All parliamentary appearances
Entries 331 to 340 of 893.
-
15 Mar 2023 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Ninapoona wenzangu wa mrengo wa Azimio kwa wiki tatu au nne hivi wakija, wanasujudu na kutoka, wakifuata yale wanaamini ni yao, inanikumbusha falsafa ya fisi.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
Kwamba fisi hakati tamaa. Hachoki hadi atakapopata.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
Naona wametulia kwa sababu wakikutazama uso wako wanajua wamepata kile wanachotaka. Lakini maheremu Kijana Wamalwa alisema, iwapo tunataka kuwa viongozi, lazima wakati mmoja ukubali kwamba unaweza kubali watu wapande kwa mabega yako waafiki malengo ya taifa. Japo mtapata kile mnataka, tafadhali wakati unaokuja, weka Kenya kwanza halafu viti vyenu vya kibinafsi vije baadaye. Asante, Bw. Spika.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa nafasi hii tunapoomboleza kifo cha Bw. Wangusi.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
Wangusi anatoka Eneo Bunge la Sirisia. Ana makazi Eneo Bunge la Kimilili na vile vile Eneo Bunge la Kanduyi. Ukienda kule mashinani, wengi walikuwa wanamjua kama Mzee Wangusi kwa sababu alikuwa mpole na mcheshi. Hakuwa mtu wa kujigamba ama kutembea na maafisa wa polisi ili kuwatisha wananchi.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
Kila mara mwaka ulipoanza na katika hafla za kitaifa, alikuwa anawaalika watu katika makazi yake ili kula na kunywa nao. Watu wetu husema kwamba mkikaa ama kunywa na mtu, si kwamba huna kile anachokupa, lakini mnafurahia gumzo ama mazungumzo nyumbani kwake.
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
Sisi kama wakazi wa Kaunti ya Bungoma tumepoteza mchapakazi. Nitamlinganisha na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi, yani
view
-
15 Mar 2023 in Senate:
, Bw. Chebukati kwa sababu si rahisi ujue watu wapole wanafikiria nini. Alikuwa ni mtu ambaye ungedhani ungeweza kumtisha kumbe anakuangalia na kukucheka kwa sababu hujamjua.
view