Davis Wafula Nakitare

Born

7th May 1943

Post

P. O. Box 126 Endebess

Email

nakitare@africaonline.co.ke

Telephone

0722489317

Telephone

0735669729

All parliamentary appearances

Entries 371 to 380 of 893.

  • 1 Mar 2023 in Senate: tunaidhisha zitumwe kwa kaunti, zipate mikono safi, watu wenye mioyo safi na wawajibikaji, ili wakulima pale mashinani waweze kupata haki yao. Naunga mkono Mhe. Osotsi na kusema kwamba tupanue mtazamo wetu kuhusiana na pesa hizi katika kaunti zote nchini Kenya ili katika mfumo wa Kenya Kwanza kuboresha ukulima, watu tuanze katika awamu safi ili kuwe na uhakikisho kwamba pesa za mtoza ushuru zinafanya kazi kwa mujibu wa katiba. Asante sana, Bw. Spika. view
  • 1 Mar 2023 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. Nikichangia kwenye hii taarifa ya usalama, nimekuwa nabukua mtandao wangu nikaona vikosi vyetu vya usalama vikifanya mazoezi na kuzuru maeneo mbalimbali kule Congo. Wakenya walikuwa wanafurahi sana wakijipigia upato kwamba Kenya ina kikosi cha uzoefu mkubwa wa kukomboa miji mbalimbali katika Bara la Afrika. view
  • 1 Mar 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 1 Mar 2023 in Senate: Ni kinaya sana sasa vikosi vyetu vimevaa mavazi ya kivita kule Congo na Somalia, na huku kwetu vijijini Wakenya wanamlilia Mungu wakiuliza ni makosa gani walifanya? Tumeona viongozi wakipaa kwenye ndege na magari ya kifahari yakitua na kuenea maeno haya ya vita lakini mpaka sasa hatujaona hatua yoyote ikichukuliwa. Mimi husema “mzaha mzaha utunuka usaa”. Haya ambayo wanafanya sasa wakitarajia kwamba ni ozoefu, yatakuja kuenea maeneo mengine nchini Kenya na watu wataanza kujipanga kisirisiri. Naomba Serikali iwache kufanya mchezo, iende katika maeneo haya ipambane na hao watu. Itakuaje tuko na idara ya ujasusi Kenya hii ambayo vile vile tuanaambiwa ina ... view
  • 23 Feb 2023 in Senate: Bw. Spika wa Muda, asante kwa nafasi hii. Ningependa kuunga mkono na kushukuru yale ambayo wakili, Sen. Mungatana, amewasilisha. Nimeona ya kwamaba ni kama mazoea ya viongozi wa Afrika kuwa na ugumu wa kutekeleza majukumu yao pasipo shinikizo za kisheria an zaidi ya hapo, kupewa adhabu kali. Tumekuwa katika Kamati mbali ambazo tumeona Kaunti zinakosa kujukumika kulipa mishahara, kodi, halmashauri za afya, watendakazi ama wanakandarasi. Haya yote yataweza tu kupata matibabu iwapo sheria ambayo ndungu yangu Seneta analeta. Itaweza kufanya kazi. Iwapo kaunti imepewa pesa za mishahara, yule anaye jukumika kulipa mishahara anapokosa kulipa ushuru, lazima apate kichapo cha mbwa ... view
  • 22 Feb 2023 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii kutoa ushauri wangu na kongole kwa viongozi wa Chuo Kikuu cha kutoka sehemu ya Ukambani. Vilevile, naona vipusa wa shule ya upili ambao wamekuja kujionea kwa macho Bunge la Seneti ambalo lina weledi wa kutunga sheria na kuchanganua masuala ya siasa. Pia, kuchanganua masuala ibuka katika nchi ya Kenya. Hii Bunge ambayo ina wazee wengi ambao wana tajiriba ya miaka mingi. Waswahili husema palipo na wazee hapaharibiki neno na palipo vijana chipukizi, wazee hutoa jasho. Hivi kwamba ni kuwaambia viongozi wa vyuo vikuu ambao wako hapa kwamba wao ni kielelezo ama ... view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Ahsante Bi. Spika wa Muda kwa fursa hii ambayo umenipa kuchangia hususan mada ya kuangazia pesa zinazokwenda mashinani. Tunapopiga kurunzi mashinani, kuna kaunti ambazo kwa sasa zimeshindwa kuwapa wakulima pembejeo na mbegu za ukulima kwa sababu fedha hazipo. Hizi pesa zitakapoachiliwa, ninatumai ya kwamba wakulima watapewa nafasi bora, wanawake na mayatima ili waweze kujipanga katika musimu huu wa upanzi. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Vilevile, Serikali imetoa mufumo mpya wa kutoka kidato cha saba, cha nane hadi shule za upili. Hivi kwamba inahitajika miundo mbinu ambayo watoto wataweza kupata madarasa, madawati na vitabu. Vyote hivi vinahitaji pesa ili yote yawezekane. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 21 Feb 2023 in Senate: Katika sekta ya kilimo, kuna viwango mbalimbali ambazo serikali imeweka pesa. Lakini ndani ya serikali kuna kupe ambazo hujificha katika miradi hii na kufuja pesa za wakulima. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus