11 May 2021 in Senate:
Naunga mkono hii Katiba. Ikipita, basi kuna mengi mazuri yatakuja. Sijui blue
view
11 May 2021 in Senate:
inasemaje? Sikuisoma vizuri au sijapata nafasi ya kuisoma vizuri. Najua ipo lakini sijui imesemwa vipi. Hapo siwezi kujua. Nataka tu ijulikane kwamba bahari ndio uti wa mgongo wetu, sisi watu wa pwani. Tunaitengemea kwa kila kitu; ndio shamba yetu kubwa ya kahawa. Labda ndio shamba yetu kubwa ya majani chai na sukari. Kwa hivyo, naamini na ninataka niamini kwamba imeangaliwa vizuri. Mwananchi wa pwani hatajiona ameachwa upande wa kiuchumi bali amekumbukwa.
view
11 May 2021 in Senate:
Mhe. Spika, kwa ule muda mchache ambao niko nao, wakati tunapoanza safari kama tunaenda mahali, na tuko karibu kupanda gari, huwa Tunasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu, tujalie tufike salama.’ Hii ni kwa sababu, vyombo tunavyosafiria vimetengenezwa na mwanadamu. Nasema hivyo kwa sababu hii Katiba imetengenezwa na mwanadamu, haikunitengenezwa na Mungu wala kuanguka kutoka binguni. Kwa hivyo, haitakosa dosari hapa na pale kwa sababu ni mwanadamu aliyetengeneza na mwanadamu si kamili. Kwa sababu mwanadamu si mkamilifu na ametunga hii sheria ambayo tumeona
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 May 2021 in Senate:
mapendekezo yake, haiatakosa kasoro. Hakuna kitu kilicho tengenezwa na mwanadamu ambacho hakina kasoro. Basi tuangalie makubwa na madogo; je, kasoro ni nyingi ama faida ni nyingi? Kwangu, faida ni nyingi na itafaidisha wananchi wa Kaunti ya Kilifi. Nikiangalia kwa kina hakuna tunacho poteza bali ni kufaidika tunafaidika. Naungana na wenzangu kuunga mapendekezo iliyoletwa mkono.
view
11 May 2021 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I vote yes.
view
11 May 2021 in Senate:
Bi Naibu Spika, asante sana kwa kunipa fursa hii ya kujiunga na wenzangu kupongeza Bunge la Seneti kwa kukubaliana na kupiga kura nzuri. Kila safari ya hatua mia huanza kwa hatua moja. Leo tumechukua hatua moja. Kwa niaba ya Kaunti ya Kilifi, nawashukuru Masenata kwa kupitisha Mswada huu. Kuna mengi ambayo tulikuwa hatupati kwa hivyo nina imani kuwa kupitisha Mswada huu, kuna mazuri mengi yatakayo fuata nyuma.
view
11 May 2021 in Senate:
Ingawa kuna kaunti nyingi ambazo hazitapata maeneo bunge zaidi, ningependa kuwakumbusha kwamba kila kilocho na mwanzo hakikosi mwisho. Sio kwamba tunawaonea au hatuwapendi, lakini siku haikuwa yao. Wakati utafika siku moja na watapata maeneo bunge mengine. Na hata kama hawatapata sehemu zaidi za uwakilishi Bungeni, nina hakika kuna mengine ambayo wameyapata mazuri kulingana na hiyo BBI. Ukiiangalia viziri utakuta hapo ndani kuna mambo mazuri mengi na mabaya hayakosi kwa sababu ni mwanadamu aliyeitengeneza. Ninaamini tulivyoanza kwa mwendo huu, tumeanza safari na nina hakika ina mwisho mwema.
view
23 Jun 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Naunga mkono wenzangu kwa yale wanayo jadili kwamba tumekosa haki na imani kwa polisi. Pia, sio polisi wote kama vile wenzangu wanavyo zungumza, lakini ukweli ni kwamba nidhamu imekosekana. Kuna utepetevu fulani katika Idara ya Polisi ambayo imefanya wengi wetu kukosa imani nao. Juzi nikiwa naelekea nyumbani, nilipofika Kilifi kabla sijaingia nyumbani, jioni kama Saa Mbili hivi iki karibia Saa Tatu, nilimkuta polisi akimfukuza mtu. Huyo mtu alipita mbele ya gari niliyokuwa, ikasimamishwa gafla na nikashuka. Mwajua kuwa tuko na sheria inayosema kwamba watu wawe nyumbani Saa Tatu inapofika. Nilimsimamisha huyo polisi nikamuliza: “Kwa nini unamfukuza huyu ...
view
23 Jun 2020 in Senate:
Bw. Spika, kule Kilifi kuna bahari. Kuna msemo usemao “Nishike samaki kumi, nishike samaki mmoja, harufu yangu ni ile ile ya samaki.” Hatutasema harufu yangu ime shika samaki mmoja au kumi! Itakuwa harufu ni ile ile. Kwa hivyo polisi wawe wazuri au wawe vipi, lakini tumekosa imani nao, Idara yao ime oza na kuna utepetevu wa nidhamu! Kuchukuliwe haki kutoka kwao kwa sababu akiuawa mmoja na jami, utaona polisi wote wametoka kupiga watu wa hiyo mtaa mzima, hakutakalika eti askari mmoja alipigwa. Lakini wana ua watu wetu kila siku na hakuna kitu kina fanyika. Ni mmoja katika askari mia moja ...
view