6 Aug 2019 in National Assembly:
Amri iliyotolewa itafanya makampuni mengi yafungwe. Kule Jomvu kuna makampuni kama vile Roadtainers, Crown Petroluem, Bayussuf na mengineyo. Bayussuf ni moja ya makampuni mashuhuri nchini. Hata Mhe. Kalembe Ndile alifanya kazi katika Kampuni ya Bayussuf. Kama kampuni hiyo ingekuwa imekufa, hatungeweza kumuona Kalembe Ndile kama tunavyomuona leo.
view
6 Aug 2019 in National Assembly:
Amri iliyotolewa itafanya makampuni mengi yafungwe. Kule Jomvu kuna makampuni kama vile Roadtainers, Crown Petroluem, Bayussuf na mengineyo. Bayussuf ni moja ya makampuni mashuhuri nchini. Hata Mhe. Kalembe Ndile alifanya kazi katika Kampuni ya Bayussuf. Kama kampuni hiyo ingekuwa imekufa, hatungeweza kumuona Kalembe Ndile kama tunavyomuona leo.
view
6 Aug 2019 in National Assembly:
Tukilazimisha makasha yabebwe na SGR pekee, baadaye wale wanaotumia mabasi wataambiwa waanze kutumia SGR na sio mabasi. Hakika wauzaji mafuta, vipuli na wengineo wataharibiwa biashara zao. Matokeo ni kwamba miji mingi ikiwemo Jomvu, Changamwe na Mlolongo yatakufa. Kwa hivyo, nachukua fursa hii kupinga amri hii vikali.
view
6 Aug 2019 in National Assembly:
Tukilazimisha makasha yabebwe na SGR pekee, baadaye wale wanaotumia mabasi wataambiwa waanze kutumia SGR na sio mabasi. Hakika wauzaji mafuta, vipuli na wengineo wataharibiwa biashara zao. Matokeo ni kwamba miji mingi ikiwemo Jomvu, Changamwe na Mlolongo yatakufa. Kwa hivyo, nachukua fursa hii kupinga amri hii vikali.
view
30 Jul 2019 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii niungane na wenzangu. Kwa niaba yangu na kwa niaba ya wananchi wote wa Jomvu, ningependa kutoa rambirambi zangu kwa wakaazi wa Kibra na Kaunti ya Bomet kwa kuwapoteza viongozi wao. Nataka kuzungumza juu ya Mhe. Ken Okoth ambaye alikuwa mtu mzuri sana. Binafsi, nilifanya kazi naye katika Bunge la 11. Mhe. Ken Okoth alikuja Jomvu kufungua madarasa huko Bangaladesh, Mikindani. Kwa hivyo, alikuwa rafiki mzuri. Mimi ni mwanakamati wa Bajeti. Miezi miwili iliyopita tulienda kushirikisha umma katika masuala ya Bajeti kule Bomet. Nilikuwa na mwenzangu, Mhe. Nyamita. Marehemu Mhe. Laboso alikuwa amekwenda ...
view
9 May 2019 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii leo kuchangia Mswada huu. Naungana na wenzangu katika kuupinga Mswada huu in totality, vikali na moja kwa moja. Vile vile, naungana na Mhe. (Dkt.) Nyikal ambaye amezungumzia… The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
9 May 2019 in National Assembly:
Sawa, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kulingana na uwezo wako na kulingana na hali ya Kiswahili, nitazungumza Kiswahili adhimu na sitaunganisha lugha nyingine yeyote. Maana ya “in totality” ni kwa jumla. Kwa hivyo nimejirekebisha na kusema “kwa jumla”. Neno “James” ni katika lugha ya Kizungu sijui niseme Jemsi Nyikal. Ni yale ambayo Mhe. Nyikal, na vile vile Mhe. Millie Odhiambo, walipinga. Katika Mswada huu kuna mambo ambayo yananigusa binafsi. Kama Mbunge kutoka kule Mombasa, tumempa uwezo mkubwa sana huyu Waziri katika mambo ya bandari. Hali hii itatuumiza sisi kama wakazi wa Mombasa, ambako bandari ipo. Hivi sasa, mdahalo mkubwa unaoendelea ...
view
9 May 2019 in National Assembly:
ambazo ziko hapo. Ile basi ambayo bandari ya Mombasa inataka kutumia, imejengwa kutokana na pesa za ushuru wa mwananchi. Haikujengwa na pesa za ushuru wa mtu mmoja. Haiwezekani kudhaifishwa au kubinafsishwa kwa mtu binafsi akaweza kuifanyia kazi ilhali ni sisi wananchi ndio tunaoilipia kodi. Kwa hivyo, ni lazima kuwe na usawa ili sisi watu wa Mombasa tufaidike katika mpango huu. Kulingana na Katiba ya Kenya, ni lazima kuwe na
view
9 May 2019 in National Assembly:
, yani watu kuhusishwa. Katika mambo haya, watu hawajahusishwa kisawasawa. Wasitufanyie ule mzaha ambao kwa Kiswahili unajulikana kama “kiriba goji, goji kiriba” – yani kutuzungusha tu hapo hapo kisha baadaye tunakuwa hatuna mbele wala nyuma. Ni mwezi mmoja na nusu uliopita tangu Serikali iamue kwamba watu watapata kipato kutoka kwa Mbuga ya Wanyamapori ya Voi. Tukiangalia katika Maasai Mara, watu wanapata kipato kule Kaunti ya Narok. Mpaka leo, hakuna chochote ambacho tunapata kutoka bandari yetu ya Mombasa. Watu wetu hawaajiriwi kazi kwa usawa. Nataka kupiga firimbi hapa leo. Hata kama bandari ni rasilimali ya Serikali kuu, ni lazima watu wahesabiwe ...
view
9 May 2019 in National Assembly:
lazima upatiwe nafasi ya kwanza katika bandari. Kwa hivyo, hivi sasa tunaona kuna watu wengi sana ambao wanaajiriwa katika bandari na kuna watu wetu ambao wamesoma na hawapati nafasi kama hiyo.
view