All parliamentary appearances
Entries 491 to 500 of 612.
-
16 Jul 2013 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Speaker, I beg to move the following Motion:-
view
-
11 Jul 2013 in National Assembly:
Mhe. Spika, mimi ni mwanachama wa Kamati ya Uchukuzi na Ujenzi na Makazi. Jana tulikuwa na kikao na Waziri anayehusika na masuala hayo. Kilichoibukwa kwenye kikao hicho ni kwamba hakuna sheria inayomuruhusu kuchukua pesa za barabara na kuzipeleka kwa serekiali za kaunti. Kwa hivyo, kama Kamati, tuliketi na kulizungumzia jambo hilo. Waziri aliomba muda. Kufikia Jumatatu ijayo, ataleta jawabu lakini hakikisho ni kwamba ni kinyume cha sheria kupeleka pesa za barabara kwa magavana, mpaka Bunge litakapobatilisha sheria iliyopo. Sheria ya Roads Levy Fund bado inatumika. Hadi sheria hiyo itakapobatilishwa, ni lazima pesa za barabara ziende kwa maeneo Bunge. Ahsante, mhe. ...
view
-
26 Jun 2013 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika kwa fursa hii. Ningependa kumpongeza Mhe. Gatobu kwa kuleta Hoja hii hapa.
view
-
26 Jun 2013 in National Assembly:
Ilivyozungumziwa mara nyingi, Kifungu 53(1)(b) kinatoa kwa uzito haki kwa kila mtoto kupata elimu, na kinasema kwamba ni lazima. Bunge litakapopata fursa ya kutekeleza Kifungo hicho cha Katiba, ni bora itafute ni vipi itawasaidia wale watoto.
view
-
26 Jun 2013 in National Assembly:
Katika Hotuba ya kwanza ya Rais wa Taifa hili, Baba wa Taifa Mzee Jomo Kenyatta alitoa changamoto tatu kubwa ambazo ni umaskini, kutojua kusoma na kuandika na maradhi. Ni kwa nini kutoka miaka 50 iliyopita mpaka leo hatujapata zuluhisho la matatizo haya? Tunapozungumzia kuhusu elimu ya watoto, elimu ya watoto wanaoishi katika sehemu kame ni nadharia. Ikiwa watoto wa Kenya wana matatizo, watoto wa kutoka sehemu kame ya Kenya au watoto wa wafugaji wana matatizo mara kumi ukilinganisha na watoto wale wengine. Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu watoto wa wafugaji ni watoto ambao wanategemea mazingara. Ikiwa kumenyesha na ...
view
-
26 Jun 2013 in National Assembly:
Hoja hii inazungumza juu ya mtoto mwelevu. Watoto welevu ni tegemeo la taifa lolote. Kama watoto welevu ni tegemeo la nchi hii katika siku za uzoni, lazima kuwe na mikakati. Tuna pesa ngapi katika kila sehemu ya uwakilishi Bunge kuwawezesha watoto hao kusoma? Nasikitika kwamba katika sehemu ninayotoka hasa Boka, Ilimani na Asa, mpaka leo, watoto hawapati fursa ya kupata manufaa ya elimu ya kawaida.
view
-
26 Jun 2013 in National Assembly:
Kwa hivyo, naunga Hoja hii mkono ilivyorekebishwa ili watoto kutoka jamii maskini waweze kupata elimu kama watoto wengine.
view
-
5 Jun 2013 in National Assembly:
Asante, Bw. Spika. Ninachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu. Bunge, kama chuo ama taasisi, inafikia upeo siku kama leo wakati tunafanya maamuzi ya kihistoria. Wakati kiongozi wa wachache anapendekeza fulani awe Waziri, kwa hakika Bunge linafika upeo wa demokrasia.
view
-
5 Jun 2013 in National Assembly:
Bw. Spika, Kipengele cha 152(2) cha Katiba ya Kenya kimetoa mamlaka ya kuteuliwa kwa Mawaziri. Kipengele cha 204(4) cha sheria ya Bunge kinakubalia ile kamati inayoamua iwapo aliyependekezwa na Rais anafaa kuwa Waziri au hafai. Mimi ninafuraha tofauti na wengine. Furaha yangu inatokana na mambo mawili. Nimefurahi, kama mfugaji. Kwa upande wa ufugaji, niko na ole Lenku. Pili, nimefurahi kama Mpwani. Kama Mpwani, niko na mhe. Kazungu Kambi. Kwa nini nimefurahi? Ni watu wachache kutoka Mkoa wa Pwani waliosimama kidete kuiunga mkono Serikali ya Jubilee. Mimi, nikiwa miongoni mwa wale wachache, sikusikitika wala kujuta kwa kumchagua Uhuru Kenyatta kama Rais ...
view
-
5 Jun 2013 in National Assembly:
Hii ndiyo fursa yangu ya pekee, na ninaichukua kumwambia mhe. Uhuru Kenyatta ni ahsante.
view