All parliamentary appearances

Entries 41 to 50 of 55.

  • 24 Sep 2013 in Senate: Bi. Spika wa Muda, ningependa kusema kwamba yule ambaye alihusika na kisa cha kigaida cha Twins Tower huko Marekani, mkewe ndiye yuko katika vyombo vya habari; anaitwa Samantha. Yeye ndiye mastermind wa kitendo cha Westgate Mall. Ametoa habari kwa facebook akisema kwamba hivi karibuni ataungana na mumewe. Mumewe alikufa kwa hivyo inamaanisha kwamba anaenda kufa. Kwa hivyo, huyo ni mwanamke amejihami, na vyombo vya habari vimetangaza hivyo. Je, Serikali ya Kenya inajipanga vipi kukabiliana na matamshi ya huyu mwanamke? Ningependa kuiomba Serikali yetu ya Kenya isilaumu Wizara ya Usalamu. Mwanadamu alimshinda Mungu akili. Katika Bustani la Eden Mungu aliwaumba Adamu ... view
  • 24 Sep 2013 in Senate: Bi. Spika wa Muda, narudia tena kusema mwanadamu alimshinda Mungu akili. Hii ndiyo sababu alimfukuza kutoka Bustani la Eden. view
  • 18 Sep 2013 in Senate: Asante, Bi Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Pia ningependa kumpongeza Sen. (Prof.) Lonyangapuo kwa kuleta Hoja nzuri kama hii, hasa kwa mama kama mimi anayetoka pwani. Sen. Lesuuda ametaja jambo fulani ambalo limenigusa moyo sana na ndio nikasimama; kwamba kwa miaka hamsini tumeongea kuhusu maswala ya usalama na mpaka wakati huu bado tunaongea kuhusu mambo hayo hayo. Hii ni wazi kwamba kuna watu ambao wanafaidika na mauaji ya wananchi. Nikigusia kwetu Mombasa, kitu ambacho kinanishangaza ni kwamba utapata vituo vya polisi vipo katika maeneo yasiostahili. Vituo vyote katika Kaunti ya Mombasa vimewekwa kwenye eneo la watu matajiri. Hawa ni ... view
  • 23 Jul 2013 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika,kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Mswada huu ambao umejadiliwa na wenzangu. Bw. Naibu Spika, kwa miaka mingi au tangu tulipopata Uhuru, tuliona vile kiongozi wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya alivyotoa ahadi nyingi sana. Pia, kiongozi wa pili na watatu vile vile walipeana ahadi nyingi. Ahadi zenyewe zilikuwa kama kuambiwa kuwa kutakuwa na upanuzi wa barabara, kurekebishwa kwa reli, ujenzi wa shule na mengi ambayo hayajafanyika hadi wakati huu. Kadri tunavyoendelea, tunazidi kupata mambo yakusikitisha katika kaunti. Inadhihirika wazi upande wa akina mama. Watoto ambao wanazaliwa kabla ya muda unaofaa hawana nafasi ya kuishi ... view
  • 23 Jul 2013 in Senate: (LASDAP) kwa miaka minane na, mara The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 23 Jul 2013 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii. Watu hawafahamu mambo ya ufugaji kwa sababu ya magonjwa yanayowakumba wanyama. Magonjwa haya yamewafanya watu wetu wasiwe na mifugo kama vile watu wa Kaunti ya Samburu na kwingineko. Sisi sote hapa mtakubaliana nami kwamba hakuna chakula kinachofurahisha Wakenya kuliko nyama. Nadhani wengi wetu saa za mchana walikula vipande vya nyama. Hata tukitoka hapa kwenda katika nyumba zetu, pia tutakula nyama. Hii ni Hoja ambayo kila mmoja ataifurahia na sote tunafaa kuiunga mkono. Tupende tusipende, katika harusi ama matanga, tunachinja ng’ombe au mbuzi. Tunafaa kujiuliza wanyama hawa hufugwa wapi na ni vipi tutaendeleza ... view
  • 11 Jul 2013 in Senate: Asante sana, Bi Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Kwanza, ningependa kumpongeza Sen. Elachi kwa kuleta Hoja huu. Leo nina hakika kwamba kama kuna vijana wanaoangalia runinga, wataona kwamba kwa mara ya kwanza, Seneti imeweza kuongea masuala yanayohusiana na vijana. Ninampongeza Sen. Elachi. Hoja hii inalenga watoto maskini kule mashinani na ikiwa itapitishwa, ninaamini kwamba suala la MRC litatatuliwa. Mara nyingi kumekuwa na recruitment ya wanajeshi na vijana wetu wamekosa kuchukuliwa kwa sababu kila kitu kilikuwa kikifanyika huku juu na sio mashinani. Kama kutaanzishwa mambo kama haya kwenye kaunti, basi huenda vijana wetu watajiona wamekumbukwa na watapata kazi ya kufanya. ... view
  • 11 Jul 2013 in Senate: Asante sana. Mama yangu hakuwa na cheti cha kumiliki ardhi ambacho pengine angepeana kwa benki na akapewa mkopo. Pengine ningesoma zaidi na nikawa kama wenzangu. Kwa hivyo, huu ni mjadala mzuri ambao kama Maseneta wengine wangekuwa hapa, leo kungekuwa na changamoto nzuri sana ya kuweza kufafanua Hoja hii zaidi. Ningetaka kusema kwamba Hoja hii itakapozaa Mswada na kuwa sheria ili NYS iweze kupelekwa kwenye kaunti, sheria zisiwe kama zile za jeshi letu wakati wanapofanya recruitment . Ningependa wazingatie umri. Mara nyingi nyingi huwa wameweka kiwango cha umri na watoto wa kwetu wa Kimijikenda wanasoma kuchelewa. Wanapofika sekondari hao huwa hata ... view
  • 9 Jul 2013 in Senate: Asante Sana, Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii. Ninaifurahia Hoja hii sana. Hata hivyo, mchango wangu utakuwa ni mfupi sana kuhusiana na Pwani ninakotoka. Swala la kilimo ni nyeti sana katika Mkoa wa Pwani. Jambo hili limekuwa likihuzunisha na kukera watu wetu kwa miaka mingi. Ardhi ya Pwani ina rutuba nyingi sana. Kuna watu wanaoamini kuwa Wapwani ni wavivu na si wakulima. Ningependa kusema kwamba wapwani ni wakulima hodari sana. Lakini shida yetu ni kuwa ardhi kubwa yetu imemilikiwa na absentee landlords . Jambo hili limefanya sisi kutotilia maanani shughuli za kilimo kwa sababu hatuna mashamba. Ningependa Serikali yetu ihakikishe ... view
  • 9 Jul 2013 in Senate: ambao hatuwajui wanakoishi. Ninaiomba Serikali iwape watu wa Pwani mashamba. . Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus