Christine Zawadi Gona

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 81 to 90 of 112.

  • 10 Feb 2020 in Senate: wakimlimbikizia. Kama ni mabaya anaambiwa maneno yote. Kwa hivyo, jina la Moi kwangu limebeba mazuri na pia kukiwa mabaya nayabeba vile vile. Nitabaki kumkumbuka. view
  • 10 Feb 2020 in Senate: Mwaka wa mwisho kuonana na yeye kwa karibu sana nilikuwa Darasa la Nane, mwaka wa 1991. Alikuwa anafungua daraja kule Kilifi. Kama wasichana kuna nyimbo tulimwimbia. Kwa vile kulikuwa na shule moja peke yake katika mji wa Kilifi, tulikuwa tuna msihi tujengewe shule ya wasichana. Baada ya kumwimbia na kumshukuru kwa daraja lile, mwaka uliofuata kuna shule ya wasichana inayoitwa Bahari Girls ilifunguliwa. Hiyo ilikuwa shule yangu ya kwanza kuhudhuria. Kwa hivyo, namkumbuka kwa hilo pia. view
  • 10 Feb 2020 in Senate: Wakati alipohudumu kama Rais, kwa mfano, ikiwa Madaraka Day, maduka yote yalikuwa yanafungwa na watu wote walitakiwa kwenda kwa uwanja. Vile vile, kila duka ililikuwa na bendera. Kulikuwa na heshima na hadhi fulani kwa taifa. Kulikuwa na uzalendo na heshima kwa viongozi. Hungemuona kijana akimtukana kiongozi anavyotaka. Hungemdharau kiongozi ama kutumia maneno mabaya. view
  • 10 Feb 2020 in Senate: Bw. Spika, hata wakati huu wa mitandao na tarakilishi, heshima na nidhamu ni lazima idumishwe. Nitamkumbuka Mzee Moi kwa heshima kubwa na uzalendo ambao alikuwa ameweka kwa taifa hili. Ukiamka asubuhi, nyimbo zilizokuwa zinakuamsha zilikuwa za uzalendo katika redio zetu. Ulikuwa unahimizwa uamke uende kazini na mambo mengi mazuri ambayo tulikuwa tukiyaona wakati ule. Wakati huu, mazuri mengi yamekuja lakini mabaya pia yamefuata. Ningewahisi tuige kile kizuri na kile kibaya tukiache. view
  • 10 Feb 2020 in Senate: Bw. Spika, kwa hayo machache, Mwenyezi Mungu ambariki mahali alipo Mbinguni, amjalie maisha mema huko kama yako, na amlaze mahali pema peponi. view
  • 10 Feb 2020 in Senate: Asante. view
  • 28 Nov 2019 in Senate: Ahsante Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii ili nitoe maoni yangu kuhusu Taarifa iliyo letwa na Seneta wa Tana River. Naunga mkono yale ambayo yamesemwa. Vile vile, ninashangaa. Mvua inafaa kuwa baraka kwa watu wetu lakini kuna wakati ambapo huwa haikuwi baraka bali inaleta maafa na laana kwa watu. Mvua hainyeshi kwa bahati mbaya. Tunajua ya kwamba tuko na msimu wa mvua na msimu wa kiangazi. Ninashangaa ni kwa nini hakuna viegezo vinawekwa ili kuzuia maafa wakati wa mvua. Nasema hivyo kwa sababu tunaishi nyanda za chini, na hata sio sisi peke yetu, kuna Wakenya wengi kule. Mvua inaponyesha, mvua ... view
  • 28 Nov 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 28 Nov 2019 in Senate: lakini akina mama na watoto hupatwa wakiwa ndani wamelala. Tumepoteza akina mama na watoto wengi kwa ajili ya mvuo hiyo. Jambo hili si la jana, leo, wala la juzi; limekupwepo tangu jadi. Ninashangaa ni kwa nini Serikali haingalii namna ya kuokoa maisha. Kwani kila siku tutakua tunakimbia kuwapelekea tents na mabati? Tutafute njia mbadala ya kuhakikisha kwamba, watu hawatapoteza maisha tena. Mvua hii inaponyesha, kuwe na viegezo vitakavyokua vinawekwa, kama kuchimba dams ili maji haya yasipotelee bahari kavu. Tunaviojua, hakuna maji haswa katika sehemu za wafugaji, ilhali mvua inanyesha. Kwa nini hizo dams hazichimbwi sasa ili mvua inaponyesha, kuingie maji ... view
  • 19 Nov 2019 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda, mimi pia ninachukuwa fursa hii kuwakaribisha MCAs wa Kaunti ya Trans Nzioa. Mimi nilikuwa MCA wa Kilifi County. Kwa hivyo, ninawakaribisha. Vile mheshimiwa Wetangula amesema hakuna mipaka kwa yale mambo binadamu anaweza kuyatekelez. Kesho ama kesho kutwa mnaweza kujipata mko hapa. Si maajabu, inawezekana. Ninataka kuwatia motisha ya kwamba, inawezekana. Bw. Spika wa Muda, nilipokuwa kwenye Bunge la Kaunti kulikuwa na mambo kama yale ambayo mmekuja kuangalia hapa. Inafaa mue makini sana wakati mnapoangalia kwa sababu tulipata kuna pesa fulani wanaingiza kwa akaunti kiholehole. Wanaweka mamilioni ya pesa katika hiyo akaunti kisha baadaye yule kibarua ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus