21 Mar 2017 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangia hotuba ya Rais. Wakati nchi hii ilipata Uhuru, ilifanya hivyo kwa sababu ya kupigana na umaskini, ujinga na magonjwa. Leo tunavyozungumza, umaskini umezidi katika nchi hii ya Kenya. Ufisadi lazima uangaliwe kwa sababu umekuwa kama jambo la kawaida. Tunajua kuwa tunaweza kupigana na hali hii pamoja. Ufisadi si jambo ambalo linaweza kupiganiwa na mtu mmoja. Ni lazima Serikali iliyo mamlakani ifanye juhudi kuangalia vile itapigana na mambo ya ufisadi. Leo ninashangaa vile The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of ...
view
21 Mar 2017 in National Assembly:
mwenzangu Mhe. Waluke alivyozungumza hapa kuhusu Serikali. Alisema karibu miaka 26 iliyopita, hakukuwa na maji kwake na leo ameona maji ya mifereji kwake. Mimi ninatofautiana vikali kabisa kwa sababu katika kaunti yangu ya Mombasa na viunga vyake, leo tunalia hatuna maji miaka mingi baada ya kupata Uhuru. Watu wakiona maji ni kama wameona almasi. Ni juzi tu, Mhe. Rais alipokuwa Mombasa ndivyo Waziri wa maji, Bwana Eugene Wamalwa alisema anatambua jambo hili ni la kweli. Lakini watu wa Mombasa watakaa kwa miezi sita ili waende kukopa pesa ili waangalie vile watarekebisha. Miaka hii yote watu wamekua wakiteseka, tutasubiri tena miezi ...
view
21 Mar 2017 in National Assembly:
Jambo lingine ni ugatuzi. Rais hajasema ukweli wa vile hali ilivyo. Huwezi kusema kwa Bunge kuwa unaamini ugatuzi halafu ukitoka nje ya Bunge, unazuia vyombo vinavyohusiana na mambo ya ugatuzi. Ninasema hivi nikimaanisha kile kitendo kilichotokea juzi kilichompata Gavana wa Mombasa, Mhe. Ali Hassan Joho kwa kuzuiwa kuhudhuria jambo ambalo kila mmoja anajua la Kaunti. Sisi tulipitisha Katiba na tunajua kuwa huduma za ferry ziko katika kaunti. Leo hii kusema kuwa unaamini ugatuzi na vile vile kuangalia kuwa viongozi ambao wako katika mambo ya kusimamia ugatuzi unawazuia, sidhani maneno haya ni ya kweli. Ni lazima tukisema tunakunywa maji, tusiwaonyeshe tunakunywa ...
view
21 Mar 2017 in National Assembly:
Mwisho kabisa, namshukuru.
view
23 Feb 2017 in National Assembly:
Ahsante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nami niweze kuizungumzia Ripoti ya Rais. Ninaiunga mkono Ripoti hii. Ninakubaliana na Rais kwamba watu wote wanatakiwa kuishi kwa umoja. Usalama wa nchi huadhirika kwa njia nyingi. Ndiposa tunazungumzia usalama juu ya lishe bora. Tunazungumzia usalama juu ya elimu. Pia tunazungumzia usalama juu ya uadui wa nje na ndani ya nchi. Bi. Naibu Spika wa Muda, juzi wewe ulikuwa mkali sana ulipokuwa ukizungumzia hali ilivyokuwa kule Baringo. Bado, pia tunasema vilevile; kwamba, ni jukumu la viongozi walioteuliwa katika sehemu zile kuona jinsi watakavyowajibika ili kudumisha usalama katika maeneo yao, ...
view
23 Feb 2017 in National Assembly:
Ninamuona Mhe. Sakaja akipiga chini vizuri kwa kuashiria kuwa anakubaliana nami kwa sababu mkwewe na mke wake wanatoka Miritini, ambayo iko katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni. Leo mama mkwe wa Mhe. Sakaja hana maji. Kwa hivyo, ninataka Serikali ya Mhe. Uhuru Kenyatta ijue kwamba mimi niliyoko katika muungano wa National Super Alliance (NASA), ambao imeshanaswa; na ndugu yangu Mhe. Sakaja, ambaye yuko katika muungano wa Jubilee, sote tunapata shida katika sehemu hiyo. Ninaomba Rais aingilie kati aone jinsi wananchi watakavyoweza kupata maji. Mwisho, ufisadi hauwezi kuisha ikiwa vita hivi tutamwachia Rais pekee. Ni lazima tupigane vita hivi pamoja. Ni ...
view
21 Feb 2017 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa pia kuchangia Hoja hii. Nampongeza Mbunge mwenzangu, Mhe. Cheptumo, kwa kuileta Hoja hii. Serikali ina jukumu kubwa sana kuona namna gani itakavyodhibiti hali ya amani katika sehemu ya Baringo. Isiwe Baringo peke yake bali iwe ni Kenya nzima. Ningepenga kutoa mfano wa vile Mhe. Shebesh alivyosema kuhusu Mungiki . Serikali ilipoamua kuwa inataka kuiondoa, Mungiki iliweza kuondoka. Ni muhimu kwa Serikali ya Mhe. Uhuru Kenyatta na Mhe. William Ruto kusimama kidete pamoja na Jenerali Nkaissery kuona kuwa maafa haya yanayoendelea kiholela yametatuliwa. Wakati wa nyuma, tuliona watu wa Sabaot wakiahidiwa na ...
view
21 Feb 2017 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ananipotezea dakika zangu.
view
21 Feb 2017 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kusema kweli narekebisha na naomba msamaha. Nina hakika Kiswahili kilikuwa kimempita kidogo. Nikisema kwa Kiswahili sanifu, Serikali ni lazima isimame kidete kuona vipi itaweza kuweka amani. Lakini kila siku The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
21 Feb 2017 in National Assembly:
wakizungumza maneno ya kuchukua kura na hali wale wanaochukua kura wanafariki, ni kama ule mfano wa msemo unaosema hiyo ni goji kirba kirba goji yaani wanatuzungusha wakituzungusha.
view