Davis Wafula Nakitare

Born

7th May 1943

Post

P. O. Box 126 Endebess

Email

nakitare@africaonline.co.ke

Telephone

0722489317

Telephone

0735669729

All parliamentary appearances

Entries 381 to 390 of 893.

  • 21 Feb 2023 in Senate: Ningependa kuwarai mawaziri wa kilimo na serikali za kaunti kwamba sisi kama Bunge la Seneti tutamulika hawa watu na “kuwapuliza doom” kuhakikisha kwamba pesa za Kaunti zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Pesa hizi zitakapofika nikuhakikisha kuna mstakabadhi mwema kati yetu, magavana na serikali ya Kitaifa. Sitarajii kwamba watakapopata pesa wakose kulipa pesa ambazo zinaenda kwa halmashauri ya afya, halmashauri ya kijamii (NSSF), na vile kulipa ushuru. Katika vitabu vya hesabu tumeona wafanyikazi wa serikali wanalipwa mishahara lakini pesa zitakazo lipa ushuru katika serikali ama kugharamia matibabu katika sekta ya afya hazitumwi katika National Hospital Insurance Fund (NHIF) . Hizi pesa zitakapofikia wafanyikazi, wapewe haki yao kwa kulipa ushuru, NHIF na NationalSocial Security Fund (NSSF), haya madeni yaondolewe. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Kuna wanakandarasi ambao kwa muda mrefu pesa zao hazijalipwa. Haiwezekani tuwe tunawapa pesa kila uchao lakini hawalipi madeni ya wafanyikazi na wanakandarasi. Tuhakikishe wale wachapa kazi wa mashinani walipwe pesa zao, wale ambao wako katika ratiba ya mwaka 2023/2024 wapewe pesa zao, ili kwa pamoja tusonge mbele na tuimarishe nchi yetu ya Kenya. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Asante sana. view
  • 16 Feb 2023 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Ningependa kushukuru uteuzi wa Seneta mwenzangu aliyechaguliwa juzi kuhudumu katika Kamati ya Teknolojia. Wakati huu sasa, watu wanasonga katika mawimbi ya teknolojia na tuliwaahidi Wakenya kwamba shule za msingi, upili na vyuo vitaunganishwa na teknolojia. Tumeshuhudia mtandao wa pesa za bottoms-up, zile za Hustlers Fund unavyochunguza kupitia teknolojia. Sote tuliopewa nafasi kama mimi kuhudumu katika Kamati ya Ukulima, tutashughulikia masuala ya miwa, ngano na mifugo maeneo yaliyo na ukame ili kuhakikisha Wakenya wananufaika katika Serikali ya Kenya Kwanza. Bw. Naibu Spika, naunga mkono Hoja huu. view
  • 14 Feb 2023 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I would like to reiterate what my senior brother has said. This country is in a turmoil and needs a lot of panel beating. Issues have been raised about consultation and partisan positions in the House. I would like to request that we have the Senate Business Committee and not “ Azimio party Business Committee. Mr. Speaker, Sir, we were elected for a reason and I request that we stick to this agenda of the SBC. We should proceed to vote, so that we allow this Committee to continue with its work. I thank you. view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Asante, Mwenyekiti wa Muda, kwa nafasi hii ambayo umenitunuku. Ni nafasi yangu ya kwanza kutaja au kuchangia pakubwa kuhusiana na swala la IEBC na mchakato mzima wa kikosi cha kuchagua watu hawa. Tume ya Serikali ambayo inahusishwa pakubwa kuajiri watu kazi ni lazima ipewe nafasi yake kikatiba ili iwape Wakenya watu ambao wana tajriba, wakakamavu, historia yao inaeleweka na wanaweza kuwajibika katika majukumu yao. view
  • 19 Jan 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Iwapo Bunge hili la Seneti litawapiga mgongo ama kuwakata miguu, itakuwa tunawaambia Wakenya tume hiyo haina haki ya kufanya kazi kikatiba jinsi ilivyokuwa inafanya. Mimi ninapinga mabadiliko hayo nikisema kwamba Mswada huu uendelee kama ulivyotoka katika Bunge la Kitaifa, ili tuwakikishe kwamba tunafiki malengo ya kidemokrasia na ya Serikali kuhakikisha kwamba kura zinapopigwa, zinawajibika, kueleweka na matokeo yanawafurahisha Wakenya wote. Kwa hayo, ninapinga mabadiliko haya na tuende pamoja kama Bunge la Seneti. view
  • 17 Oct 2007 in National Assembly: Mr. Deputy Speaker, Sir, for record purposes, could the Assistant Minister tell us whether after it was discovered that Mr. Ayanu was not the Mau Mau war veteran Gen. Mathenge, the Government continued to pursue the whereabouts of this hero or whether the October 17, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 4521 search was terminated? The Government of Kenya never involved the Ethiopian Government in finding out more about Mr. Ayanu before money was spent on him. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus