Bady Twalib Bady

Parties & Coalitions

Born

1st May 1974

Email

badibadi94@yahoo.com

Telephone

0722346475

All parliamentary appearances

Entries 71 to 80 of 177.

  • 9 May 2019 in National Assembly: Kwa hayo machache, nashukuru Wabunge wenzangu kwa kukataa Mswada huu kwa sababu utatuumiza. Nikimalizia kwa sababu tunataka kwenda kufuturu baada ya dakika tano, nataka kuchukua fursa hii nikiwa Muislamu na Mbunge ambaye anahudumu katika kipindi cha pili cha Bunge hili, kuwaombea Waislamu wote popote pale walipo. Nawatakia Ramadan njema. Wafunge kwa kusaidiana baina ya wenyewe kwa wenyewe na kusimamisha dini ya Kiislamu. view
  • 9 May 2019 in National Assembly: Asanteni na Mwenyezi Mungu atusaidie. Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Napinga sana Mswada huu kutoka Pwani, eneo Bunge la Jomvu, Kaunti ya Mombasa. view
  • 6 Dec 2018 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii kuchangia Hoja hii ambayo inaangazia walioteuliwa kwenye Tume hii. Kuna jambo ambalo limenifurahisha zaidi kutoka kwa mwanakamati ambaye amezungumza sasa hivi. Amesema waliangazia hawa wote ambao waliomba kazi hii na wakawaona ni watu wa tajriba kubwa. Hakika wanaweza kufanya kazi nzuri ili kutoa mchango mkubwa katika Serikali yetu ya Kenya. view
  • 6 Dec 2018 in National Assembly: Nimeiona kazi ambayo dada Charity alishiriki wakati wa nyuma. Tuliona akifanya kazi kwa njia nzuri. Vile, Balozi Salma alikuwa akifanya kazi kama balozi. Tumeiona kazi yake. Alitoa mchango mkubwa sana katika nchi hii ya Kenya. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hii na kupongeza Kamati hii. Tutapitisha wale ambao wamefanyiwa vetting ili waanze kazi na kutoa mchango katika Serikali yetu ya Kenya. view
  • 6 Dec 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nichangie katika mambo haya. Narudia kusema kuwa ni lazima Kamati iangalie vigezo fulani ambavyo vimetajwa. Waheshimiwa wenzangu wanaweze kuangalia hali ya vijana na walemavu. Pia, nasihi vijana na walemavu watume maombi wakati nafasi kama hizi zinapotangazwa. Sharti maombi yao yaambatane na zile kanuni ambazo zitahitajika. view
  • 6 Dec 2018 in National Assembly: Kwa hayo machache, nashukuru kwa kunipatia fursa hii. Naunga mkono hawa ambao wamewekwa hapa wachaguliwe. Asante, Mhe. Spika wa Muda. view
  • 6 Dec 2018 in National Assembly: On a point of order, Hon. Temporary Deputy Speaker. view
  • 6 Dec 2018 in National Assembly: Mhe. Spika wa Muda, mimi na Mhe. Njagua tunaenda kuchukua shahada zetu kesho kule Mount Kenya University. Nakuomba kwa unyenyekevu umpatia ruhusa kwa sababu tunaitwa tukachukue vyeti vyetu. view
  • 25 Jul 2018 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii leo ili niunge mkono Hoja hii ambayo imeletwa na ndugu yetu Owen Baya ambaye ni Mbunge kutoka Kilifi kuhusu mambo ya mkorosho. Kusema kweli, jambo hili ni la maana sana kwa sisi Wapwani kwa sababu ni muda mrefu sana ambapo Pwani ilibobea kwa mambo ya ukulima, na hasa ukulima wa korosho mpaka tukaona katika sehemu ya kilifi kulikuwa na mtambo mkubwa sana wa kusaga korosho. Mpaka dakika hii mtambo ule umekufa. Itakumbukwa vizuri kabisa kuwa mleta Hoja hii ametoa mifano kadha wa kadha. Ni dhahiri wengi tunaosafiri kwa ndege tunapewa ... view
  • 25 Jul 2018 in National Assembly: Itakumbukwa ni juzi tu pale Kilifi tukiwa na Mheshimiwa Aisha Jumwa, ambaye alizungumzia sana kuhusu mambo haya katika Karisa Maitha Stadium na maneno kama haya tumeyaunga mkono kutoka nyanjani hadi hapa. Tukiwa Bungeni tunaendelea kuyaunga mkono. Kwa hivyo, jambo kama hili la korosho… view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus