David Ole Sankok

Parties & Coalitions

David Ole Sankok

Nominated by the Jubilee Party to represent Persons living With Disabilities (PWDs) in the National Assembly.

All parliamentary appearances

Entries 1711 to 1720 of 2182.

  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Madaktari waligoma kwa siku mia moja na hili Bunge pamoja na Serikali hatukujitokeza kama vile tulivyojitokeza wakati wa migomo ya waalimu. Hatujatilia maanani mambo ya afya na ndio sababu ninamshukuru Mhe. Mohamed Ali kwa kuileta Hoja hii. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Sio kawaida mtu kufariki katika hospitali ndogo ama zahanati kwa sababu wagonjwa wanaelekezwa katika hospitali ambazo zina vifaa. Lakini madaktari, kwa sababu ya kukosa kulipwa vizuri, wanajaribu hivi na vile katika hizo hospitali ndogo mpaka wagonjwa wanaaga dunia. Hoja hii itawafanya madaktari pia wawe waangalifu. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Kama mgonjwa akifariki daktari hatalipwa ada ya hospitali, yule daktari atajaribu juu chini kuokoa maisha kwa sababu hayo maisha yameshikanishwa na pesa zake za huduma. Iwapo daktari hatalipwa mgonjwa akiaga dunia, basi atajaribu vyovyote vile ili aokoe huyu mgonjwa kwa sababu hivyo ni kuokoa pesa zake. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Wakati mwingine tukihimiza Serikali katika Miswada, ni kama kuomba Serikali itusaidie, nao wananchi ambao walijitokeza mapema kutuchagua, wakasimama kwa jua, mvua, vumbi na upepo mwingi wakituomba, wanahuzunika tunapokosa kuwahudumia. Ninamuomba Mhe. Ali abadilishe hiyo sentensi iamrishe Serikali. Hii ni kwa sababu Bunge hili linagawa rasilimali za nchi hii. Tunafaa kutoa amri ya kwamba hamna mgonjwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: ambaye atalipishwa pesa za hospitali wakati ameaga dunia, haswa, ada ya hospitali. Sisi hatufai kuomba, bali kutoa amri. Sisi ndio tunabeba mfuko wa mali ya pesa ya wananchi. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Inasikitisha pia kusikia kwamba mzazi anashindwa kulipa ada ya hospitali ya mtoto wake na inabidi amuibe yule mtoto bila kupenda kwake. Sisi Wabunge na Serikali tulitangaza kwamba matibabu itakuwa bila malipo lakini mgonjwa akifika kule anaambiwa alipe na ikabidi aibe mtoto wake. Hii inahuzunisha sana na ingetakiwa kuamsha kilio cha Bunge hili ili kuamrisha Serikali iweze kulipia watoto ada za hospitali, sio tu wale ambao wamekufa, lakini hata wale ambao wanaishi. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Hivi juzi, mama alilazimishwa kubeba maiti ya mtoto wake kwa umbali wa kilometa tano. Hata kama hatuna utu, hata kama sisi tumepata nafasi ya kupata mshahara, mtoto kuaga kwa mikono yako inaumiza roho. Mama huyo alikuwa katika kilio halafu baadaye anaambiwa aipeleke maiti kwa polisi. Kumpoteza mtoto ni uchungu sana na ukibebeshwa hiyo maiti kwa umbali wa kilometa tano ni uchungu zaidi. Sisi Wabunge na hata Serikali hatujatilia maanani umuhimu wa afya ya wanachi wetu. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Kwa hivyo, ningesema kwamba huduma ya afya irudishwe kwa Serikali kuu ili tuweze kuwa na msemo kama Bunge la Taifa. Hata tukijaribu kupitisha Hoja kama hii, itabidi iende katika Seneti au bunge za kauti ili iweze kupitishwa. Kama afya ingekuwa katika Serikali kuu ingekuwa rahisi kwetu kupitisha Hoja hii. Kwa hayo mengi, naunga mkono Hoja hii mia kwa mia ili iweze kuwasaidia wananchi wetu, haswa kwa maneno ya afya. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Pia, ningetaka kuwashukuru sana watu wa Nyali kwa sababu inaonekana kwamba ule uchunguzi Mhe. Mohamed Ali alikuwa akifanya katika Jicho Pevu haukuwa wa bure. Amekuwa na jicho pevu la kuangalia maslahi ya Wakenya wote, sio watu wa Nyali peke yao. Kwa hivyo, na waambia asante sana. Pia, ninawahimiza Wakenya kuchagua vijana chupavu kama Mhe. Mohamed Ali ili tuwe na Bunge ambalo litaleta Miswada ya maana ya kuwasaidia wananchi wa taifa la Kenya. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus