Bady Twalib Bady

Parties & Coalitions

Born

1st May 1974

Email

badibadi94@yahoo.com

Telephone

0722346475

All parliamentary appearances

Entries 151 to 160 of 177.

  • 23 Feb 2016 in National Assembly: Jambo lingine ambalo ningependa kulizungumzia ni ufisadi na usimamizi mbaya wa viwanda hivi. Ninataka kusisitiza kwamba hizi ndizo sababu ambazo zinaleta shida. Tunastahili kujua ni kwa nini viwanda vyetu vinaanguka, na ni shida gani zinazoikumba sekta ya sukari. view
  • 23 Feb 2016 in National Assembly: Mhe. Spika, ni vyema kuona kamati tekelezi ikifuatilia suala hili na kuhakikisha kwamba Ripoti hii imetekelezwa kikamilifu na kwa wakati unaofaa. Tumeona kamati nyingi zikiwasilisha Ripoti zao Bungeni lakini Kamati Tekelezi haifuatilii na kuhakikisha kwamba ripoti hizo zinatekelezwa vilivyo. Tunajiuliza ni kwa nini viwanda vya sukari vinaanguka nchini Kenya? Hatuzungumzii kiwanda cha sukari cha Mumias peke yake bali tunazungumzia kiwanda cha sukari cha Ramisi, na kiwanda cha nyama cha KMC kule Mombasa, ambacho kiko katika constituency yangu. Tunasikitika kwamba viwanda hivi vinaendelea kuanguka badala ya kuimarika. Vinatusababishia matatizo makubwa. Bidhaa hii adimu, ambayo watu wanataka kuitumia, haitatumika kwa sababu kuna ... view
  • 23 Feb 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii na mimi nichangie Ripoti hii ya Maadili ya Kitaifa na Sera za Utawala. Hii iko katika Kipengee cha Kumi cha Katiba yetu ya Kenya. Ningependa kusema kuwa katika Ripoti hii yako mengi ambayo yametokea. Tumeona ugatuzi umetusaidia. view
  • 23 Feb 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kama nilivyosema, ugatuzi umetusaidia sana katika nchi yetu ya Kenya lakini ufisadi bado umekithiri katika sehemu nyingi. Ni lazima tulishughulikie jambo hili vilivyo kama Serikali ili tuwe na maadili mema ya kujimiliki katika nchi hii. Pia, bado hakuna usawa wa kijamii katika kumiliki afisi nyingi sana katika nchi hii. Kuna kelele nyingi sana kutoka kwa jamii nyingi ambazo ni dogo. Kwa mfano, jamii yangu ya Wajomvu ni dogo sana katika nchi hii lakini inatambulika katika makabila ambayo yako hapa nchini. Bado makabila madogo kama haya hayajazingatiwa vilivyo. Pia, ningependa kuunga mkono mwenzangu, Mhe. ... view
  • 23 Feb 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii tena kuchangia Ripoti hii. Kusema kweli, katika nchi yetu ya Kenya, kuna mambo mengi ambayo tumefanya ya kimataifa, jambo moja likiwa ni lile Kongamano la Biashara ambalo lilifanyika katika ukumbi wetu wa Kenyatta International Conference Centre (KICC), Nairobi. Pia, ni muhimu sana kuona kuwa katika yale mambo ya kimataifa ambayo tunajihusisha nayo, tunapaswa tuhusike sana kama vile ndugu yetu, Mhe. Katoo, ameeleze kuhusu mambo ya Afrika Mashariki. Tunafaa kuangalia yale ambayo yanaendelea katika Afrika Mashariki. Tukiwa nchi ambayo imekomaa, tunaona kuwa kuna shida nchini Burundi na tunafaa kujiuliza nchi ... view
  • 23 Feb 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu wa Spika wa Muda, singependa kutumia muda mrefu. Ninaona zimebaki dakika tano peke yake. view
  • 23 Feb 2016 in National Assembly: Kwa hayo machache, ninaunga mkono. view
  • 1 Apr 2015 in National Assembly: Asante sana mhe Spika kwa kunipatia fursa hii ili nami nichangie Hotuba ya Rais. Kwanza, ningependa kumpongeza Rais kwa Hotuba yake ambayo aliweza kutoa. Kulingana na Hotuba yake alizungumzia upanuzi wa bandari yetu ya Mombasa. Alisema hivi sasa inafikia kituo cha 19 na yuko katika mipangilio ya kuongeza vituo vya 20 na 21. Nikiwa Mbunge wa pale Jomvu, nasema kuwa katika kupanua bandari hiyo bila kupanua miundo msingi itakuwa ni shida kwa sababu ya msongamano mwingi. Ndani ya bandari ile ya Mombasa kutoka vituo vilipokuwa tano na sita, barabara zilikuwa ni hizo hizo. Leo mhe Rais anazungumzia vituo 19, 20 ... view
  • 1 Apr 2015 in National Assembly: Asante sana mhe Spika kwa kunipatia fursa hii ili nami nichangie Hotuba ya Rais. Kwanza, ningependa kumpongeza Rais kwa Hotuba yake ambayo aliweza kutoa. Kulingana na Hotuba yake alizungumzia upanuzi wa bandari yetu ya Mombasa. Alisema hivi sasa inafikia kituo cha 19 na yuko katika mipangilio ya kuongeza vituo vya 20 na 21. Nikiwa Mbunge wa pale Jomvu, nasema kuwa katika kupanua bandari hiyo bila kupanua miundo msingi itakuwa ni shida kwa sababu ya msongamano mwingi. Ndani ya bandari ile ya Mombasa kutoka vituo vilipokuwa tano na sita, barabara zilikuwa ni hizo hizo. Leo mhe Rais anazungumzia vituo 19, 20 ... view
  • 1 Apr 2015 in National Assembly: mabalozi wa Nyumba Kumi na pia wahudumu wa afya ambao tunawaita CommunityHealth Workers, kwa ile kazi nzuri ambayo wanafanya na hawapati malipo fulani. Kuhusu mambo ya ufisadi, nampongeza Rais kwa ile hatua ambayo amechukua kijasiri. Lakini kitu ambacho ningependa kusema ni kwamba kabla wale ambao wametajwa hawajaweza kutajwa, ilikuwa ni lazima uchunguzi kamili ufanyike. Kwa shauri tukiangalia katika hii Hotuba ya Rais na Ripoti ambayo tumepata kutoka kwa Tume ya Ufisadi--- Nikizungumzia tu kuhusu Kaunti yangu ya Mombasa, Gavana wa Kaunti yangu Ali Hassan Joho, naona ametajwa na tuhuma kuhusu soko. Soko hilo halikutajwa kuwa yeye amelinyakua, lakini limetajwa kuwa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus