Christine Zawadi Gona

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 112.

  • 11 Mar 2020 in Senate: Asante Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili kusema maneno machache kuhusu Malalamishi ambayo yako mbele yetu. Kwanza, nampongeza Sen. (Prof.) Kamar kwa kuleta Malalamishi haya kwa wakati ufaao. Ni kweli kabisa kwamba watu huwa na miungano kwa ajili ama kusudi la kunufaika. Nitapeana mfano wa Kilifi. Tulikuwa na mtambo wa korosho na kulikuwa na miungano ama co-operatives ambazo zilianzishwa wakati huo. Wengi ambao walikuwa wakichanga pesa walikuwa kina mama kwa sababu mtambo huo uliwaandika kina mama wengi sana. Hata hivyo, pesa yao ilienda hivyo na hakuna anayejua kwa kuwa mtambo wenyewe ulisambaratika. Wahenga walisema; yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. ... view
  • 11 Mar 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 11 Mar 2020 in Senate: Tulifanya ziara Afrika Mashariki yote. Katika mizunguko yetu tuliona kuna sehemu kadha wa kadha ambazo zinahitaji mkazo. Kwa mfano, tulitembelea Zanzibari, tukakuta maafisa wenu pale hawaielewi lugha ya Kiswahili kabisa. Afadhali sisi angalau tunajaribu. Tulishangaa jinsi wanavyofanya kazi na watu wengini. Ninawasihi mtilie mkazo Kiswahili ili kiwe kikitumika katika nchi zote za Afrika Mashariki. Hii ni kwa sababu kuna biashara inayoendelea baina ya mataifa haya ya Afrika Mashariki. Kwa hivyo, ninafikiri Kiswahili kingedumu zaidi katika nchi zote husika za Afrika Mashariki. Kuna mambo mengi ambayo yanaenda sawa na mengine hayaendi sawa--- view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Asante Bw. Spika. Nakuunga mkono kuwakaribisha wanafunzi na walimu wao kutoka Kaunti ya Kiambu. Ningependa kumtambua Sen. Wamatangi kama kiongozi mwenye bidii. Tumetembea Kaunti ya Kiambu mara nyingi tukiangalia miradi ya barabara. Naamini kwamba watu wa Kaunti ya Kiambu wako sawa. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Bw. Spika, Sen. Wamatangi ndiye mwenyekiti wa Kamati ya Nishati, Barabara na Usafirishaji. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Nakuunga mkono kutoa rambirambi zangu kwa familia ya marehemu mhe. Dori kwa kumpoteza kiungo muhimu katika jamii. Mhe. Dori alikuwa mlezi katika nyumba yake. Kwa kumpoteza Mhe. Dori, ninahakika familia hiyo imempoteza mtu wa maana ambaye watamkumbuka kwa siku nyingi. Sisi sote ni watembezi ulimwenguni. Wakati utakapofika, kila mtu atarudi mavumbini tulikotoka. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Bw. Spika, Mhe. Dori alikuwa mwenyekiti wa wabunge wote wa Pwani; wabunge wa Seneti na wale wa Bunge la Kitaifa. Mhe. Dori alipenda sana ushirikiano. Mhe. Dori alipenda tukishirikiana katika mambo ya Bandari ya Mombasa. Alisistiza kwamba bandari ikihamishwa, watu wa Pwani watateseka. Mhe. Dori alikuwa na marafiki kutoka pande zote za Kenya kwani Kwale kunaishi makabila zote. Naamini kwamba kifo cha Mhe. Dori kinahusisha jamii zote za Kenya. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Nikizungumzia ushirikiano, nimgependa kuwapa hadithi fupi. Kuna bwana moja aliyekuwa mkali sana na mke wake mpaka ikawa bibi yake anamuogopa sana kiasi kwamba hawezi kumuambia jambo lolote akiogopa kwamba atakaripiwa. Hivyo, mzee huyo aligonjeka na kuenda hospitali. Kule hospitalini, alipewa kichupa atakachotia mkojo wake wa kwanza akiamka asubuhi. Mzee yule alienda nyumbani na kichupa chake lakini hakumuambia mke wake kazi ya kichupa hicho. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Asubuhi ilipofika, mzee yule alikojoa ndani ya kichupa alichopewa hospitalini na kukiweka kando ya kitanda. Mke wake alipoamuka, aligonga kichupa cha mzee yule kwa bahati mbaya na mkojo ukamwagika bila mzee yule kujua. Kwa sababu ya ukali wa yule mzee na kutokuwa na ushirikiano na mke wake, mama yule alikata kauli na kuchukua kichupa hicho kisha akaenda akakikojolea yeye mwenyewe na kukirudisha palepale. view
  • 10 Mar 2020 in Senate: Bw. Spika, wakati mzee yule alipoamuka, hakujua kama kuna kitendawili kilichofanyika. Mzee yule alichukua chupa iliyokuwa na mkojo na kuelekea hospitalini. Baada ya mkojo huo kupimwa, daktari alimuambia mzee yule kwamba hajui kama wampe pongezi au wamuambieaje kwani mkojo wake ulidhihirisha kwamba ana uja uzito. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus