All parliamentary appearances
Entries 221 to 230 of 895.
-
20 Sep 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
-
20 Sep 2023 in Senate:
kukimbia, ni kama umemuona nyoka. Ndio hayo ninayoona katika Jumba la Seneti. Ukimuona nyoka, toroka. Yale ambayo tumependekeza kama Kamati ya Mamlaka na Heshima ya Bunge ni kali, lakini unapoyavulia, lazima uyaoge.
view
-
20 Sep 2023 in Senate:
Namuonea huruma. Tunaweza punguza nusu lakini mwezi moja iwe ya matibabu kisha miwili awe nje ya Bunge. Hiyo ni miezi mitatu na nyinyi mnajuwa mambo ni matatu.
view
-
20 Sep 2023 in Senate:
Sitaki kupita hapo, ila naomba Maseneta tufanye kazi pamoja; tuwe na heshima. Kiongozi kama Nyegenye amechukuwa miaka mingi ya kusoma kuwa na tajriba, ana familia, hadhi na kutambulika kote ulimwenguni. Haiwezekani mtoto bado ananyonya anakuja kumpaka tope. Sisi tutasimama na mapendekezo na nadhani kwamba heshima itadumu katika Jumba la Seneti. Kwa hayo mengi, wanaume wenzangu, tukaze kamba tujitetee tunapotetea wanawake, lakini wasitumie uume wetu kama donda la kufanyia mzaha. Nikimalizia, nyinyi mnakumbuka kuna matamshi wamekuwa wakisema kama una kile kitu kitumie kikupe kile unachokitaka. Sijui ni kitu gani, shangaeni tu. Hata mimi nashangaa ni kitu gani. Lakini hicho kitu ni ...
view
-
3 Aug 2023 in Senate:
Point of order
view
-
3 Aug 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kwa mujibu wa Kanuni 105 ya Kanuni za Kudumu za Seneti, lazima Seneta awajibike kwa matamshi yake. Sisi kama Maseneta na viongozi wa Kenya Kwanza tulikula kiapo kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba na kuhakikisha ugatuzi unafanya kazi. Sen. Osostsi hawezi kujilimbikizia heko kwamba kama siyo wao, kaunti zetu hazingepata pesa. Hiki ni kinaya kwa sababu sisi kama Walio wengi katika Serikali tuna vikao vya mara kwa mara na Mhe. Rais. Haya ndio masuala sisi hujadili kwa minajili ya kusukuma ajenda ya maendeleo za gatuzi zetu. Naomba asiwe wa kujipiga upato kwa sababu hata hapa Seneti ...
view
-
2 Aug 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika kwa nafasi hii na vile vile kumshukuru Waziri kwa kazi ambayo anafanya. Anadhihirishia Wakenya ya kwamba kando na kuwa mwanasiasa, mwanamke pia ana uwezo wa kufanya kazi kando na kanuni za kijinsia zilizowekwa na tamaduni zetu. Tumeona miradi mingi ya maendeleo ya maji katika kaunti mbalimbali humu nchini. Katika Kaunti ya Bungoma, kuna mradi wa maji inayotoka Mlima Elgon ambao unaofadhiliwa na nchi za kigeni. Tunashukuru kwa sababu unaenda kuchangia pakubwa kwa wakaazi wa mji wa Bungoma, Kaunti nzima pamoja na Kaunti ya Busia kupata maji.
view
-
2 Aug 2023 in Senate:
Je, katika mustakabali wa Serikali wa upangaji kazi, ni mradi upi mwingine wa kitaifa umeratibiwa katika Bajeti ambao unanufaisha wakaazi wa Kaunti ya Bungoma na Kakamega ambao ni majirani wetu? Ili watu wanapo sherehekea na kukupa heko, tusipitwe na miradi ya mandeleo ya maji.
view
-
2 Aug 2023 in Senate:
Naelewe kuwa tumekuwa tunajadiliana na we kupitia vyombo mbali mbali na baadaye najua tutaendelea kuzungumza. Kwa sababu, wanasikiza kutoka kule nyanjani, itakuwa vyema kutaja kwa kifupi mradi upi tunaenda kupata. Hii ni kwa sababu walikuwanatazamia katika mipangilio yako, maji ya Nabuyore yatatumika kuliunda bwawa ambalo litatupa maji katika maeneo bunge zaidi ya nane.
view
-
2 Aug 2023 in Senate:
Sitaki kusema mengi. Natarajia kwa moyo mkunjufu jibu la Mheshimiwa Waziri.
view