Davis Wafula Nakitare

Born

7th May 1943

Post

P. O. Box 126 Endebess

Email

nakitare@africaonline.co.ke

Telephone

0722489317

Telephone

0735669729

All parliamentary appearances

Entries 181 to 190 of 895.

  • 8 Nov 2023 in Senate: Tumejadili mambo ya wahubiri na lazima wawe wa ukweli. Viongozi pia wawe wa ukweli. Fisi aliambia mawe, ‘hata tukinyamaza vipi, mmesikia’ na lazima tupige kura turekebishe mambo ya Meru. Asante, Bw. Spika. view
  • 2 Nov 2023 in Senate: Asante, Bw. Naibu wa Spika. Nashukuru kwa nafasi hii kwamba mhusika mkuu katika mchakato wa kubanduliwa nje ya kiti apewe nafasi hii kujieleza wazi, Wakenya wakisikiza. Vile vile, madai ambayo viongozi wa wadi wako nayo, waje wajieleze na stakabadhi zinazoweza kudhibitishwa na Seneti. Halafu, kama ni kunyolewa, watu waandae maji, sabuni na haki itendeke kwa yeyote ambaye atakuwa na makosa. Iwapo hana makosa, atasamehewa. Ninavyofahamu ni lazima kila mtu awajibike katika uongozi. Tutakuwa tunampa nafasi, yeye na Bunge la Kaunti, ili waaajibike kutokana na hoja watakozoleta Seneti. Gavana na wenzake wawe kielelezo kwa magavana wengine Kenya hii watakaojipata katika hali ... view

  • 2 Nov 2023 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. Ningependa kuanza na ya kwanza. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu Nambari 53(1) kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Elimu, kuhusu ongezeko la visa vya mimba za mapema kwa wanafunzi wa shule za upili katika Kaunti ya Bungoma. Katika kauli hiyo, Kamati iangazie yafuatayo - (1) Iarifu Seneti kuhusu idadi ya wanafunzi wa shule za upili katika Kaunti ya Bungoma waliopata mimba mwaka huu wa 2023, ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2022. (2) Ibaini sababu zinazopelekea kuongezeka kwa visa hivyo vya mimba za mapema, hususan katika shule ya Upili ya St. Thomas ... view

  • 2 Nov 2023 in Senate: (3) Ieleze hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya wahusika waliowapachika mimba wanafunzi hao, ili kukomesha hali hii ambayo imeathiri viwango vya masomo katika kaunti hiyo. view

  • 31 Oct 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa wakati huu kuchangia. Wakati gavana huyu alikuwa hapa kujitetea alipoletwa na kaunti yake husika, aliponea chupuchupu. Utetezi wake ulifanywa katika kikao ambacho hatukuwepo lakini kwa sababu ya uamuzi wa jumla wa Seneti kwamba waliyokubaliana nayo pia sisi tukubali, tukakubali shingo upande. Watu wa kaunti hii wana mambo ambayo wangependa kusikia yakitajwa, yakijadiliwa na yakizungumziwa peupe mchana. Pia wanataka kujua rafiki yao ni nani na asiyekuwa rafiki yao ni nani. Wanataka kujua kama Seneti inajua yanayoendelea katika kaunti yao ama hapana. Wanajua kwamba katika majadiliano ya watu wachache, kuna mazungumzo ya chini kwa chini ambayo hao ... view
  • 31 Oct 2023 in Senate: Leo, wana nafasi kusikia wazi. Wale wanaoitwa madaktari, maprofesa na walimu wadhihirishe uwezo wao wazi mchana kadamnasi. Ni wapi ama ni shinikizo zipi zinahakikisha kwamba wanapata haki ama nafasi ya kujieleza kwa sababu Seneti ni Bunge la kutetea ugatuzi. view
  • 31 Oct 2023 in Senate: Iwapo viongozi kama Wabunge wa Kaunti wamekata kauli kwamba lazima Pilato awape nafasi wamsulubishe Barnabas ama Yesu, sisi ni nani tuje hapa tuchukue nafasi yao kana kwamba hawana akili ilihali ni watu timamu kuambiwa hatima yao? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus