Bady Twalib Bady

Parties & Coalitions

Born

1st May 1974

Email

badibadi94@yahoo.com

Telephone

0722346475

All parliamentary appearances

Entries 81 to 90 of 177.

  • 18 Apr 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii ili nichangie Hoja hii. Kwanza, naunga mkono Mhe. Martha Wangari kwa kuleta Hoja hii muhimu sana kwa maisha ya wananchi wa Kenya. Ametoa mfano mzuri wa mahali kama Gilgil ambako watu wanasongamana sana huko Naivasha. Amesema kwamba alipofika hapo aliona watu takribani mia tano ambao walikuwa wameketi kwenye ofisi za usajiri. view
  • 18 Apr 2018 in National Assembly: Naunga mkono Hoja hii kwa sababu itawawezesha watu wengi hasa akina mama kusajili watoto wao ndiyo waingie shuleni. Siku hizi ni sheria kwamba kila mtoto ama mwanafunzi lazima asajiriwe na stakabathi ya kuzaliwai ili aweze kuingia shuleni. Vile vile, natoa pendekezo kwa Serikali kwamba wakati hawa watoto wote wanaingia shuleni wanakuwa na stakabathi za kuzaliwa ambazo zinaonyesha wao ni Wakenya. Moja kwa moja wakimaliza shule wapewe vitambulisho vyao haraka iwezekanavyo ili wakitoka shuleni hakuna haja tena kuzunguka ofisi mbalimbali ili kupewa stakabathi hii muhimu. view
  • 18 Apr 2018 in National Assembly: Tumeona watu wakienda sehemu mbalimbali kutafuta stakabathi hii na maofisa wa Serikali wakati mwingine wanachukua advantage yao kwa sababu wana hamu ya kupata stakabathi hizi. Kwa hivyo, wanafanya ufisadi na hii si haki. Lakini hii huduma ikienda katika Nyanja, kwa mfano kutoka kwenye eneo bunge mpaka wadi, litakuwa jambo la maana sana. Huduma hii itakuwa imerushwa nyanjani na watu wetu watasaidika kwa haraka. Tunaona kuwa wengi hawawezi kutafuta kazi ikiwa hawana vitambulisho. Wengi katika kutafuta stakabadhi za kuonyesha umiliki hawawezi kumiliki mali zao bila kupata vitambulisho kama Wakenya. Kuwezesha na kuona kuwa huduma hii inapatikana kwa njia nyepesi kutarahisisha na ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii ili nami nichangie. Kwanza, naunga mkono Hoja hii kwa shauri ni muhimu sana. Vile vile, nataka kumpongeza jirani na ndugu yangu Mohamed Ali ambaye in Mbunge wa Nyali kule Mombasa. Tumetoka kaunti moja na ameleta Hoja hii ambayo inapendekeza kuwa na hospitali ya rufaa katika mji wa Mombasa. Vile vile, sisi kama wanasheria katika kifungu cha 25 cha Sheria ya Afya, tumepewa nguvu ya kupendekeza kwamba katika kila gatuzi tuwe na hospitali ya rufaa ya kiwango cha sita. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Leo hii, mapendekezo hayo yatatusaidia. Kwa mfano, kule kwangu Jomvu kulitokea matatizo makubwa sana katika sehemu ya Owino Uhuru ambako kulikuwa na athari ya sumu. Tuliona huko Mombasa Kaunti kupitia Gavana Ali Hassan Joho walijaribu kuwatibu wananchi ambao waliathirika na hiyo sumu. Mpaka sasa, kwa shauri hakujakuwa na hospitali kubwa ya kuweza kuwatibu hao watu, bado athari hizo zimeongezeka. Leo hii, ukiangalia watoto ambao wanazaliwa, wengine wamedua. Pia wazee wanatamani kupata watoto wengine lakini mayai yao hayafanyi kazi vizuri. Kwa hivyo, watoto hawawezi kupatikana. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Kwa hivyo, Hoja hii ni nzuri sana. Tukiwa na hospitali ya rufaa tutaweza kutekeleza mambo mema kama yale ya ndugu yangu Mhe. Wamalwa ya utekelezaji. Utakuwa ni utekelezaji wa ukweli kupitia kwa kamati. Katiba yetu katika Kifungu cha 43 kinasema kwamba kila Mkenya ana haki ya kupata matibabu. Kwa hivyo, tukiwa na hospitali ya rufaa huko Mombasa haitatosha. Ni muhimu, hospitali hizi ziwe Kenya nzima ili tuone Wakenya wakiishi katika hali nzuri ya kuweza kupata matibabu kama haki yao ya kisheria. Tumeona ndugu yangu Mohamed Ali amechanganua vizuri kabisa na kusema madaktari Kenya nzima ambao wamesajiriwa ni 11,000. Lakini, wale ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: hawawezi kukimu yale mahitaji ya mamilioni ya watu ambao wako Kenya. Kwa hivyo, tukiangalia hali hii ya kuwa na madaktari wachache humu nchini, tunaona tunawapeleka wagonjwa hospitalini na baada ya siku chache tunawaona hao wagonjwa wakirudi katika hali ambayo si sawasawa. Ndugu Mohamed Ali amesema kwamba, ni kweli Wabunge matumbo yakiwatokota kama vile mtambo wa kusaga unga, wanapata njia ya kuweza kukimbia ulaya na sehemu nyingine kwa sababu wana huduma za bima na mambo mengine. Vile vile, hata tumbo la Spika nalo likitokota kama vile mashine ya tuk tuk, vile vile anaweza kwenda ulaya kupata matibabu. Lakini mwananchi wa kawaida ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa vile madaktari wetu ni wachache, ninapendekeza wale ambao wanafanya kazi kwa kandarasi waajiriwe. Pia, ninapendekeza wahudumu wa kijamii katika sekta ya afya, yani community health workers, ambao wanafanya kazi katika hospitali zetu lakini hawajaajiriwa rasmi, waajiriwe ili waweze kuendelea kuwapa wananchi huduma. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Wiki mbili zilizopita, nilizungumzia kuhusu shida ya maji na leo naungana na ndugu yangu Mhe. Maanzo, kusema kwamba magonjwa mengi sana yanaletwa na shida ya ukosefu wa maji. Kama vile ilivyo katika Kipengele cha 43 cha Katiba yetu, kila mmoja ana haki ya kupata huduma ya afya. Vile vile, kila mmoja ana haki ya kupata maji safi katika nchi yetu ya Kenya. Jomvu kwangu watu wanaumia kwa sababu ya ukosefu wa maji safi. Ni muhimu sana tushikane na washikadau wote katika nchi hii kuona kuwa tumewapatia maji safi wananchi wetu ili hali yao ya afya iwe nzuri. Tusipofanya hivyo, katika ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Kariuki na tunataka afanye kazi yake bila kumuingilia. Na penye matatizo tusi- mvictimise bali tuhakikishe kwamba amefanya kazi yake vizuri na hospitali hizo zimepata dawa na kuweza kuendelea kuwahudumia Wakenya. Kwa hivyo, namuunga mkono ndugu yangu, Mhe. Mohamed Ali, Mbunge wa Nyali; kwa kuleta Hoja hii na kuona kuwa Hoja hii haitarudishwa nyuma. Kamati ya Utelekelezaji ifanye juhudi kuona kuwa yale tuliyoyafanya yametekelezwa. Serikali, kupitia Kamati ya Bajeti, ione kuwa pesa zimetengewa shughuli hii. Kando na kuwa na Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Eldoret na hii ya hapa Nairobi, sisi watu wa Mombasa tungependa kujivunia kuwa na hospitali ya ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus