All parliamentary appearances
Entries 341 to 350 of 893.
-
15 Mar 2023 in Senate:
Sen. Osotsi amesema kwamba wakati huo kulikuwa na mibabe ama mafidhuli. Kulikuwa na kundi la wanabiashara ambalo lilikuwa limejipanga kuteka nyara nchi hii kupitia teknolojia lakini Bw. Wangusi alisimama kidete. Aliwapa Wakenya nafasi ya kujiandaa kwa mfumo mpya wa mawasiliano.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
Vyombo vya mawasiliano vimeenea nchini humu kwa sababu wa uongozi wa Bw. Wangusi. Vile vile, kulikuwa na siasa kati ya kampuni za Safaricom, Airtel na Telkom. Bw. Wangusi alisimama kidete na kusema kuwa kila kiwanda na mwanabiashara lazima atii sheria na kuafiki malengo ya Serikali. Hadi wa leo, vita hivyo vimetulia na kila mtu anatafuta shilingi yake kwa haki.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
Sisi kama watu wa Bungoma tumempoteza kiongozi shupavu. Langu ni kurai Serikali kwamba iwapo wafanyakazi wamefanyia kazi kwa muda mrefu na wana tajriba ya juu, si vyema kuwatelekeza na kuwarudisha mashinani ilhali weledi wao, historia yao na kumbukumbu za kazi zinahitajika kwa vizazi vijavyo.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
Kwa familia ambayo naijua binafsi, kwa niaba ya viongozi wa Kaunti ya Bungoma na wananchi wa Kaunti ya Bungoma, tunasema pole. Mungu hupeana na Mungu hutoa. Mimi naamini tutakutana kule Paradiso ambao ni mji wa asali na maziwa. Tutakumbuka umbali tumetoka. Ee Mungu, anapoenda Wangusi, tupe muda zaidi tuishi Kenya hii tunyoroshe mambo ili tutakapokutana na Wangusi tutasema it has been a good journey . Mungu atuneemeshe na tufikie hatima ya mapenzi yake.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kwa hayo mengi, nashukuru kwa nafasi hii.
view
-
14 Mar 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Ijumaa na Jumamosi tulikuwa na kikosi cha Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kule Kaunti ya Kitui. baadhi ya maswali ambayo mwenzangu Spika ameuliza ni maswali ambayo wakulima wa ndengu waliuliza. Kwa mfano, ni mbolea mifuko mingapi ambayo imeletwa maeneo hayo na ni vigezo vipi waliotumia kuwapa wakulima mbolea hiyo? Katika kumbukumbu na vitabu vya wataalam wa kilimo, ekari moja ya shamba iwapo ni la mahindi huhitaji magunia kadhaa ya mbolea. Wanayosema yameafikiwa na Idara ama Kilimo ama hii ni mbolea ambayo imekuwa inapeanwa tu kwa minajili ya kukimu kiu cha wakulima Kenya? Hoja ...
view
-
14 Mar 2023 in Senate:
Tungependa kujua Serikali imepeleka magunia ya kutosha? Maeneo ya Trans-Nzoia, Bungoma na Kakamega mvua imeanza na wakulima wameanza kupanda. Iwapo mbolea ni chache, Kamati ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, tutaweka majembe yetu chini ili kuhakikisha kuwa wale ambao wanapaswa kufanya kazi wanaifanya kikamilifu. Ninaunga mkono.
view
-
14 Mar 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda. Katika maeneo mbalimbali humu Kenya kuna ukataji miti katika maeneo ambayo yametajika jinsi ulivyosikia. Nadhani ni mpango ambayo mabepari wa kisiasa wako nao kuhakikisha maeneo fulani humu nchini yanapoteza uridhi wake. Kwa mfano, misitu ya Kaimosi, kiitikadi na kijamii, mila na desturi za Watiriki hufanyika katika misitu hii. Haiwezekani kupata watu kuja tu na mashine kukata miti pasipokubaliana na washikadau maeneo haya. Pia, misitu ya Malava na mlima Elgon. Ninaomba kwamba, iwapo kuna njama ya Serikali ama wale waliomo serikalini na mafidhuli wanabiashara, sisi kama Maseneta kutoka maeneo yetu tupambane na wao kule mashinani. Kama ...
view
-
9 Mar 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ningependa kuchukua mwelekeo ambao Kiongozi wa Wengi amechukua. Hususan changamoto, shida na unyanyasaji wa Wakenya ambao ulitekelezwa na Wakoloni, vizazi vya Wakoloni ama Waafrika wanaoendeleza ukoloni mamboleo.
view
-
9 Mar 2023 in Senate:
Yale ambayo yanaendelea katika Kaunti ya Kericho na sehemu mbalimbali humu nchini, lazima yakome. Ni lazima Serikali ya Kenya Kwanza tuhakikishe kwamba wale ambao mashamba yao yalichukuliwa, wapate haki yao.
view