Davis Wafula Nakitare

Born

7th May 1943

Post

P. O. Box 126 Endebess

Email

nakitare@africaonline.co.ke

Telephone

0722489317

Telephone

0735669729

All parliamentary appearances

Entries 301 to 310 of 893.

  • 24 May 2023 in Senate: ambaye ametoa uongozi na kuapa kwamba atafuata sheria na kanuni za Katiba, kuhakikisha kwamba kila Mkenya ambaye yuko na nafasi ya kazi anawajibika na vilevile anapata kipato kwa jasho lake. vilevile, haya yanadhihirika wakati huu wa Serikali. Kuna wauguzi ambao wanahudumu chini ya mfumo wa Universal Health Care (UHC) na mkataba wao ulikamilika juma lililopita. Mhe. Rais na Serikali yake walikuwa kwa mkutano kule Naivasha. Katika mkutano huo, magavana waliahidi kwamba hawa wachapa kazi, wahudumu wa afya, wataendelea kufanya kazi pasipo bugdha yoyote. Kufikia sasa, wauguzi hawana mbele wala nyuma na hawajui hatima yao iko wapi. Kazi yetu sisi kama ... view
  • 24 May 2023 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii. Waziri ametaja kwamba kupatia Wakenya umeme ni jambo ambalo anashughulikia. Kuna vijana mliowaandika kufanya kazi ya kuunganisha nyaya za umeme ili Wakenya wapate umeme. Mko na malighafi ya kutosha kuhakikisha Wakenya wanapata umeme? Iwapo hawatoshi, ni mbinu zipi ama vigezo vipi ambavyo mnatumia kuhakikisha kwamba Wizara yako inawapa Wakenya wote nafasi ya kupata ajira kutokana na rasilmali tulionayo katika Wizara yako? view
  • 24 May 2023 in Senate: Mr. Deputy Speaker, Sir, I apologize. I have nothing to say. I was to contribute to something else. view
  • 4 May 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Ningependa kuchangia Taarifa ya Sen. Okenyuri kwamba walimu wa nchi wanachekwa na jamii. Ukiangalia jinsi taasisi inayohusika na maswala ya walimu huharakisha na walimu hawapati nafasi kufanya kazi zao za ziada ili kuongeza kipato. Ukiangalia jinsi walimu hawa wamekuwa wakisahihisha mitihani hii na mchakato mzima, inastahili Serikali iwe imetenga fedha za kuwalipa walimu hawa baada ya kazi zao. Baadhi ya walimu hawa wana mikopo kwenye benki na mashirika mengine. Ni jambo la busara Serikali kuwalipa walimu kwa kazi waliyoifanya. Kando na kulipa kwa kusahihisha, ni walimu hao ndio hufunza wanafunzi ambao hubobea na kupata ... view
  • 4 May 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 3 May 2023 in Senate: On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. view
  • 3 May 2023 in Senate: Bw. Naibu wa Spika, ningependa kunukuu kutoka kwa Sheria na Kanuni za Bunge 110 kwamba Seneta anaweza kuhairisha jambo lolote hadi wakati mwingine. Haya ni kwa mapendekezo ya Mwenyekiti ili yale ambayo yanajadiliwa kwa sasa, yaweze kupewa muda zaidi ili mapendekezo ambayo Maseneta wameweza kutoa kwa siku ya leo yaweze kuorodheshwa ama yawekwe kama mchango katika ripoti ya Kamati ya Ugatuzi. Hii ni kwa sababu, hatuwezi tena kuanza kusukuma gurudumu upya ilhali tuko na nafasi kama Seneti kukata kauli mara moja na kuamrisha fedha hizi ziweze kutumika mara moja katika ujenzi wa makao makuu ya Kaunti husika. Kwa hayo, naomba ... view
  • 2 May 2023 in Senate: Bw. Spika, asante kwa nafasi hii. Ninadhani alicholeta Sen. Cherarkey ndani ya Bunge hili, ni kwamba kuna matapeli katika Serikali. Vile vile, kuna nyenzo ama lemba zao katika shirika la ndege ambao wako na mkataba wa kupora na kupunja pesa za umma. Haiwezekani mtu kurejesha matokeo ya kuanguka mtihani ama kipato cha shirika hilo kwenda chini, na Serikali inampigia makofi na kutia sahihi kandarasi mpya. Ni kinaya sana. view
  • 2 May 2023 in Senate: Sijaona Waziri au mtu yeyote katika Serikali, akikashifu Shirika hili kwa matokeo duni jinsi tunavyoona. Juzi tumeona wenzetu Mombasa wakilalamika kwa sababu shirika hili lilifutilia mbali shughuli zao kule Mombasa na kwenda mpaka nchi za ughaibuni. Kwa sababu wameshindwa, sasa wengine hawapaswi kufua dafu katika usafiri wa ndege. Mimi ninaunga Sen. Cherarkey mkono. Iwapo wameshindwa, wafunge shirika hilo kabisa. Milango ifungwe, watu wafukuzwe waende nyumbani na tuanze upya kwa karatasi jipya lisilo na dosari yoyote. Iweje mabilioni yamezwe na walafi kupitia shirika hili, ilhali kuna viwanda vya sukari na kuna wakulima wachochole mashinani ambao hawana pesa? Tutamlilia nani iwapo Serikali ... view
  • 27 Apr 2023 in Senate: Asante sana Bi. Spika wa Muda kwa nafasi hii. Kwanza ni kushukuru Seneta wa Kakamega, Sen. (Dr.) Khalwale, kwa kuleta Hoja hii kwenye Seneti, ili mambo ya kiroho vile vile yaweze kujadiliwa kwa akili na kudhibitiwa kimwili. Katika vyombo vya habari na mashinani tunakotoka, tunaona maajabu na vituko. Kwa mfano, unapata mhudumu wa injili akiwarai wafuasi wake, wainue marinda ama watoe mishipi na kugusagusa sehemu zao za “transformer”, na kuwapa matumaini kwamba watapata uponyaji ama watoto. Kuna wale ambao wanaambiwa watoe mashati na unamuona muhudumu anagusagusa matiti huku akicheka akikejeli akisema, “wewe hauogopi televisheni?” Lazima wananchi wa Kenya wapate haki. ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus