All parliamentary appearances
Entries 501 to 510 of 612.
-
5 Jun 2013 in National Assembly:
Katika ukurasa wa saba wa hii Ripoti, utaona kwamba Kamati inasema wateuliwa hawa hawana visa vya ufisadi na wamelipa kodi. Wamesafishwa. Ni kwa nini wasipewe zawadi? Kama wewe huhusiki na ufisadi, na unalipa kodi kila siku, unastahili kupewa bendera uende nayo nyumbani.
view
-
5 Jun 2013 in National Assembly:
Bw. Spika, kuna jambo ambalo ningependa kumuomba mhe. ole Lenku aliangazie. Kwa nini? Kuna akina mama waliozaa watoto wanne ama watano katika sehemu fulani humu nchini, ambao mpaka sasa bado hawajapata vitambulisho. Akina mama hao wanapatikana katika sehemu ya Hirimani, katika eneo Bunge la Bura. Ninamwomba mhe. ole Lenku aliangazie suala la utoaji vitambulisho kwa Wakenya, ndio shughuli hiyo ifanywe kwa njia ya haki na usawa kwa Wakenya wote.
view
-
5 Jun 2013 in National Assembly:
Janga kubwa linaloiathiri jamii katika eneo la Pwani ni matumizi ya madawa ya kulevya. Ninamwomba ole Lenku ayaangazia masuala ya ulanguzi wa madawa ya kulevya kwa dhati zaidi, ili watoto wetu warudi katika utu na ubinadamu.
view
-
5 Jun 2013 in National Assembly:
Kuna mzozo unaotokota hivi sasa. Serikali imetoa amri operesheni ifanywe. Operesheni hiyo inafanywa katika Taita Ranches. Ng’ombe 80,000 wa wafugaji wako katika Taita Ranches. Kwa bei ya soko leo, thamani ya ng’ombe hao ni kati ya Ksh3.5 billion na Kshs4 billion, lakini Serikali iko tayari kwenda huko na helikopta na kuwafukuza ng’ombe hao. Bw. Spika, wafugaji walienda mahakani wakapewa court order inayoiamrisha Serikali kusitisha operesheni hiyo, lakini Serikali imekataa kutii amri ya mahakama. Tulianzia kwa ofisi ya Katibu wa Kudumu, tukateremka chini lakini amri ya mahakama ilikataliwa. Je, wafugaji wanadhulimiwa kwa sababu wao ni Wasomali? Wanadhulumiwa kwa sababu wao ni ...
view
-
4 Jun 2013 in National Assembly:
Ahsante Mheshimiwa Spika, nimesimama kwa hoja ya nidhamu. Natumaini umesikia Mheshimiwa aliyezungumza mbele yangu akisema mwenendo wa mataifa ya Kiafrika umeongozwa na nchi za Kiafrika zisizokuwa na rekodi nzuri ya haki za binadamu. Je, Mh. Spika, Bunge hili au mwanachama yeyote wa Bunge hili anaruhusiwa kuzungumzia ubaya wa nchi jirani yetu? Ahsante Mhe. Spika.
view
-
4 Jun 2013 in National Assembly:
Ahsante Mheshimiwa Spika, nimesimama kwa hoja ya nidhamu. Natumaini umesikia Mheshimiwa aliyezungumza mbele yangu akisema mwenendo wa mataifa ya Kiafrika umeongozwa na nchi za Kiafrika zisizokuwa na rekodi nzuri ya haki za binadamu. Je, Mh. Spika, Bunge hili au mwanachama yeyote wa Bunge hili anaruhusiwa kuzungumzia ubaya wa nchi jirani yetu? Ahsante Mhe. Spika.
view
-
28 May 2013 in National Assembly:
Ahsante sana Naibu Spika. Nachukuwa fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu na wewe kwa fursa hii. Naipongeza Kamati ambayo ilifanya utafiti na kuleta Hoja hii muhimu mbele yetu.
view
-
28 May 2013 in National Assembly:
Naibu Spika, Katiba hii inalinda haki za wanyama pia. Lakini wanyama hawasomi Katiba! Wale ambao walikuja na kuchinjia wanyama Langoni mwa Bunge, ningewaalika kabla hawajachinja nguruwe wasome Katiba kwanza.
view
-
28 May 2013 in National Assembly:
Katika Kifungu 94 (1) cha Katiba ya Kenya kinatoa mamlaka ya kipekee itakapokuja kwa maswala ya utunzi wa sheria. Si Utawala ama Mahakama. Ni Bunge lenye mamlaka ya kutunga sheria.
view
-
28 May 2013 in National Assembly:
Hatutaomba msaada kwa Tume ya Sarah Serem kutusaidia kama Wabunge kututungia Katiba ambaye haiambatani na vifungu vya Sheria ya nchi hii.
view