All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 55.

  • 9 Oct 2013 in Senate: , itakuwa ni rahisi watalii kuweza kufika mahali alikozikwa kule Bangale, Malindi. Shughuli kubwa sana za utalii hapa kwetu Kenya, tunaona zimelenga hoteli zilizoko kwenye ufuo wa bahari. Na utaona kwamba kuna shida kutoka Kiwanja cha ndege cha Mombasa hadi mahotelini ilhali ni sehemu ambayo ingechukua hata dakika kumi, lakini siku hizi tunachukua hata masaa sita. Wakati mwingine magari yanakwama ukifika mahali panapoitwa Changamwe ama Kipevu. Kuna msongamano wa magari na wakati mwingine magari yanakwama pale kwa masaa 24; hayaendi na hayarudi, kwa sababu njia inayotoka kwenye uwanja wa ndege kuelekea Nairobi ama kuingia Mombasa, ama kuenda Jomvu, kuna msongamano ... view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Pia ningependa kumpongeza Sen. Karaba kwa Hoja yake nzuri kama hii ambayo inaenda kutufungulia mambo mengi katika nchi yetu ya Kenya. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, kwa siku chache ambazo nimekaa Nairobi, kuna maswala ambayo najiuliza kuhusiana na mambo ya barabara. Barabara kuu ya Thika iko na karibu leni 12 na inaingia katika Jiji letu la Nairobi. Ukishaingia Nairobi utapata leni mbili tu. Kwa hivyo barabara ya leni 12 inaungana na barabara ya leni mbili pekee yake katika Jiji letu. Hiyo inachangia msongamano wa magari katika Jiji letu la Nairobi. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, pia nataka kusisitiza kuwa haya yote tunayoyaongea hapa yamesababishwa na utawala uliopita na wanasiasa ambao matumbo yao mpaka dakika hii sioni kama yameshiba na wala hayatashiba. Hii ni kwa sababu nakumbuka zamani view
  • 9 Oct 2013 in Senate: nyingi zilikuwa zinabebwa kwa magari ya moshi--- view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, hata yeye pia wakati mwingine huwa anachanganya. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, nimechanganya. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, nilikuwa nasema kwamba haya yote tunayoongea hapa kuhusu shida za barabara zimechangiwa sana na Serikali zilizopita na wanasiasa wa hapo awali. Nakumbuka zamani container zilikuwa zikibebwa kwa gari la moshi. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, kuna maneno mengine ambayo siyafahamu. Kwa hivyo, nitaongea Kiingereza na mnisamehe. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, kama mpaka leo container zetu za mizigo zingekuwa zinapelekwa kwa gari la moshi, nafikiri kuwa msongamano wa magari ungekuwa umeisha katika barabara zetu. Wanasiasa ndio walisababisha kuondolewa kwa mizigo katika magari ya moshi na kuanzisha biashara zao za kusafirisha mizigo kwa barabara. Usafiri wa reli ulififia na biashara zao zinaendelea barabarani hadi wakati huu. Watakapokubali kutii sheria za nchi hii na kuunga mkono uvumbuzi wa barabara za reli na mizigo yote kusafirishwa kwa magari ya moshi, huenda tukapunguza msongamano huu ambao tunaongea juu yake hapa. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus