All parliamentary appearances
Entries 521 to 530 of 612.
-
14 May 2013 in National Assembly:
Ukisoma kifungo cha 152(3), kinasema Bunge lisihusike katika kuteuliwa kwa mawaziri watakao endesha shughuli ya kitaifa. Hii ni historia kubwa ambayo ninafuraha nikisimama hapa leo kuchangia Hoja hii.
view
-
14 May 2013 in National Assembly:
Bi. Naibu wa Spika, hii ni heshima kubwa kwa taasisi ya Bunge na Wabunge. Mawazo ni tofauti. Baadhi yetu wanasema kwamba asilimia fulani ya Mawaziri wateule wanatoka mkoa fulani na asilimia fulani wanatoka mkoa mwingine. Lengo na maudhui ya kubuni Serikali ni kuhudumia wananchi. Inafaa wale wanaoleta hoja hii wakumbuke kwamba Serikali iliyopita ilikuwa ya sehemu mbili za nchi hii. Zaidi ya asilimia 50 ya Mawaziri wa Chama cha ODM walitoka Mkoa wa Nyanza. Kwa nini wakati huo wenzetu hawakushangaa? Mbona leo wanaona ajabu?
view
-
14 May 2013 in National Assembly:
Bi. Naibu wa Spika, silipotoshi taifa. Prof. Anyangâ-Nyongâo hatoki eneo la Pwani. Mhe. James Orengo hatoki eneo la Kaskazini Mashariki. Mimi sipotoshi Bunge. Nazungumza nikijua kilichotokea. Kwa hivyo, nataka kumuomba mheshimiwa aangalie idadi ya Mawaziri---
view
-
14 May 2013 in National Assembly:
Ahsante, Bi. Naibu wa Spika. Nikiendelea, lengo letu si kuangalia ni mkoa upi umewakilishwa kwenye Baraza la Mawaziri. Lengo letu ni kuona jinsi huduma ya Serikali itakavyomfikia Mkenya popote alipo, bila ya kujali kama anatoka eneo la Tana River, Kaskazini Mashariki ama Nyanza. Lengo na maudhui yetu---
view
-
14 May 2013 in National Assembly:
Ahsante, Bi. Naibu wa Spika. Mamlaka ya kuajiri Mawaziri ni mamlaka ya Utawala. Si mamlaka ya Bunge. Kazi yetu ni kuunga mkono ama kukosoa yanayopendekezwa.
view
-
14 May 2013 in National Assembly:
Nikiendelea kuzungumzia tunayojiuliza leo kwa mara ya kwanza, haswa nikizingatia kwamba baadhi yetu wanasoma vipengele fulani vya Katiba kwa sababu vilema hawamo kwenye ratiba ya walioteuliwa; nakiri kwamba kwa sasa vilema hawamo kwenye ratiba ya walioteuliwa kuwa Mawaziri lakini uteuzi huo bado haujakamilika. Hivi sasa, tunawakagua wateule 14 lakini Katiba imeruhusu kuteuliwa kwa Mawaziri wasiozidi 22. Kwa hivyo, hii ni shughuli ambayo bado inaendelea.
view
-
14 May 2013 in National Assembly:
Bi. Naibu wa Spika, nimefurahi sana kuichangia Hoja hii kama ilivyo kwa sababu---
view
-
14 May 2013 in National Assembly:
Bi. Naibu wa Spika, nimesikia lakini neno âkilemaâ na âwalemavuâ lina maana sawia. Sidhani kama mhe. Mwaura anaweza kunifunza Kiswahili.
view
-
14 May 2013 in National Assembly:
Ahsante, Bi. Naibu wa Spika. Sisemi hivyo kwa sababu ya kuonyesha madharau kwa walemavu. Namuomba msamaha ndungu yangu Mwaura na walemavu wote nchini Kenya. Natumai mhe. Mwaura amefurahi.
view
-
14 May 2013 in National Assembly:
Bi. Naibu wa Spika, nikiendelea, lengo na maudhui yetu ya kuangalia uteuzi wa Mawaziri hivi leo ni kutoa huduma kwa nchi ya Kenya. Nimetoka katika sehemu ya Tana River. Tunavyozungumza, barabara zimekatika katika sehemu hiyo. Zaidi ya watu 10,000 hawana makao. Je, tutamkimbilia nani kwenye ofisi ya Wizara husika kuomba usaidizi ili wakazi wa sehemu hiyo wapate huduma? Mizozo imeibuka kwenye kila pembe ya nchi hii. Ni vipi tutapata Waziri haraka atoe huduma inayostahili ili tupunguze ukabila na siasa za vyama? Tunataka tupate Mawaziri ili watoe huduma kwa Wakenya kwa sababu wao hawatakwenda kuuliza ni nani anayetoka Nyanza ama Pwani. ...
view