3 Aug 2016 in National Assembly:
Ningependa kusema kuwa ni muhimu tuipatie Kamati hii nguvu na tuichukue Ripoti hii kwa vifua vyetu ili tuelimishe wananchi walio mashinani kuhusu sheria ambayo tumepitisha na kuwaeleza haki zao. Ni sharti tuunge mkono Kamati hii ili tukimbie pamoja panapo matatizo na wananchi wetu watakuwa sawa. Kwa niaba ya wananchi wangu wa eneo Bunge la Jomvu, ningependa kurudisha shukrani na pongezi kwa juhudi za Kamati ya Ardhi kwa kazi nzuri iliyofanya katika eneo Bunge langu na sio tu kwa kuzungumza hapa Nairobi, lakini kwa kuzunguka eneo lote.
view
2 Aug 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nami pia niunge mkono Mhe. Mwadime. Kitu ambacho ningependa kutofautiana na Mhe. Ali Wario ni kwamba Sheria iko, lakini tetesi huja baada ya ile sheria iliyowekwa kuwa haitumiki. Hi indio maana watu wa pale huweka tetesi ili waone namna wanaweza kusikizwa. Kwa hivyo, ni vizuri vile Mbunge waVoi Mhe. Mwadime amezungumzia juu ya tetesi za wanyama pori ili kuhakikisha kuwa Serikali imepeleka maofisa wakutosha kwa hizo mbuga za wanyama. Inafaa tuangalia sehemu zote ambazo ziko na shida na mambo ya wanyama wapori li ili sehemu hizo zihifadhiwe vizuri. Mhe. Spika, katika ...
view
2 Aug 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda kwa kunipata nafasi hii nichangie. Mimi pia napinga kwa sababu ambazo Mhe. (Bi.) Mwenyekiti ametoa. Naziunga mkono na pamoja twapinga. Ahsante.
view
2 Aug 2016 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mimi pia nachukua fursa hii kuunga mkono Ripoti hii. Tumeona kuwa hali ya mazingira ni muhimu sana katika hali ya maisha ya mwanadamu. Vile vile, tunaona ya kuwa katika mambo haya ya mazingira na ya misitu, kuna mambo mengi ambayo yanasababishwa na mambo haya kama vile vitega maji. Maji ni muhimu katika kila sehemu ya nchi hii. Bila maji, hatuwezi kupata njia ya kukuza vyakula vyetu na mambo mengine. Vile vile, ningependa kusema kwamba nimeunga mkono Ripoti hii na marekebisho yote ya Seneti. Pia, nampongeza mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Amina, kwa kazi nzuri ...
view
2 Aug 2016 in National Assembly:
Kwa hivyo, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili nami nichangie katika Ripoti hii na kumpongeza Mhe. Amina kwa kazi nzuri aliyoifanya. Asante sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
13 Apr 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii niunge mkono Mswada huu. Kando na kuunga mkono Mswada huu ninataka kusema kuwa Wakenya wengi sana wana matumaini na benki zetu za Kenya. Lakini matumaini hayo kwa wale wanaoweka pesa zao huko yanawaletea shida. Benki nyingi sana hapa nchini Kenya hivi sasa tunaona zinamilikiwa na matapeli. Nikisema hivyo, karibuni ilikuwa Benki ya Imperial na juzi Benki ya Chase. Wananchi waliokuwa wanalia kwa sababu wameweka pesa zao huko ni wafanyi kazi wadogo. Mpaka saa imekuwa ni shida kuona kuwa pesa zao haziwezi kuwasaidia. Inasikitisha sana kuona kuwa mwananchi wa kawaida anaweza kutoka ...
view
13 Apr 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii nichangia Hotuba ya Rais. Kwanza, ninawapongeza wanajeshi wetu wa Kenya ambao wako Somalia wakifanya kazi na kuona kuwa nchi hiyo imetulia kama nchi yetu ya Kenya. Kabla ya kuchangia yale ambayo Rais alisema juzi, ningependa kurudi nyuma kidogo katika hotuba ambayo aliitoa mwaka jana akisema kuwa ataweka Kshs10 bilioni kuwalipa watu ambao walifanyiwa dhuluma za kihistoria. Ninakumbuka mwaka huo tulichangia Hotuba ya Rais na tukasema kuwa jambo hilo halitawezekana. Nilipata fursa ya kuzungumza na kusema kuwa badala ya kuweka Kshs10 bilioni kwa watu ambao wamedhulumiwa kihistoria, afadhali pesa hizo zingewekewa mabalozi wetu ...
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker, for giving me this opportunity to present a Petition on employees of Hantex EPZ Limited on unfair dismissal. I, the undersigned, on behalf of the dismissed workers of Hantex EPZ Limited, draw the attention of the House to the following:- THAT, Article 41(1) and (2) of the Constitution entitles every worker to the right to fair labour practices, fair remuneration, reasonable working conditions, right to form, join or participate in activities of a trade union and the right to go on strike. THAT, in the recent past, about 900 employees of Hantex EPZ Limited have been ...
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
THAT, the issues in respect of which this Petition is made are not pending before any court of law or any constitutional body. Therefore, your humble Petitioners pray that the National Assembly through the Departmental Committee on Labour and Social Welfare:- (i) intervenes to ensure the unfairly dismissed employees are reinstated to their jobs and their outstanding salaries paid in full; and, (ii) recommends any other measure that it may deem fit in addressing the plight of the Petitioners And your Petitioners will every pray.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Mwanzo, ningependa kumpongeza Mhe. Gladys Wanga kwa kuja na Hoja hii. Nataka niwe kwa rekodi kuwa nimeunga mkono Hoja hii.
view