27 Feb 2018 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili mimi pia niweze kuchangia Mswada huu. Ningependa kuunga mkono Mswada huu kwa sababu una mambo mengi mazuri kuhusu miundo msingi katika nchi yetu ya Kenya. Pili, ningependa kumshukuru Mwenyekiti wa kamati ya barabara, Mhe. Pkosing, ambaye namjua vizuri kwa utendakazi wake. Ni mheshimiwa ambaye tulifanya naye kazi katika Bunge ambalo lilipita na katika Bunge hili leo twafurahi kuwa tuko pamoja naye katika mambo haya ya barabara. Vile vile, ningependa kumtambua Mhe. Maina Kamanda ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Barabara wakati wa nyuma. Binafsi, katika Bunge la Kumi ...
view
27 Feb 2018 in National Assembly:
Mswada huu unaonyesha idara mbalimbali ambazo zinahusika na barabara katika vitengo mbalimbali. Wameweza kutenganisha barabara ambazo ni za KeNHA, KURA na vile vile zile za KeRRA ambazo zinaingia mashinani. Hilo ni wazo zuri kwa sababu mara nyingi sisi tunasumbuliwa sana huko mashinani tukiulizwa barabara fulani ziko kwenye kitengo gani. Lakini watu hawajui jinsi barabara humu nchini zimeainishwa. Wao hufikiri barabara zote ziko The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
27 Feb 2018 in National Assembly:
chini yetu sisi Wabunge ilhali kuna watu ambao ndio wahusika wakuu katika masuala ya barabara. Kwa hivyo, katika Mswada huu, tumeonyesha vitengo mbalimbali vya barabara.
view
27 Feb 2018 in National Assembly:
Vile vile, Mswada huu, katika kipengele cha 46(5), kinazungumzia malipo. Jambo hili ni zuri sana kwa sababu juzi katika sehemu mojawapo ya barabara pale Jomvu, KURA walikuwa wanataka kunijengea barabara nzuri sana lakini wakaniambia, “Hakuna provision ya
view
27 Feb 2018 in National Assembly:
.” Niliona jambo hili haliingii kwenye akili na nikarudi kwa wananchi wangu na kuwaambia, “Liwe liwalo. Hatuwezi kutengeneza barabara tukavunja makao ya watu.” Tungeondoa nyumba, barabara ambayo tungetengeneza ingetumiwa na nani? Mswada huu ambao umesukwa na mwenyekiti Mhe. Pkosing, unatambua kwamba sharti malipo yapeanwe kwa watu ambao ardhi na mali yao itaathiriwa na ujenzi wa barabara.
view
27 Feb 2018 in National Assembly:
Kipengele cha 96 chazungumzia habari. Kuna shida kubwa hapo. Kwa hivyo naunga mkono Mswada huu zaidi. Nikipeana mfano, watu wa KURA wanataka kutengeneza barabara kwangu lakini wanasema eti wananchi wakae chini wajadiliane kisha ndiyo wapeleke maafikianao kwao. Ndiposa nilisema si sawa hivyo. Wao wanataka kutengeneza barabara. Kwa hiyo waje wazungumze na wananchi huko mashinani na kusema wanataka kujenga barabara fulani kwa ajili ya jambo Fulani. Kwa hivyo, mimi nikiungalia Mswada huu naona una mambo mengi mazuri. Siku chache zilizopita Mhe. Rais Uhuru Kenyatta alikuja Shika Adabu kule Mombasa. Nilisimama na kusema hatuwezi kupanua bandari yetu ya Mombasa bila kupanua externalinfrastructure ...
view
27 Feb 2018 in National Assembly:
hatutaki tena litoke katika nchi inayokua kama Kenya. Tunataka tuone barabara zetu zimenawiri na kuwa sawasawa. Kama Mbunge mwenzangu alivyozungumza hapa, barabara ya kutoka bandarini ambayo inaitwa gateway to East and Central Africa ndiyo barabara ambayo inafanya biashara katika nchi zetu za Uganda, Rwanda, Burundi na sehemu nyingine kunawiri. Kwa hivyo, ni lazima barabara hizi zitengenezwe na namwambia mwenyekiti wa Kamati inayosimamia barabara kwamba tutashirikiana pamoja na Kamati yake katika sehemu zetu tofauti ili tuweze kukuletea matatizo yetu tuone kuwa tumeyatatua kwa ajili ya wananchi wetu ambao wametuchagua. Kwa hayo machache, nakushukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa ...
view
21 Feb 2018 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo imeletwa na ndugu yetu, Mhe. Rashid Kassim. Kwanza, nataka na mimi nifanye kama vile dadangu Janet alivyowashukuru watu wa kwake. Na mimi ninataka kuwashukuru wananchi wa Eneo Bunge langu la Jomvu kwa kunichagua kwa mara ya pili niwawakilishe katika Bunge hili. Walinichagua mwaka wa 2013 nikiwa kijana mwepesi na wakanichagua mwaka 2017 nikiwa Garang De Mabior – mzee fulangenge. Kwa hivyo, nawashukuru sana wananchi wangu wa Jomvu. Vile vile, natoa rambirambi zangu kwa niaba ya wananchi wa Jomvu na mimi mwenyewe kwa watu wa ...
view
21 Feb 2018 in National Assembly:
na yeye katika kijiji kimoja ambacho alikuwa akizungumzia kuhusu amani na watu kukaa pamoja. Leo ameleta Hoja hii. Ni muhimu sisi Wabunge tumuunge mkono na hata tushikane pamoja. Kama kwake kuna matatizo tuende tusaidiane kama ndugu ili nchi ya Kenya iwe moja kwa watu kupendana.
view
21 Feb 2018 in National Assembly:
Nashukuru kwa kunipatia nafasi hii. Mwenyezi mungu akijalia utanipatia nafasi kuchangia ile Hoja ya sera ya nyumba kwa sababu nimebofya mpaka kidole kimeshaanza bonyea mpaka saa hizi. Nashukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Hoja hii. Asante sana na Mungu awabariki wote.
view