11 May 2021 in Senate:
Bw. Spika, ninaunga mkono kwamba wanawake wanawajibika kiasi fulani. Kwa mafano, haya mapendekezo ya Katiba yamesema kutakuwa na Seneta mwanamke. Tutakuwa na wanawake 47 tukiongezea na labda wanaume 47 watakaokuwepo iwapo haya mapendekezo yatapitishwa.
view
11 May 2021 in Senate:
Bw. Spika, ninakubaliana na wenzangu kwamba ni kweli mwanamke ndiye anawajibika. Fanya hesabu haraka tu uangalie hapa ndani kumesalia wanawake wangapi na wananume ni wangapi. Kisha fanya hesabu uone wanaume na wanawake huwa wangapi katika Bunge hili la Seneti. Utakuta mwanamke anawajibika na ndio maana wengi wako hapa ndani wanasikiza jinsi Mswada huu unavyoendelea. Hivyo basi, ninakubali mwanamke mmoja awe katika Bunge la Seneti. Vile vile, ningetamani mwanamke mwengine abakie kwenye Bunge la Taifa. Hii ni kwa sababu, kuna changizo kubwa mwanamke angefanya akiwa kule. Kwa hivyo, nakubaliana kwamba kungekuwa na mwanamke katika Bunge la Taifa na Seneti.
view
11 May 2021 in Senate:
Mhe. Spika, nashukuru kwa Katiba ambayo tuko nayo. Nikiwa Seneti, sina uwezo wa kutembea kaunti nzima, lakini nikiwa kwenye bunge la kaunti, nilitembea. Waheshimiwa wengi walikuwa na miradi yao. Hatukuwa tunajuwa majosho ya ng’ombe. Josho la ng’ombe ni ‘cattle dip.’ Sasa hivi kuna majosho mengi yamejengwa. Wale ambao hawana uwezo wa kuosha ng’ombe wao ama kuwapa dawa, wanaenda katika majosho yale kuwaosha ng’ombe wao.
view
11 May 2021 in Senate:
Madam Deputy Speaker, I vote yes.
view
11 May 2021 in Senate:
Naamini kwamba iwapo pesa itaongezeka katika magatuzi, kuna maendeleo mengi ambayo yatapatikana ambayo hayakuwa yanapatikana kwa sababu ya uhaba wa pesa. Nakubaliana kwamba iwapo mjumbe wa Bunge la Kaunti atakuwa anapata zile
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 May 2021 in Senate:
pesa za maendeleo---. Sasa hivi, ni gavana ambaye anawapea. Gavana asipopenda, hakuna pesa wanazopata. Iwapo hii Katiba itapita, Mbunge wa Kaunti atakuwa na pesa yake. Atafanya miradi kulingana na ile kata yake anayotoka. Atazingatia upungufu katika kata yake akifanya maendeleo na hakuna mtu atamwingilia.
view
11 May 2021 in Senate:
Vile vile, nashukuru na niseme kwamba angalau watu wa Kilifi tumeweza kuwa na barabara mbili au tatu. Sisi pia tunajiita Wakenya. Pale nyuma, tulikuwa tukisema pwani si Kenya. Hii ni kwa sababu hatukuwa tunayapata mengi. Angalau kuna kidogo tunaweza hesabu. Kwa mfano, barabara. Sio nyingi, lakini zipo. Sio kama vile ilivyokuwa mwanzoni, wakati tulikuwa hatuna kabisa. Nakubaliana kwamba, iwapi pesa zitakuwa mashinani, hatutakuwa tunatengemea Bunge la Taifa au Serikali kuu itutengenezee barabara. Tutakuwa na uwezo huo kama kaunti wa kutengeneza barabara na vitu vingine vingi ambavyo vinakosekana. Kama barabara ni ya murram, sio lazima Executive ikubali ndiposa ifanyike. Itakuwa inafanyika.
view
11 May 2021 in Senate:
Mhe. Spika, ningependa kuzungumzia mapendekezo ya Building Bridges
view
11 May 2021 in Senate:
Iwapo itapita, wale wabunge ambao watabahatika kuchaguliwa, tutapata waziri wetu kutoka kwa wale wabunge. Mimi naunga mkono. Hii ni kwa sababu, ni mara ngapi tuliita Waziri wa Kilimo hasa wakati ule wa nzige? Tulisumbuka sana kuita Waziri wa Kilimo na Ilikuwa vigumu sana kupatikana. Vile vile, tumemwita Waziri wa Barabara mara nyingi lakini inakuwa shida kupatikana. Kwa nini? Ndio maana naunga mkono Katiba hii au mapendekezo haya. Iwapo itapita, basi waziri watatoka hapa, haina haja tukawafuate mbali. Tukimtaka, tutampata hapa hapa, kwa maana ni mmoja wetu, tuko naye, and twala naye. Ni haraka sana kuonana naye na kutatua mambo ambayo ...
view