Davis Wafula Nakitare

Born

7th May 1943

Post

P. O. Box 126 Endebess

Email

nakitare@africaonline.co.ke

Telephone

0722489317

Telephone

0735669729

All parliamentary appearances

Entries 241 to 250 of 895.

  • 26 Jul 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Jambo tunayozungumzia sasa inaweka Mawaziri katikati ya jiwe na pahali pagumu. Yule ambaye aliwateua na anawaamini kwa uchapakazi na uadhilifu wao ameona kwa hekima yake kuwapa nafasi kusafiri naye katika nchi za ng’ambo kutetea nafasi na hadhi ya nchi ya Kenya na mustakabadhi wa Wizara zao na nchi wanayokwenda. view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Hapa sisi kama wawakilishi na watumwa wa wapigaji kura, vile vile tunadai wakuje hapa kutupa majibu yao. Ni kama shingo kuuliza kichwa: “Mbona hautumiki kumeza chakula unachotafuna?” view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Bw. Spika, naomba kwamba Bunge la Seneti na wachapakazi wake wawe na udiplomasia wa mapema, kujadili ratiba na mipangilio kwa mapema. Vile vile Mawaziri na wasaidizi wao wawe na mawasiliano ya karibu na Bunge la Seneti ili mipangilio yao isilete aibu mbele ya Wakenya. view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Kwa mfano, sisi ni Serikali. Wale tunaoshutumu ni wachapakazi wa Serikali. Itakuwaje mkono mmoja unaukata mwingine kwa madai kwamba mkono huu haujathibiti majukumu tuliyoupa? Mimi kama mmoja wa Maseneta wa Serikali, tutawarai viongozi wenzangu katika Serikali tuwe na kikao na tusemezane haya maneno. Hii ni kwa sababu, hatuwezikuwa tunakuja hapa kulia na baadaye tena, tutakaa Mawaziri kupanga agenda ya nchi. Asante, Bw. Spika. view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Asante, Mhe. Spika wa Muda kwa nafasi hii. Ningependa kuchangia machache kuhusu Mswada ambao Seneta ameibua kwamba lazima serikali za kaunti ziwe na mfumo wa elektroniki utakao tumika kuhakikisha kwamba watu wanapata leseni zao kwa wakati unaostahili. Vile vile, kupitia mfumo huu, itakuwa rahisi kufuatilia ni watu wangapi wamesajiliwa na kupewa leseni za kufanya kazi katika kaunti husika. Mswada ambao Seneta ameleta, ni kuhakikisha kwamba Serikali itakuwa na kumbukumbu za majina, kampuni na biashara zinazohusika katika kaunti husika. Wakati ambao wanawasilisha stakabadhi zao kuhakikisha kwamba biashara zao zinapewa leseni ni rahisi serikali kupata stakabadhi, majina ya wenye kampuni na kampuni ... view
  • 26 Jul 2023 in Senate: Sasa ni jukumu la serikali husika kupitia stakabadhi hizi na kuwapa walioomba nafasi majibu kwa wakati unaostahili. Wasipofanya hivyo, wanabiashara hao wataendelea kufanya kazi zao, kwa sababu, Mswada ulioletwa hapa unajukumisha washika dau katika kaunti kufanya kazi zao jinsi inavyostahili. Mhe. Spika wa Muda, mwisho kabisa, vijana na wale ambao ni chipukizi katika biashara wataweza kupata nafasi ya kulipia ushuru au leseni zao kwa awamu moja. Katika mfumo wa elektroniki, anapobonyeza na iwapo anataka kupata leseni mbali mbali, mfumo huu unamwezesha kupata idhini kwa wakati unaostahili na wakati huo. Sio jinsi inavyotendeka sasa. Wafanya biashara hao au wawekezeji hao wanatundika ... view
  • 25 Jul 2023 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii. Namuomba samahani ndugu yangu Sen. Cherarkey. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 25 Jul 2023 in Senate: Kulingana na Kanuni za Seneti Nambari 105, yale yanapaswa kujadiliwa ni mambo ya ushuru wa aina nyingi unaotozwa. Sielewi mustakabali wa hoja za ushuru na utupaji wa mawe, sufuria kwenye vichwa, tetesi dhidi ya viongozi wasio hapa na ushuru ambao unalipwa. Sijaona ushuru kwa sufuria wala kwa mambo haya. Naomba Seneta adhibitishe uhusiano wa viambajengo ambavyo ametaja na mada iliyoletwa na ndugu yangu Seneta. Asante. view
  • 18 Jul 2023 in Senate: Madam Temporary Speaker, on a point of order. Pursuant to Standing Order No.105, my good friend alleges of people being taken to DCI by his Excellency the governor. Is it in order for the good advocate /barrister to allege that bloggers or young people working online will end up being disabled by the current governor? Is it in order to say that boda boda are bad people? Are you talking about boda boda riders or the motorbike itself? view
  • 18 Jul 2023 in Senate: Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie yale ambayo Sen. Maanzao ametaja. Katiba inatupa ruhusa ya kumiliki mali na rasilmali hapa Kenya. Yale yanayojiri ni kinaya na kinyume na matarajio ya wanademokrasia hapa Kenya. Sisi Wakristo tunajua kuwa maandamano ni kubeba matawi na mabango kwa amani. Tumekuwa tukishuhudia maandamano ya madaktari, walimu na wakulima. Wakati wa maandamano, hatujawahi kuwa na bughdha au purukushani yeyote, uharibifu wa mali na watu kuumia. Sijui wanademokrasia hao wanaandamana kushinikiza nini. Sijui wanataka tupoteze maisha ya watu wangapi ili wajue kuwa ni maandamano. Sijui wanataka watu wangapi wajeruhiwe ili waseme kuwa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus