8 Nov 2022 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nitaiendeleza hii lugha ya taifa kwa sababu watu huringa na lugha yao. Kwa hivyo, nakushukuru pia kwa kulifahamu swala hilo. Ukienda Urusi, wanazungumzia lugha yao. Ukienda Uarabuni, wanazungumza lugha yao na wameendelea zaidi. Hapa kwetu, tumejaribu kuchukua lugha ya kigeni na kuiweka mbele. Ndiyo sababu hata hatuwezi kutengeza sindano ya kushona nguo. Basi wacha niachie hapo.
view
8 Nov 2022 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, nachukua fursa hii kwanza kukushukuru wewe na kukupongeza kwa kunipa fursa mimi nitie sauti yangu katika swala hili. Naunga mkono marekebisho ya Katiba kuihalalisha NG-CDF katika Katiba iwe haitasumbuka na kusitokee mtu kwenda kuishtaki ama kuilalamikia. Iwe iko ndani ya Katiba na iwe ni sheria kwamba hizi fedha ziwe zinakuja bila kuwa na kikomo wala hofu. Mengi yamezungumzwa lakini mimi pia nitatia sauti yangu hapo. Hakika, NG-CDF ni hazina ambayo imesaidia wananchi. Kenya ni taifa ambalo wengi wa wananchi hawana ajira na wengi ni maskini. Wenye uwezo ni wachache. Wengi wanashindwa hata kunywa chai. Wengine wana ...
view
8 Nov 2022 in National Assembly:
. Ni yeye mwenyewe ataenda kwa wananchi na kuwauliza wanataka awafanyie nini na pesa zao. Hana sababu ya kwenda kuombaomba. Tupewe uwezo wa kutumia hii NG-CDF kuwalipa hata wale wazee wa mtaa ambao hawalipwi chochote. Tuweze kuwalipa hata kama ni kitu kidogo kupitia hazina hii ya NG-CDF. Imewasaidia walala hoi. Wazee wa mtaa pia ni miongoni mwa watu wanaotatua kesi nyingi na kusaidia katika masuala ya usalama katika maeneo yetu. Ajabu ni kwamba hakuna kitu wanacholipwa. NG-CDF ni chombo muhimu sana. Hivi sasa, shule za umma zina magari ya kuwazungusha watoto katika ziara za elimu kwa sababu ya NG-CDF. Ingekuwa ...
view
8 Nov 2022 in National Assembly:
CDF, mambo ya usafiri yangekuwa katika shule za kibinafsi pekee. Naomba kuwa NG-CDF ibakie ili isaidie. Ihalalishwe kwenye Katiba ili iendelee. Si vibaya hata hawa ndugu zetu Maseneta wakipewa fedha, bora zimfaidi mwananchi. Wakati mwingine unasikia Serikali ikisema kuwa uchumi umeimarika. Uchumi hauwezi kuimarika kama mwananchi hana kitu mfukoni mwake! Lazima uchumi uhusiane na mwananchi. Kwa hivyo, hata wale Maseneta wakitaka fedha za kuwasaidia wananchi, wapewe. Ikiwa zile fedha Wawakilishi wa Akina Mama watapewa zitasaidia, itakuwa vizuri zaidi. Ikiwa Wawakilishi wa Akina Mama, Wajumbe na Maseneta watasaidia, wananchi ndio watafaidika. Hili ni taifa letu sote. Kwa hivyo, ni lazima tushirikiane ...
view
2 Nov 2022 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Nachukua fursa hii kumshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kunipa hii fursa ili niweze kupenyeza sauti yangu katika Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili. Naunga mkono kwa sababu wakati Baraza hili litakapobuniwa, nina imani kwamba Kiswahili kitashamiri na kitakuwa lugha muhimu katika Taifa letu. Mataifa mengi yaliyondelea yalitumia lugha za mama. Ukiangalia Uingereza, Urusi na Bara la Arabu, wanatumia lugha zao na nchi hizo zimeendelea zaidi. Ukiangalia Taifa Jirani letu la Tanzania, limeweza kuwa na maendeleo mengi kwa sababu ya kutumia lugha zao. Ningeomba kwamba almashauri zote za kiserikali ziweze kuweka maandishi katika milango ...
view
12 Oct 2022 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia fursa ya kupenyeza sauti yangu katika janga hili la ukame. Lakini, kabla ya hayo, nachukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwa katika Bunge la Kumi na Tatu. Kama sio uwezo wake, singekuwa hapa. Nina imani nitafanya mema wakati huu wa kipindi hiki cha miaka mitano.
view
12 Oct 2022 in National Assembly:
Pili, nachukua fursa hii kukupongeza kwa kuchaguliwa kama Naibu Spika wa Bunge hili la Kumi na Tatu. Tuna imani utafanya haki pamoja na Spika Moses Wetangula katika The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
12 Oct 2022 in National Assembly:
Bunge hili, ili wote wapate fursa ya kuzungumza. Nachukua nafasi hii pia kushukuru familia yangu kwa kunipa moyo na nguvu wakati wa kampeni, ili nisirudi nyuma mpaka nikapata ushindi. Nawashukuru sana. Pia, nichukua fursa hii kuwashukuru wangwana wa Kisauni kwa kunichagua kuwa Mjumbe wao na kwa kuniamini ili niweze kuwaakilisha katika Bunge hili la Kumi na Tatu. Nina imani kwamba wako katika mikono salama na nitakaa na wao. Tutasaidiana kwa hali na mali kuhakikisha kwamba Eneo Bunge letu la Kisauni linasonga mbele. Baada ya kunipumzisha katika Bunge la Kumi na Mbili, nashukuru kwa sababu waliniamini na wakaona kwamba wamekosa huduma ...
view
12 Oct 2022 in National Assembly:
Namshukuru Mhe. Rais kwa kurudisha huduma za utendakazi wa bandari kwa Wapwani. Tunawaomba wawekezaji warudi ili watumie fursa hiyo ili vijana wetu wapate ajira. Pia, bandari irudishe ile mfumo wa zamani wa ‘white card’ ili watoto wetu waendelee kupata ajira. Watoto wetu wamekaa mabarazani. Tuna imani kwamba ikiwa watarudisha hiyo ‘whitecard’ itatusaidia zaidi ili watoto wengi waajiriwe. Kutakuwa na moyo na hata wao watakuwa na ufahamu kwamba baada ya muda fulani, watarudi kufanya kazi na wengine watabadilishana baada ya miezi mitatu.
view
12 Oct 2022 in National Assembly:
Suala la maskwota ni tatizo kubwa Pwani, hasa Kisauni. Nina imani Serikali hii ya awamu ya tano itashughulikia suala hili. Moja katika ahadi walizozitoa ni kwamba wataumaliza uskwota na tunasubiri kuona hilo jambo likitekelezwa.
view