All parliamentary appearances
Entries 351 to 360 of 612.
-
29 Jun 2016 in National Assembly:
Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nami nichangie Hoja iliyo mbele yetu. Kwanza, ningependa kutoa kongole kwa ndugu yangu Yusuf kwa kuweza kutupa kofi ya fahamu. Mheshimiwa Yusuf ametupiga kofi ya fahamu na ametuzindua tuweze kuishukuru historia ya taifa la Kenya. Utakapoangalia kwa uchache wa fikra, Hoja iliyo mbele yetu haina maana. Lakini utakapokwenda kwa bahari na upana, utakapofurahia historia ya taifa lako na kumbukumbu ya kule tulikotoka, Hoja iliyo mbele yetu ni muhimu na inastahili kuungwa mkono na kupitishwa ili sehemu hiyo iweze kuhifadhiwa iwe katika kumbukumbu ya taifa ama katika makavazi ya ...
view
-
29 Jun 2016 in National Assembly:
kiasi ya kufika trilioni. Katika hii trilioni, raslimali ngapi tumetenga kando kwa minajili ya wale waliopigania Uhuru wa taifa hili? Hawa mashujaa wamekuwa masikini kuliko masikini wengine wote. Watoto wao na wajukuu wao wako katika hali mbaya. Tumetenga pesa gani kulinda haki ya wale mashujaa wachache waliopigania Uhuru wa Kenya? Badala yake, tunaraukia kitendawili kila asubuhi ambacho hakiweki ugali mezani. Kwa aibu kubwa, Wakenya wameenda Ethiopia kuleta mtu anayeitwa Elema Ayanu, ambaye ni “ndugu” yangu. Yeye ni Oromo. Mimi naye tunaongea lugha moja. Kama atakuwa shujaa, atakuwa shujaa Ethiopia sio Kenya. Angalia wale mashujaa ambao tuko nao humu nchini, wako ...
view
-
29 Jun 2016 in National Assembly:
Kwetu kuna shule ya upili ya Mau Mau. Mashujaa 11 waliuawa pale. Kwa minajili ya kutambua juhudi yao, tumejenga shule ya upili pale angalau historia na damu yao isiende bila kutambulika. Wakati umewadia wa kuhifadhi kumbukumbu na kuweka makavazi haya ili watoto wetu wajue historia. Mchakato wa Uhuru wa Kenya ulianza Kamukunji. Uhuru wa pili ulianza Kamukunji. Kama nilivyosema, dhalimu yeyote akija, Kamukunji iko na tutapambana naye.
view
-
29 Jun 2016 in National Assembly:
Leo mimi ni muungaji mkono mkubwa wa Rais Uhuru Kenyatta. Tumetoka mbali. Tulipigwa na vitoa machozi kama vile majuzi watu walipigwa hapa. Wakati wetu, tulipigwa na tukavumilia tukitetea Kenyatta International Convention Centre (KICC). Mimi na Rais Uhuru Kenyatta tulipigwa na vitoa machozi lakini wengine leo wanaona ni ajabu watu wengine kupigwa na vitoa machozi. Hivi ni vitu ambavyo ni lazima tuvumilie wakati tuko kwa Upinzani. Kwa hivyo, nasimama nimpe kongole ndugu yangu, Mhe. Yusuf.
view
-
29 Jun 2016 in National Assembly:
Naunga mkono Hoja hii kwa sababu ninapenda kumbukumbu na historia ya taifa ya Kenya.
view
-
22 Jun 2016 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipa hii fursa ili niweze kuchangia Hoja hii. Kabla ya hapo, ningependa kuleta suala la kisheria mbele yako. Kama Wabunge, kifungu cha Saba cha Katiba ya Kenya kinasema kuwa lugha ya taifa ni Kiswahili. Lugha rasmi ya Kenya ni Kiswahili. Unapoangalia Kanuni za Bunge, kifungu cha 77, kinasema kuwa maongezi yote yanayoongewa hapa yaongewe kwa Kiswahili. Sisi tunaoenzi lugha hii tuna matatizo wakati tunafanya utafiti kwa Hoja ambazo zinaletwa mbele yetu. Tumeomba Bunge mara kadha wa kadha itupe Kanuni za Bunge kwa lugha ya Kiswahili ili tuchangie Hoja zinazoletwa hapa Bungeni. Kuzungumza kwa Kiswahili si ...
view
-
22 Jun 2016 in National Assembly:
Najua vile mtu aliyeuawa anasikia lakini kutangaza wizi wa mifugo janga la kitaifa, ni kupoteza njia. Ningependa kumwambia Mhe. Cheptumo aangalie Uganda iliyokuwa na matatizo kama hayo. Mhe. Museveni alituma jeshi kule. Matatizo haya mengi yamezidi katika eneo la Elemi Triangle katika Bara Afrika. Elemi Triangle inamilikiwa na jamii moja. Ikiwa ni sehemu ya Ethiopia, South Sudan au Kenya, watu wanaoishi Elemi Triangle ni jamii moja. Haya ni masuala ya mila. Mila ya kishenzi; mila ya dhuluma na mila isiyotambua mali wala maisha ya mwanadamu. Tutachukua hatua gani kama Serikali kuhakikisha mila hii ya dhuluma na ushenzi imesimamishwa? Ukisema tuitangaze ...
view
-
8 Jun 2016 in National Assembly:
Thank you very much for giving me this opportunity, Hon. Temporary Deputy Speaker. On my behalf and that of the people of Bura Constituency, my I take this opportunity to wish the House and the nation Ramadhan Kareem. That said and done, it is wrong to anchor the existence and practices of a structured ranking of schools and candidates in a statute law. I am saying so because Article 204(2) of the Constitution has appreciated different stages and levels of development that our country is in today. It went ahead to giving remedy in terms of giving the Equalisation Fund ...
view
-
8 Jun 2016 in National Assembly:
measure performance of students for a country which has different levels of development. That rule is not fair. There is another issue that I want to share. There have been different consultants at different levels. There is the Omingo Report on Education of 1974; the Koech Report of 1980s and the United Nations Development Programme’s (UNDP) 2002 Report. They all raise a red flag in terms of Arid and Semi-Arid Lands (ASALs) and children of pastoralists. Key issues in this Report are enrolment and retention rates. We are at the very basic. Educational issues of enrolment and retention have not ...
view
-
14 Apr 2016 in National Assembly:
Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii ili niweze kuchangia Hutoba ya Rais kwa taifa. Vifungu vya 10, 32 na 240 vya Katiba vinampa Rais mamlaka kuzungumza na taifa kutoka Bunge la Taifa. Ni sikitiko na aibu wakati Waheshimiwa wa Bunge wakijua Rais anakuja kutekeleza wajibu wa kikatiba wanampokea na kumpigia firimbi. Tunasema hii ni aibu na tunailaani vikali.
view