Davis Wafula Nakitare

Born

7th May 1943

Post

P. O. Box 126 Endebess

Email

nakitare@africaonline.co.ke

Telephone

0722489317

Telephone

0735669729

All parliamentary appearances

Entries 321 to 330 of 893.

  • 29 Mar 2023 in Senate: Bi. Spika wa Muda, nadhani nchi nzima inasikiliza mjadala huu na pande zote zina haki kutoa hoja ambazo Wakenya wanaskiliza kwa makini. Ninaelewa fika yale mambo ambayo yanashinikiza ndugu zetu walio kwenye upande wa wachache kwenye Bunge. Ni sawa kwa sababu sheria inawapa uwezo wa kusema yale wanasema. La muhimu ni kuwa kule tunakotoka, watu wanataka kuona Mawaziri wakiwajibika. view
  • 29 Mar 2023 in Senate: Sen. Sifuna umetaja vipengele ambavyo kwako ama kwa wale walio kwenye upande wa wachache, sheria hizi zinawangandamiza ama kuwafinya Maseneta wasijieleze fika mbele ya umma. Ni sawa na tuna nafasi ya kubadilisha. Kile tunasema kama walio upande wa Serikali ni kwamba Mawaziri ambao wamechaguliwa na Mhe. Rais wanapofanya kazi yao hapa Kenya ni lazima wawajibike. Ni vyema wajieleze na kudhihirisha kwamba Kenya ni yetu sisi sote. view
  • 29 Mar 2023 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kwa mfano, juzi tumeona Baraza la Mawaziri. Kwenye vyombo vya habari, kulikuwa na taarifa kwamba kutakuwa na ubinafsishaji wa mashirika ya Serikali zikiwemo hoteli. Hiyo ni sawa lakini kuna Mawaziri ambao tanangoja hapa. Waziri husika anafaa kuja na kutueleza aliuliza nani ruhusa ya kubinafsisha mali ya Serikali kwa sababu sisi ni viongozi ambao tunawaakilisha Wakenya. view
  • 29 Mar 2023 in Senate: Mimi kama Seneta wa Bungoma, hatutakubali kubinafsisha Kiwanda cha Sukari cha Nzoia pasipo kuhusisha wapigakura wa Kaunti ya Bungoma na watu wengine ambao wanatoka pembe mbali mbali za Kenya. Ni lazima Mawaziri waje hapa ili tuwaweke kwa msasa na ikiwezekana tuwatundike juu ya msalaba jinsi Sen. Mungatana alivyosema. Wakenya wana haki ya kupata majibu kutoka kwa Mawaziri. Kuna masuala ya mipaka hapa Kenya. Kumekuwa na shida ya barabara kule Malaba na Busia. Jinsi nilivyosema jana, kazi ya Mawaziri si kupiga picha. Wanafaa kuja kutueleza kwa sababu tunawapa bajeti. Tunafaa kujua kama tunapata haki kama Wakenya ama kazi yao ni kujinufaisha ... view
  • 29 Mar 2023 in Senate: Naunga mkono Kiongozi wa Wengi kwamba Mawaziri wawe wakija. Hata hivyo, jinsi Sen. Sifuna alivyosema, tunafaa kufungua milango na kuzungumza Wakenya wakisikia. Kama ni lugha tuseme na kama ni mifano tutoe kwa sababu wanaporudi kwa Baraza la Mawaziri, wanafaa kwenda kumwambia Mhe. Rais kwamba tumewauliza maswali na wameshindwa kujibu ili awape nafasi ya kwenda kufanya masomo ya ziada nyumbani ili tukiwaita tena watupe majibu tunayotaka. view
  • 29 Mar 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 29 Mar 2023 in Senate: Watu wa Mombasa, tunasikia Bandari iko kwa shida. Ni lazima Waziri aje atueleze ni mikataba gani, ni nani wanahusika na kama tuna haki ama hoja za kuthibisha ya kwamba kuna watu wanaotaka kupora nchi ya Kenya, tuwanase. Sisi ndio wengi katika Seneti. Sioni kitakachotutisha lakini ni lazima tufuate sheria, Mawaziri waje watueleze. Wakenya kule nyumbani wasikilize kwamba tuliuliza kile walichotutuma na majibu tumeypata. view
  • 29 Mar 2023 in Senate: asante Bi. Spika wa Muda, ninashukuru kwa furusa hii na naomba tuendelee na yale tunayopaswa kuendelea nayo. view
  • 29 Mar 2023 in Senate: Bi. Spika wa Muda, ninaunga mkono. view
  • 28 Mar 2023 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Ningependa kuunga mkono Hoja iliyotolewa na Sen. Osotsi. Baadhi ya wanafunzi katika shule za upili, vyuo vikuu na vyuo anuwai, wako nyumbani kwa sababu hawana karo. Serikali za kaunti zimeweka wanafunzi hawa katika mfumo wa kuimarisha masomo yao kwa wale ambao ni wachochole kifedha. Hivi kwamba, serikali ya Kitaifa imekosa kuwachilia pesa kuenda mashinani huku tukizingatia kwamba sisi kama Seneti na Bunge la Kitaifa tulitia sahihi na kupitisha kwamba pesa ziteremuke. Hivi kwamba, ninaunga mkono mapendekezo ya Seneta Osotsi kwamba tuelezwe ni kwa nini kunakucheleweshwa kwa fedha za kuenda kwenye kaunti ilhali tunaona Mawaziri humu Kenya ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus