1 Mar 2023 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda, kwa kuniruhusu niweze kupenyeza sauti yangu kwa suala hili. Nitafanya haraka kwa sababu ya muda ili wengine wapate nafasi ya kuchangia. Kwa kweli, inasikitisha sana Mahakama Kuu kuidhinisha kusajiliwa kwa vyama hivi vya usagaji na ushoga ama uhanithi. Mimi nitawasihi majaji hao wamche Mwenyezi Mungu. Hapa duniani tumekuja kulima shamba ambalo matunda yake tutayapata mbeleni. Kwa hivyo, lolote wanalolifanya na maamuzi yote wanayoyatoa hivi sasa watakutana nayo mbele akhera, ambapo wote wataondoka katika ulimwengu huu. Hakuna mtu atabaki. Pia wajue kwamba wataweka kumbukumbu za vizazi vilivyoko na vitakavyokuja kulingana na maamuzi ambayo wanayafanya sasa. ...
view
21 Feb 2023 in National Assembly:
Ninakushukuru kwa taratibu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
21 Feb 2023 in National Assembly:
Kuhusu swala la CBC, kwa kweli taifa halijakuwa tayari kwa haya mageuzi ya elimu. Shule zilizochaguliwa kuwa na junior secondary school ni chache ukilinganisha na wanafunzi walio wengi zaidi. Walimu waliochaguliwa ni wachache ukilinganisha na shule na wanafunzi. Fedha, pia, za kuwezesha mchakato huu kuendelea kikamilifu. Shule zote hazina mahabara na CBC haiwezikukamilika bila mahabara. Wazazi wanaumia kifedha kupeleka watoto wao junior secondary schools. Wanaambiwa wabadili sare za shule na pia waende na madawati. Kila siku kuna mambo mapya mpaka inakuwa vigumu kutekeleza swala hili. Kwa hivyo, ninasimama na wengi wa Wajumbe Bungeni ambao wamezungumzia kuwa swala hilo bado; Serikali ...
view
16 Nov 2022 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika wa Muda. Hata mimi nilibonyeza kidude kitambo ili nizungumzie swala la NG-CDF, lakini sikupata nafasi. Labda uniruhusu dakika moja niseme ni vyema waachilie hizo pesa kwa sababu zinasaidia wengi sana kule mashinani. Umaskini ulioko kule mashinani ni mkubwa sana. Hata watu wakiambiwa wapeleke mia mbili ya chakula shuleni inawashinda. Ni vyema sana Serikali iachilie hizi fedha ambazo zinasaidia watu maskini. Hali ni ngumu na kazi hakuna. Watu wanategemea hiyo pesa. Kwa hivyo, sioni sababu ya Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Hazina ya Taifa kusema kwamba ataenda kutafuta ushauri kwa Mkuu wa Sheria. Hii ni kwa sababu ...
view
16 Nov 2022 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, kupanda miti kando ya barabara ni muhimu sana. Miti inasaidia kunyonya hewa chafu kutoka kwa mazingira na kuachilia hewa safi ambayo tunatumia. Miti husaidia sana kuboresha mazingira. Afya za watu wengi mahali kuna miti ziko imara kuliko mahali hakuna miti. Miti ikipandwa kando ya barabarani ama mitaani itazuia mmomonyoko wa udongo. Ukipanda miti, hata wakati wa mvua hakutakuwa na mafuriko. Katika sehemu ambako hakuna miti, mafuriko yanakuwa makubwa na athari zake zinakuwa kubwa zaidi.
view
16 Nov 2022 in National Assembly:
Uzuri wa kupanda miti ni kwamba kunafanya mahali panapendeza. Wakati wa ukame, kunakuwa na maua aina fulani yanayotoka. Wakati wa mvua pia kunatokea maua ya aina fulani ambayo hutupatia vivuli katika sehemu zile. Miti pia ni muhimu sana kwa sababu kuna viumbe wanaolala hapo, kama vile ndege ambao wanakwenda pale usiku. Hapo ndipo nyumba zao. Kwa hivyo, ni muhimu kwa mkandarasi yeyote anayejenga barabara alazimishwe apande miti. Miti husaidia watu wengi na hata viumbe vingine ambavyo vinaishi katika miti hiyo.
view
16 Nov 2022 in National Assembly:
Kwa hayo mengi, ninaunga mkono Hoja hii.
view
8 Nov 2022 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nitaiendeleza hii lugha ya taifa kwa sababu watu huringa na lugha yao. Kwa hivyo, nakushukuru pia kwa kulifahamu swala hilo. Ukienda Urusi, wanazungumzia lugha yao. Ukienda Uarabuni, wanazungumza lugha yao na wameendelea zaidi. Hapa kwetu, tumejaribu kuchukua lugha ya kigeni na kuiweka mbele. Ndiyo sababu hata hatuwezi kutengeza sindano ya kushona nguo. Basi wacha niachie hapo.
view
8 Nov 2022 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, nachukua fursa hii kwanza kukushukuru wewe na kukupongeza kwa kunipa fursa mimi nitie sauti yangu katika swala hili. Naunga mkono marekebisho ya Katiba kuihalalisha NG-CDF katika Katiba iwe haitasumbuka na kusitokee mtu kwenda kuishtaki ama kuilalamikia. Iwe iko ndani ya Katiba na iwe ni sheria kwamba hizi fedha ziwe zinakuja bila kuwa na kikomo wala hofu. Mengi yamezungumzwa lakini mimi pia nitatia sauti yangu hapo. Hakika, NG-CDF ni hazina ambayo imesaidia wananchi. Kenya ni taifa ambalo wengi wa wananchi hawana ajira na wengi ni maskini. Wenye uwezo ni wachache. Wengi wanashindwa hata kunywa chai. Wengine wana ...
view
8 Nov 2022 in National Assembly:
. Ni yeye mwenyewe ataenda kwa wananchi na kuwauliza wanataka awafanyie nini na pesa zao. Hana sababu ya kwenda kuombaomba. Tupewe uwezo wa kutumia hii NG-CDF kuwalipa hata wale wazee wa mtaa ambao hawalipwi chochote. Tuweze kuwalipa hata kama ni kitu kidogo kupitia hazina hii ya NG-CDF. Imewasaidia walala hoi. Wazee wa mtaa pia ni miongoni mwa watu wanaotatua kesi nyingi na kusaidia katika masuala ya usalama katika maeneo yetu. Ajabu ni kwamba hakuna kitu wanacholipwa. NG-CDF ni chombo muhimu sana. Hivi sasa, shule za umma zina magari ya kuwazungusha watoto katika ziara za elimu kwa sababu ya NG-CDF. Ingekuwa ...
view