Christine Zawadi Gona

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 61 to 70 of 112.

  • 10 Mar 2020 in Senate: Bw. Spika, hayo yote yalitokana kwa sababu ya kukosa ushirikiano. Maseneta na wabunge wa Bunge la Kitaifa wanafaa kushirikiana. Shida inapokuja, tunapaswa kushirikiana kama vile marehemu Mhe. Dori alikuwa kipaumbele kusema kwamba watu washirikiane. Mhe. Dori hakuwa na ubaguzi na mtu yeyote. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake Mhe. Dori mahali pema peponi. view
  • 4 Mar 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. Nataka kumpongeza Sen. Kihika kwa kuleta mjadala huu wa kina mama. Bw. Spika, Mwenyezi mungu alimuumba mwanamke akiwa ametulia sana kwa sababu alikuwa kiumbe cha mwisho kuumbwa. view
  • 4 Mar 2020 in Senate: Vitu vyote vilikuwa vimeumbwa, lakini akaona bado havitoshi; kuna upungufu; ndio maana akamuumba mwanamke. Kwa hivyo, mwanamke ni kiumbe ambacho The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 4 Mar 2020 in Senate: hakifananishwi na mtu mwingine yeyote. Yeye ni kiumbe cha kipekee ambacho Mwenyezi Mungu akakipa hadhi kubwa. Vile vile, Bw. Spika, kwa uchache tu, kuna msemo naskia wazungumshi wakizungumza siku hizi, kwamba gavana akiwa mwanaume, mwana chini wake awe mwanamke. Mimi napinga hilo. Nasema kwamba gavana akiwa mwanamke, basi chini yake awe mwanamume kwa sababu twaweza kina mama. Na haya sio mambo na pesa--- view
  • 4 Mar 2020 in Senate: Wajua mahali pengine hapana mjadala. Upende, ukatae; mwanamke ni kiumbe muhimu. Kama ulikuwa wa maana sana, mbona ubavu utolewe nitengezwe mimi, na ulikuwa uko nao mwilini mwako mwenyewe? Kwa hivyo, mwanamke ni kiumbe muhimu; tukubali hilo kwanza. Halafu pia nataka kuishukuru Serikali ya Kenya; pamoja na yote ambayo uko nayo, imenifanya mimi nimekaa hapa Seneti leo. Hii ni kwa sababu ya Serikali ya Kenya na vyama vyetu tulivyo navyo. view
  • 4 Mar 2020 in Senate: Najipongeza kama Seneta niliyekaa hapa, lakini bado sijatosheka. Kama vile Jakobo alikuwa anampenda Rachel, lakini hakumpata akampata Leah. Sio aliyekuwa amemtaka, lakini hakufa moyo; akarudi pale pale mpaka akampata Rachel. Nasi pia vile vile tuko hapa, lakini bado tuko na ari na mawazo ya kwamba kesho tutapata pale mahali tulipokuwa tukipataka. Sen. Wetangula, lako hilo nnakupa. Tuko hapa, lakini kisha baada ya muda, na sisi pia tutatoka tuwe na vile viti ambavyo twavitaka. Mwisho nikimalizia, Bw. Spika, nataka kumsifu mwanamke. Mwanamke amebobea mpaka kwa jua kali pia yupo; sio katika vyeo vikubwa tu, hata jua kali. Wanawake wamekuwa wabunifu, na ... view
  • 4 Mar 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 3 Mar 2020 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. Nasimama kwa hoja ya nidhamu, kwa sababu sielewi kile anachosema Sen. Wario. Mjadala ulio hapa unahusu usalama, wala si COVID-19. Najaribu kufuata, lakini sipati picha kamili. view
  • 3 Mar 2020 in Senate: Bi Spika wa Muda, nami pia nasimama ili kuzungumzia swala la usalama. Ni kweli kabisa kuwa hatuna usalama Kenya, haswa kwenye mipaka yetu. Jana tulionyeshwa kina mama waliokuwa wanakimbia na watoto wakati watu walikuwa wanafyatuliana risasi. Nilipokuwa nikitazama runinga leo asubuhi, kulikuwa na maelezo kuhusu hali ya mipaka yetu katika maeneo ya Turkana na Samburu. Walionyesha watoto wa miaka kumi hivi wakitumia bunduki zilizo na risasi nyingi. Waziri (Dkt.) Matiang’i aliwapa muda warudishe bunduki hizo. Kulikuwa na maandishi kuwa bundiki hizo zinatoka Nigeria na sehemu nyingine. Sijui wanaingilia wapi, ilhali kuna vizuizi kwenye kila mpaka. Hiyo inamaanisha kuwa hakuna usalama ... view
  • 20 Feb 2020 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Naungana na wenzangu katika mjadala ulioko mbele yetu, kwamba Waziri aje hapa ili tuzungumze naye ama tumuulize maswali kuhusu nini anachokipanga kuhusu watu wetu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)