Christine Zawadi Gona

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 91 to 100 of 112.

  • 23 Jul 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii niweze kuzungumza kuhusu taarifa ambao iko mbele yetu. Namshukuru Mhe. Sen. Faki. view
  • 23 Jul 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Nakubaliana na wezangu ambao wamezungumza mbeleni kwamba yale yanataka kufanyika ni unyanyapaa wa hali ya juu. Sisi watu wa Pwani, hasa Kilifi, Mombasa na Kwale ni Wakenya kama Wakenya wengine. Kwa hivyo, kama peas zimekuja kama zimetulenga, wachazitufikie. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 23 Jul 2019 in Senate: Kama kitu ni kizuri, kinakuja Nairobi. Mtu wa Kilifi akitaka msaada, atatoka Mombasa, Kilifi au Tana River mpaka Nairobi. Hiyo si ungwana. Maana ya ugatuzi ni nini ikiwa watu watatoka kule mashinani na kuja Nairobi? Watu wa chini wanafaa kufaidika na kuinuka kiuchumi. Kama ni nyumba za kupangisha, wale watakua maofisini wataenda kupangisha nyumba hizo na biashara itasongea. Ninaungana na wenzangu kwamba si haki zile ofisi zije Nairobi kwa sababu bahari iko Pwani. Ninauhakika watu kama wale wangepewe nafasi, wangehamisha bahari lakini Mwenyezi Mungu alipanga iwe kule. Wacha watu wa Pwani wafaidike na wale matunda yao. Mwenyezi Mungu aliwaumba na ... view
  • 10 Jul 2019 in Senate: Asante sana, Bi.Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Arifa iliyo hapa mbele yetu. Kusema ukweli, Mwenyezi Mungu aliumba Wanyama na msitu viwe visaidizi kwa mwanadamu. Vile vile, Serikali ilipokuwa inakataza watu wasikate misitu, walifunga njia lakini hawakufungua njia. Walisema watu wasikate, lakini kuna watu ambao walikuwa wanaishi wakitegemea hiyo misitu. Hawakuwatolea The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 10 Jul 2019 in Senate: njia baada ya kufunga misitu. Ni jambo gani mwanachi wa kawaida atafaidika nacho tena? Wamewacha watu wakiwa wanateseka. Kuna watoto ambao hata hawaendi shule. Shule ni za bure lakini kuna vitu vingine si bure kwa sababu ni lazima mtoto awe na sare ya shule na vitu vingine ambavyo vinahitajika. Vile vile, kuna sehemu zingine, hakuna viwanda vya kazi, wanategemea hiyo misitu wako nayo iwasaidie kwa kuni, makaa na vitu vingine vingi. Waliposema watu wasikate misitu hawakuto njia mbadala. view
  • 6 Jun 2019 in Senate: Shukrani Bw. Spika kwa kunipa nafasi hii kuwakaribisha wasichana kutoka Kaunti ya Tharaka Nithi. Naamini kwamba watajifunza mengi hapa. Naamini kwamba kuna viongozi watakaotoka miongoni mwao. Nawasihi wawe mfano mzuri tukizingatia mara nyingi shule nyingi huchomwa wakati wa mitihani. Nawahimiza wanafunzi hawa wawe na nidhamu. Wasiwe watovu wa nidhamu kwani wakikosa nidhamu, wanawapa wazazi wasiwasi, hasa mama, kwa sababu ndiye mwenye kuhangaika zaidi kuhakikisha watoto wake wamesoma. Naomba wanafunzi watakapotoka hapa wajue kwamba kuna viongozi waume na wanawake. Viongozi wanawake sana sana hufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja. Mbali na kuwa Maseneta, kuna kazi mbali mbali ambazo sisi hufanya. Ukihesabu ... view
  • 26 Sep 2018 in Senate: Asante sana Bw. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii nichangie mdahalo huu. Nampongeza Eliud Kipchoge kwa kuvunja rekodi. Najua si yeye pekee bali kuna wengine ambao walitangulia. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 26 Sep 2018 in Senate: Mdahalo huu umekuja wakati mzuri. Kuna jambo moja nzito sana hasa kwetu watu wa Mombasa. Michezo kwetu haijatiliwa mkazo sana. Serikali za Kitaifa na zile za Ugatuzi kwa jumla hazijatilia mkazo sana mambo ya michezo. Tuna changamoto kubwa ya ukosefu wa kazi. Michezo ingekuwa imetiliwa mkazo, watu wengi wangefaidika. view
  • 26 Sep 2018 in Senate: Kule kwetu kuna mihadarati na mambo mengi ambayo yameharibu watoto. Igekuwa michezo imetiliwa mkazo vile ambavyo inatakiwa, watoto wengi wangekuwa wameepukana na mihadarati ambayo iko kule. Vile vile, napendekeza kama wenzangu walivotangulia, kwamba kama kuna haja ya kitengo fulani ambacho wanamichezo wangekuwa wanaagaliwa. Jana tukiwa kwenye Kamati ya Barabara na Usafiri, kuna mama mmoja aliwafananisha wanaume na ndege ambao wana miti mingi. Kwa hivyo “miti mingi” ya wanaume kama ingepungua, nina hakika ufisadi ungepunguka hapa Kenya. view
  • 26 Sep 2018 in Senate: Nasema hivyo kwa sababu wanaume wengi ndio wanashikilia nyadhfa kubwa kubwa. Kwa hivyo, hiyo “miti” yao, kama wangejaribu kuikatakata ama kuipunguza, nina uhakika ufisadi ungepungua, mambo mengi yangefanyika na pesa ingefika mashinani na kwa vile vitengo inavyotakiwa. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus