2 Mar 2016 in National Assembly:
Ningependa kusema ya kwamba Mswada huu umetambua walemavu, akina mama na jamii ya watu wadogo wadogo yaani marginalised community kuwa ni lazima wapate haki sawa sawa. Katika kipengele cha 31 cha Mswada huu, kinasema kuwa kila mmoja ana haki sawa ya kumiliki ardhi katika ardhi za kijamii. Kwa hivyo, Mswada huu unawapatia nguvu wale wakaaji ama wenyeji ambao wako katika ardhi hizo katika maamuzi yoyote yanayotaka kufanyika katika ardhi hizo. Vile vile, tunaona kuwa ikiweza kufanya hivyo, itaweza kutoa nguvu kuwa jambo lolote, hata likiwa ni la kuekeza, watu wenyewe washauriwe halafu kisha baada ya kuweka maamuzi, ndio tuone kwa ...
view
2 Mar 2016 in National Assembly:
Jambo kama hili mimi binafsi limenifurahisha nikiwa Mbunge wa Jomvu kwa ajili kuna sehemu kadhaa katika sehemu yangu kama vile Aldina, Maganda na sehemu nyingine za Bangladesh, KCC na Ganahola. Tukiangalia katika sehemu ya Aldina, wenyeji walikaa hapo takribani tangu Kenya haijapata Uhuru. Vile vile, Tume ya Kuchunguza Mambo ya Ardhi -
view
2 Mar 2016 in National Assembly:
- ilikwenda pale. Waliweza kuweka jopo na wakasema yule anayedai kuwa mahali pale ni pake ajitokeze. Hawakujitokeza.
view
2 Mar 2016 in National Assembly:
Huu Mswada unatupa nguvu kuona kuwa wale mabwenyenye ambao wanakuwa na makaratasi ya kumiliki ardhi na wenyeji wakiwa wanaishi mahali hapo hapo, itaweza kuwapokonya nguvu. Pia, nikiangalia hali hii ya wenyeji, ni lazima wahusishwe. Ni muhimu kwa shauri nikiangalia mradi mkubwa sana wa reli unaofanyika, watu katika sehemu yangu ya Maganda, ambapo inapitia walipewa makaratasi, yaani allotment letters kusubiri hati miliki zao. Unaona mradi ule unafanyika, mtu anapigiwa hesabu za nyumba yake, lakini hapigiwi hesabu ya ardhi. Jambo kama hilo si jambo la sawa sawa. Ni muhimu sana watu watambue wenyeji na wawapatie hati miliki za ardhi ili ziwafanye kuwa ...
view
2 Mar 2016 in National Assembly:
Naunga mkono Mswada huu na nampongeza ndugu yangu Mhe. Alex Mwiru na Kamati yake yote ya Ardhi kwa kufanya kazi na kuleta mambo ambayo tunayazungumzia katika Bunge hili leo. Kwa sababu zamani tulikuwa tunawaita “walala hoi”, sasa tutawaita “walala hai” kwa shauri watakuwa na ukweli wa kuona watakuwa na haki ya kumiliki ardhi katika seheme zao.
view
2 Mar 2016 in National Assembly:
Tukiangalia, kuna wale wa jadi. Kama sehemu yangu, kuna sehemu inaitwa Kwa Shehe. Wenyeji wa pale walitoka sehemu ambazo hazijapimwa na mpaka leo, wanalipa malipo ya ardhi katika kaunti. Jambo hili si la sawa sawa. Ni muhimu wenyeji kupewa hati miliki za ardhi.
view
2 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuunga mkono Mswada huu, lakini kuna mambo ambayo nayapinga. Napinga Kipengee cha 35, ambacho kinasema kwamba mtu akiwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
2 Mar 2016 in National Assembly:
amechukua ardhi ya mtu mwingine kabla ya kupitishwa kwa Mswada huu, mtu yule ndiye atakayetambuliwa, baada ya kupitishwa kwa Mswada huu, kuwa mwenye ardhi hiyo. Nasema vizuri sana kwamba tutaupiga msasa Mswada huu, ili tuone kwamba waliochukua ardhi za wenyewe kabla ya Mswada huu---
view
24 Feb 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia fursa hii nami nichangie Mswada huu. Kwanza, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu ni mzuri. Mswada huu utampatia nguvu Msimamizi wa Bajeti katika kufanya kazi yake. Kipengele cha 226 cha Katiba yetu ya Kenya kimeonyesha wazi wazi Msimamizi wa Bajeti na jinsi majukumu yake yanavyostahili kufanywa. Katika Mswada huu, tumeona kuwa kazi kubwa ya Msimamizi wa Bajeti ni kuhakikisha kuwa pesa zote ambazo zinakusanywa kutoka kwa umma zimepangwa kwa njia sawa na kutumiwa kwa hali ambayo zimepangiwa. Katika Bunge hili, ni bora kuhakikisha kuwa afisi ya Msimamizi wa Bajeti imepewa nguvu. Ili afisi ...
view
23 Feb 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia fursa hii ili niichangie Ripoti hii. Kwanza, ninataka kuiunga mkono Ripoti hii inayozungumzia mambo mengi yanayohusiana na sukari katika nchi yetu ya Kenya. Kama tunavyojua, zaidi ya watu millioni sita nchini wanategemea sekta hii. Shida kubwa katika sekta ya sukari ni uagizaji wa sukari kutoka nje. Hili ni jambo ambalo linavifanya viwanda vyetu kuvurugika ama kutoendelea vizuri.
view