Davis Wafula Nakitare

Born

7th May 1943

Post

P. O. Box 126 Endebess

Email

nakitare@africaonline.co.ke

Telephone

0722489317

Telephone

0735669729

All parliamentary appearances

Entries 351 to 360 of 993.

  • 18 Jul 2023 in Senate: Hawasemi chochote. Bei ya unga imekuwa juu, hakuna mtu anapinga. Ukienda Tanzania, Uganda na nchi za Ughaibuni, hali ya maisha imepanda. Sijaona waingereza ama ndugu zetu Watanzania wakibeba sufuria vichwana. Falsafa ya sufuria kichwani imetoka wapi? view
  • 18 Jul 2023 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kwa mara ya kwanza katika Kenya hii, yale ambayo viongozi wanatamka mbele ya uma na kupiga vifua kwamba lazima nchi isimame, biashara zivunjwe, hiyo si demokrasia wala haki ya Wakenya. view
  • 18 Jul 2023 in Senate: Ninaomba kama viongozi tumakinike, tuwe jasiri na tusimame wima. Tujadili na tubainishe mbichi na mbivu kikatiba; tusuluhishe mambo haya lakini sio yale ambayo naona kwenye barasi za nchi ya Kenya. view
  • 18 Jul 2023 in Senate: Mwisho kabisa, kuna tabia mbovu ambayo nimeona. Ndugu zetu wanatumia vyombo vya habari kusambaza--- view
  • 18 Jul 2023 in Senate: Madam Temporary Speaker, it is a point of information. view
  • 18 Jul 2023 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. Arifa ambayo ningependa kuongezea ni kwamba, kulikuwa na Waziri wa Ukulima Kenya hii na alipewa Kshs14 billion kuhakikisha mahindi na nafaka imepandwa katika Galana Kulalu. Lakini alipongatuka ofisini, hata magunia ishirini pekee yake hangeweza pata. Bilioni kumi na nne na sasa wameungana kubeba sufuria kwenye vichwa, ni kinaya na kejeli kwa democrasia ya nchi hii. Asante, Bi. Spika wa Muda. view
  • 18 Jul 2023 in Senate: Asante, Bi Spika wa Muda. Kanuni za Kudumu No. 105, sielewi mbona Mheshimiwa anahashiria kwamba wanao ingia kwenye Bunge hili kama Maseneta huwa wanaashiria kutumia vileo ama mihadarati wanapo fanya kazi zao. Naomba adhibitishe ama aombe msamaha. view
  • 18 Jul 2023 in Senate: On a point of information, Madam Temporary Speaker. view
  • 29 Jun 2023 in Senate: Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ya kuwakaribisha waalimu wenzangu ambao wameongoza kikosi cha mabinti wenye nishati mpwito mpwito. Wamezuru Seneti siku ya leo kujionea kwa macho yale yanayoajiri hapa. Shule hii imo miongoni mwa shule zinazobobea kimasomo katika Kaunti ya Bungoma. Ni shule mojawapo ambayo kiongozi wa akina mama Mhe. Catherine Wambilianga alizindua mchakato wa kuboresha masomo na fedha za bursary katika Kaunti ya Bungoma. Ni shule mojawapo ambayo waasisi wake ni kanisa la Friends . Shule hii inatambulika kwa michezo, uimbaji wa kwaya na talanta mbalimbali. Mimi ninajivunia waalimu na wanafunzi ambao wako hapa. Ni kielelezo ... view
  • 29 Jun 2023 in Senate: Asante Bi. Spika wa Muda kwa fursa hii ambayo umenitunuku ili nikaribishe wanafunzi na walimu wa Friends School, Bwake. Chanzo cha jina Bwake ni Kaunti ya Bungoma. Hii ni ishara kwamba kitaasisi ama kiafrika, watu hugura kutoka eneo moja hadi lingine. Hawa jinsi walivyo hapa, ni ndugu zangu kutoka Kaunti ya Trans Nzoia. Wazazi wao walitia jitihada ili wawe katika uhai huu na shule hii. Walimu vilevile ambao wamehakikisha wanafunzi wamekuja hapa, wanaelewa kwamba, jukumu la Bunge la Seneti ni kutunga sheria. Hususan, kudhibiti matumizi ya fedha katika kaunti, kutunga sheria, kuafiki malengo ya ugatuzi na pia kupambana na ufisadi ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus