21 Feb 2017 in National Assembly:
Sijawatoa matusi, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
21 Feb 2017 in National Assembly:
Nikiomboleza na kusikitika na ndugu zangu wa kule Baringo na sehemu za Pokot, ni lazima Mhe. Nkaissery apandishe soksi zake na akaze ukanda vizuri, atume maofisa na kuweka amani katika sehemu hiyo. Mimi binafsi nikiwa Mbunge wa Jomvu---
view
11 Oct 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nami nichangie Mswada huu. Kwanza, ningependa kushukuru Mswada huu kutoka Bunge la Seneti. Ni Mswada mzuri kwa sababu watoto wengi hukosa elimu kwa sababu ya kukosa msingi bora. Niseme kwamba tumeanza kuona matunda ya Mswada huu. Kwa mfano, pale Jomvu, eneo Bunge langu, ipo shule ya msingi ya Jomvu ambayo inayo shule ya chekechea. Mheshimiwa Ali Hassan Joho, Gavana wa Mombasa, aliona umuhimu kuhakikisha kwamba shule za chekechea zina ufanisi na zinajengwa kwa muundo wa kileo. Ninayo imani kwamba haya anayofanya Gavana Joho atayafanya vile vile katika nchi ...
view
11 Oct 2016 in National Assembly:
Kwa hivyo, tumeona mifano. Shule za chekechea katika Bara Ulaya zinachukuliwa kuwa muhimu sana kwa sababu ndizo msingi wa kumuweka mtoto aonekane kweli anaweza kuwa na taaluma fulani. Pia ni muhimu kuwa na mpango kabambe kwa sababu tunaona watoto wengi sana wanatoka katika hali ya maisha ya mabanda na wengi hawajiwezi katika sehemu nyingi tunazotoka. Kwa hivyo, kupitia mfumo wa elimu ya bure ambayo iko sasa, watoto wengi wanaenda shule. Ni bora kuangalia katika Serikali Kuu na katika serikali za kaunti kuona kuwa kutakuwa na lishe kwa shule zote za chekechea katika nchi nzima ya Kenya ili hao wanafunzi wanaoenda ...
view
11 Oct 2016 in National Assembly:
Elimu ni chombo muhimu sana katika maisha. Ninasema hivyo kwa sababu watoto ambao hawakusoma hufanyiwa kejeli wanapocheza na watoto wenzao. Unaona mtoto anakaa pale na kwa vile mmoja alienda shule, humuuliza yule hajasoma maana ya “debe tupu”. Kwa Kiswahili sanifu tunasema “haliachi kelele”. Lakini, kwa yule hajasoma, akiulizwa “debe tupu” atasema “lijaze kitu ili lijae”. Kwa hivyo, hiyo ni njia moja inayomfanya asizungumze sawa na wenzake.
view
11 Oct 2016 in National Assembly:
Nikiwa Mbunge wa Jomvu, nimeupongeza sana Mswada huu. Nimeupongeza kwa ajili ya kunifaidi katika eneo Bunge langu. Shule ya chekechea ambayo imejengwa, watoto wataendelea kusoma na wataonekana kwa fikra zao kuwa wanasomea mahali ambapo ni pazuri. Mswada huu umezungumza kuhusu shahada ya diploma kwa wale watasomesha shule za chekechea. Tumeona kuwa watu wengi wamesoma kozi za elimu ya msingi ya watoto katika vyuo tofauti tofauti. Ni jukumu letu sasa kuangalia katika serikali za kaunti na Serikali Kuu tuone kuna mpango mzuri ili walimu waandikwe kwa wingi na watoto wetu wapate elimu hii. Kwa hayo machache, Mswada huu umenifurahisha. Ninaona watoto ...
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hoja hii. Kwanza, mimi pia naungana na wenzangu kukupa pongezi nyingi sana kwa namna ambavyo umetuelekeza katika Bunge hili. Haikuwa rahisi. Kama vile ndugu yangu Mhe. Mwanyoha alivyosema, Bunge hili liko na wanaume. Vile vile naongezea sisi kule Pwani twasema liko na nyangumi na papa ambao wanaweza kutafuna mtu akifanya mchezo. Kwa hivyo, tunashukuru kuona kuwa mawimbi yale umeweza kuenda nayo na kutupeleka kwa njia ya sawasawa. Pili, nakupongeza kwa busara yako. Nimekuja ofisini kwako mara kwa mara nikitaka kufafanuliwa vipengele vya sheria na umenieleza namna ya kufanya kazi ambayo nimepewa ...
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
segemnege. Kama halingepitishwa, basi maisha ya watu yangelikuwa ni hali Waswahili wanasema ‗goji kiriba na kiriba goji‘. Yaani ni pale pale ambapo sisi tunarudi. Mhe. Spika, nafikiri tulifanya kazi nzuri sana. Tunakupongeza kwa kuongoza mijadala yetu na kuhakikisha kwamba tumepitisha sheria kwa njia nzuri ambayo itawafurahisha Wakenya. Mwisho, nawatakia wabunge wenzangu likizo njema. Tushikane mikono pamoja. Mungu atujalie turudi Bunge tena na tufanye kazi kama ndugu ili tuwasaidie wananchi waliotuchagua.
view
3 Aug 2016 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja hii. Nakushukuru zaidi kwa sababu hapo awali, vile vile, ulinipa nafasi ya kuchangia mambo haya ya ardhi. Naunga mkono Ripoti hii nzuri na kuipongeza Kamati ya Pamoja ya Uwiano kwa kufanya kazi nzuri. Ningependa kumpongeza Mwenyekiti wetu wa Kamati ya Ardhi, Mhe. Mwiru, kwa kazi nzuri. Kama Mbunge wa Eneo Bunge la Jomvu, sehemu ya Pwani ina shida nyingi ya maswala ya ardhi na nimeona juhudi yake. Kulingana na Ripoti hii, nimemsikia akizungumzia mikataba ya kupangisha, yakikaribia kuisha ni muhimu kwa wale wanaohusika kujulishwa miaka mitano kabla, ili wajue namna ...
view
3 Aug 2016 in National Assembly:
kuwa hawatafurushwa kabla ya kujua watakachofanya. Ni muhimu kuwa wanapojulishwa, Kamati izingatie uhalali wao kwa sababu kule Mombasa kuna watu wanaoishi mahali na mikataba ya kupangisha yana mtu mwingine. Ni vile tu hakuwatoa mahali pale. Kwa hivyo, ni muhimu uhalali uangaliwe ili mikataba ya kupangisha yakiisha, mashamba yarejeshewe wenyewe badala ya kuyarejesha kiholela. Ni muhimu kuzingatia mambo haya na kuhakikisa kuwa wenyeji wanapewa haki yao. Tulihakikisha kuwa dhuluma za kihistoria zimeshughulikiwa na Mwenyekiti ametaja mambo yote katika maeneo haya. Vile vile, Hoja hii imehusisha watu wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi na inafafanua jinsi ya kushughulikia dhuluma za kihistoria. Kipengele ...
view