboda, basi kungekuwa na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 19 Apr 2023 in National Assembly: shida kubwa sana ya ukosefu wa ajira kwa vijana. Kwingine, bodaboda hututumika kama ambulensi za kubebea wangonjwa, haswa sehemu ambazo barabara ni mbaya. Kwa hivyo, view
  • 19 Apr 2023 in National Assembly: ni sekta muhimu ambayo inapaswa kuboreshwa. Ni kweli kuwa kuna ajali nyingi sana zinazosababishwa na bodaboda . Kama wenzangu walivyosema, katika hospitali nyingi, kuna wodi zilizotengewa watu wa bodaboda tu kwa sababu ni wengi. Hii inasababishwa na kutokuwa na mafunzo ya uendeshaji wa bodaboda hizo. Sekta hii pia inashuhudia umaskini mwingi sana. Maskini wengi sana ndio wanatumia mfumo huu wa usafiri. Wengi wa waendeshaji wanashindwa kwenda kusomea uendeshaji wa view
  • 19 Apr 2023 in National Assembly: kwa sababu ya bei ghali ya karo. Tunapaswa kubuni taratibu zinazofanya bei ya karo kuwa tahafifu ili waendeshaji bodaboda waweze kwenda shule na kujua kanuni za barabara. Wengi wanashindwa kwenda kusoma kwa sababu hali ni ngumu. Pia wanatakiwa kupatia wenye bodaboda Ksh500 kwa siku, kwa kila Ksh1,000 wanazopata. Kwa hivyo, tunapaswa kubuni taratibu zitakazofanya bei ya karo iwe tahafifu ili waendeshaji bodaboda wapate mafunzo na ujuzi wa kuendeleza biashara hii. view
  • 19 Apr 2023 in National Assembly: na tuk-tuk ni muhimu sana. Kwa hivyo, kama Bunge la Taifa, tunapaswa kubuni taratibu za kuwasaidia. Hata serikali za ugatuzi zinapaswa kutoa viegezo vya kujikinga haswa wakati kama huu wa mvua na pia wakati wa jua. Serikali za kaunti pia ziwapatie helmets na pia sehemu za kusafisha helmets hizo. Si tu watu kutumia helmets na koti zile bila kusafishwa. Zinaweza kusababisha maradhi. Ni mambo mengi ambayo tunahitaji kupanga kwa utaratibu ili kukuza sekta hii ili iweze kuwafaidisha watoto na vijana wetu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus