Christine Zawadi Gona

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 71 to 80 of 112.

  • 20 Feb 2020 in Senate: Bw. Spika, kuna matamshi mengine ambayo mtu akiyatamka, anavunja watu mioyo. Mfano ni kusema kwamba hao nzige wamegeuka rangi ya dhahabu ama samawati na kwa hivyo watakufa. Kwa mfano, kuna Maseneta wanawake na wanaume. Watoto wenu wadogo wanawaona kama ‘mungu’ wao. Hata wakipigwa na mtu au hata wakitukanwa, wanasema: “Baba akija---” Anajua baba yake hawezi kufanya kitu, lakini baba yake kwake ni ‘mungu’ wake; anaamini kuwa anaweza kila kitu. Sasa sisi na wananchi tunamtegemea Waziri wetu kama baba anayeweza kila kitu. Lakini sasa akijitokezea na kuzungumza maneno aliyozungumza, ni kumaanisha kwamba huyu baba hawezi kutegemewa na inavunja mioyo vibaya sana. ... view
  • 20 Feb 2020 in Senate: Waziri anafaa aja ili tuzungumze naye na atuambie ni nini anapanga kuhusu watu wetu ambao mashamba yao yamevamiwa. Ni vipi watapata chakula na hao nzige ambao anasema wakiwa rangi ya manjano wanakufa--- Ninavyojua mimi, hao nzige wake ambao wamekuwa rangi ya manjano wanazaana ile ‘mbaya mbovu.’ view
  • 20 Feb 2020 in Senate: Wanabebana mgongoni. Nzige wa kike ndiye anayebeba wa kiume. Kwa hivyo, wako hapa na shughuli ni moja tu ya kuzaa. Yeye akisema kuwa watakufa, anajua aje? Basi anafaa aje hapa atuambia hao nzige wake wamefika wapi, na anawaza nini. view
  • 20 Feb 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. Vile vile, nimesimama kuchangia mjadala unaoendelea nchini kuhusu ugonjwa wa Corona Virus . Waswahili husema: ‘ukiona cha mwenzio kinanyolewa, chako tia maji.’ view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Sasa katika yote tunayozungumza, ni mikakati gani ambayo imewekwa kuona kwamba ugonjwa huo utakapoingia humu nchini, utakabiliwa vilivyo? Iweje basi Mchina akitoka kwao na aingie hapa nchini awe hana huo ugonjwa lakini Mkenya aliye China akirejea hapa nyumbani awe nao? Kama Wakenya walisema ndege zao zisiende China, sawa. Je, walikataza za China kuingia Kenya? Kama hawajakataza, lengo na madhumuni yao ni nini? Wale walio kule China ni watoto wetu tuliozaa sisi. Mwenyezi Mungu aliweka siri kwamba hakuna anayejua atakufa lini. Kuwaacha watoto wetu wakae kule China ni sawa na kuwahukumu wafe. Tumeshawatoa kafara. Kama mzazi, mimi naona tunapoteza. Balozi wetu ... view
  • 19 Feb 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 10 Feb 2020 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii niweze kutoa rambirambi zangu pamoja na za jamii nzima ya Kilifi. Nakumbuka wakati huo alikua ni mtukufu Daniel arap Moi. Namkumbuka kama jinsi wenzangu walitangulia kusema hasa nitaanza na maziwa nikiwa prefect wakati ule darasani nilikuwa nikihesabu hata wenye hawakuja shule ili yawe mengi na mimi nibebe. Wakati mwingine nilikuwa ninaenda shule hata kama nina homa kwa sababu nimetoka kwa jamii ambayo haijiwezi kiasi kwa hivyo mlo ulikua mmoja na singeweza kukosa shule kwa maana yale maziwa yalikua yananisaidia. Nilikuwa ninaandika wale hawako ili niweze kupelekea wale wenzangu waliokua nyumbani waweze kupata. Katika ... view
  • 10 Feb 2020 in Senate: Bw. Spika, tuliachwa na wazazi wetu tukiwa wadogo na ninaishi naye mpaka sasa. Tunavyoishi kukiwa na machungu yoyote ambayo yanamguza “Moi” utakuta watu view
  • 10 Feb 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus