Bady Twalib Bady

Parties & Coalitions

Born

1st May 1974

Email

badibadi94@yahoo.com

Telephone

0722346475

All parliamentary appearances

Entries 131 to 140 of 177.

  • 23 Mar 2016 in National Assembly: Mambo ya saratani ni mambo ambayo yamesumbua wananchi wengi wa Kenya. Ninavyozungumza, mimi binafsi katika ofisi yangu pale mashinani, nina mmoja wa wafanyikazi wangu anayeugua saratani ya matiti. Ilituchukuwa karibu miaka miwili kumfanyia Harambee mpaka akatolewa lile titi na akawekwa lile titi bandia. Jambo hili ni la kusikitisha kwa sababu yeye aliwapata watu wa kumfanyia Harambee lakini wengine wasio na uwezo wa kufanyiwa mambo kama hayo, inakua ni shida. Mhe. Naibu Spika wa Muda, tunaona athari ya ugonjwa wa saratani kwa watu wengi katika sehemu nyingi nchini. Watu wakitaka kupata matibabu, mpaka waje kwa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, Nairobi. ... view
  • 23 Mar 2016 in National Assembly: kuangalia mambo ya ugonjwa wa saratani na viwekwe katika kila sehemu na nyanja ya nchi yetu ya Kenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda, zaidi, tunaona ugonjwa wa saratani unasababishwa na mambo ya vyakula. Kupitia kwa wizara inayohusika na mambo ya afya, ni vizuri kuona kuwa vyakula vinavyoingia nchini vimethibitishwa kuwa sawa. Isiwe vyakula vinavyowachiliwa kuingia nchini na kusababisha magonjwa kwa wananchi wetu. Tukiangalia hali ya kutibu magonjwa ya saratani, imekuwa hali ngumu kwa sababu wagonjwa waathiriwa wanapokuja Nairobi, inabidi watafute pesa za kutibiwa kwa kila hatua ya matibabu. Wengi wao hufuata viongozi kama sisi na kuwaambia wanatakiwa kufanyiwa matibabu hospitali ... view
  • 3 Mar 2016 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu wa Spika. Kama nilivyoeleza jana, jambo la ardhi likitajwa, takribani watu asilimia 80, watu wa Pwani tukiwemo, huguswa kwa njia moja au nyingine. Kipengee cha 31 kinaweka haki sawa ya kutambua akina mama na jamii za watu wanyonge tunaowaita kwa lugha ya kimombo “marginalized communities”. view
  • 3 Mar 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu wa Spika, siku zinazofuata, wakati tutakapokua tukiupiga msasa Mswada huu, tutataka kurekebisha Vipengele vya 35 na 46 kwa sababu vinatoa mwanya kwa mabwenyenye kunyemelea ardhi ambazo ni za jamii inayokaa katika sehemu hizo. view
  • 3 Mar 2016 in National Assembly: Tumefurahishwa na Mswada huu, lakini pia nikiangalia, sisi tulipitisha Katiba ya Kenya, 2010 tukiihusisha Tume ya National Land Commission (NLC) na masuala ya ardhi. Kutoka kwenye ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho wa Mswada huu, sijaona NLC ikihusishwa. Ni muhimu mchango wa tume hiyo uonekane ili waweze kutusaidia. view
  • 3 Mar 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu wa Spika, kule kwetu Pwani, watu wanakaa miaka mingi, na ukimuuliza mtu anaishi wapi, atakuonyesha kaburi ya babu aliyemzaa babu yake. Kwa hivyo, Mswada huu utatufanya sisi kama viongozi kuwa daraja ya watu wetu na Serikali, na tutahakikisha kwamba Serikali imewapatia hati miliki. view
  • 3 Mar 2016 in National Assembly: Kama ulivyozungumza hapo awali, kule kwetu Pwani kuna sehemu inayoitwa Maganda. Kwa sasa wakazi katika sehemu hiyo wako na allotment letter, lakini watu hawajapatiwa hati miliki ilhali mradi mkubwa wa Serikali unapita huko. Watu hao wanaambiwa kwamba wanafanyiwa hesabu kulingana na nyumba zao, lakini si kulingana na ardhi ambayo wanamiliki pale. Kuidhinishwa kwa Mswada huu kutawapatia wenyeji hao fursa ya kusikika na waweze kumiliki ardhi hiyo. view
  • 3 Mar 2016 in National Assembly: Vile vile, tukiangalia sehemu za Aldina, Ganahola na sehemu nyingi za eneo Bunge langu, tutapata kwamba kuna matatizo kama hayo. Jambo zuri ambalo ningependa kulisema ni kuyataja yale mambo ambayo ndugu yangu Mhe. Wesley Korir aliyazungumzia jana. Wengi wa mabwenyenye wanahamia kwenye sehemu wanakoishi jamii. Unamwona mtu ako na karatasi ya hati miliki lakini ukimuliza mahali anakuja kumiliki hata hajui. Kwa hivyo, Mswada huu ukipita utapeana haki sawa na utapeana haki za zile jamii ambazo zinaishi katika sehemu zao zisikizwe kwa jambo lolote ambalo litafanyika. Ninasema hivi kwa sababu katika eneo langu la Jomvu na Pwani nzima, shida za ardhi ... view
  • 3 Mar 2016 in National Assembly: Mwisho kabisa, ninapongeza Kamati ambayo imefanya kazi hii. Wametutoa katika lindi la shida na waliokuwa wanajiita walala hoi sasa watakuwa walala hai. Kwa hayo machache, Mhe. Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ambayo ilikuwa imenipita lakini ukanirudisha kwa amri zako nimalize yale ambayo sikuwa nimemaliza jana. Asante, Mhe. Naibu Spika. view
  • 2 Mar 2016 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii nichangie Mswada huu. Jambo la kwanza, nataka kuunga mkono Mswada huu kwa sababu swala la ardhi, hasa kwa sisi ambao tunatoka Pwani, takribani karibu watu asilimia 80 wanakumbwa na jambo hili kwa njia moja ama nyingine. Vile vile, kwa wenzetu katika jamii ya wafugaji, jambo hili linawakumba. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus