All parliamentary appearances

Entries 31 to 40 of 55.

  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, ningependa pia kusisitiza hapa kwamba hizi ambulances ambazo tunazizungumzia zina hatari yake. Kuna ambulances zingine ambazo hazibebi wagonjwa. Kwa mfano, kwetu Mombasa tulikuja kugundua ya kwamba magari mengi yenye ving’ora vya kuashiria kuwa wagonjwa wanakimbizwa hospitalini huwa yamebeba madawa ya kulevya. Kwa hivyo, wakati tutakapopanua barabara hizi ili kutenga barabara za ambulance na fire brigade, Serikali inafaa kuwa macho, kwa sababu nyingi huwa hazibebi wagonjwa bali ni kusafirisha silaha na mihadarati. Kwa hivyo, pia kuna hatari yake. Tunaweza kupanua barabara kisha tukawapanulia majemedari wasioshiba, ambao wanatuharibia nchi yetu. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika ninatoa onyo. Huenda ambulances hizi badala ya kusafirisha wagonjwa--- view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Nasema kwamba kuna wakati niliona na kusikia kwa runinga kwamba ambulances zinabeba madawa ya kulevya. Hili ni jambo ambalo lilionekana Kenya nzima. Kama mwenzangu haangalii runinga itabadi aanze. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, nasema kitu cha kweli ambacho nimeshuhudia katika runinga. Kuna wakati pia nilisoma kwa gazeti. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Yes, Mr. Deputy Speaker, Sir. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, naomba kuwa nikiongea Kiswahili pia nyinyi mniongeleshe kwa Kiswahili. Naomba urudie tafadhali. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, kwa sababu mmeniomba nitoe thibitisho, naomba kuondoa statement yangu kwa sababu ni kitu nilichokiona likini sina ushahidi. Lakini ninataka kuirekebisha na kusema kwamba ningependa kutahadharisha na kutoa onyo kwamba huenda ambulance na magari ya kuzima moto yakatumiwa kwenye biashara isiofaa, kwa sababu magari hayo hayasimamishwi. view
  • 9 Oct 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, kwa sababu mmenichanganya kichwa sitaendelea. Naunga mkono Hoja hii. view
  • 24 Sep 2013 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Kwanza ningependa, kwa niaba ya akina mama wote wa Pwani, wazee wa Kaya wa Kimijikenda na akina mama wote ulimwenguni ambao wamepitia uchungu kuzaa, kulaani kitendo hiki cha ugaidi kilichotokea katika Westgate Mall. Hawa ambao tunawaita Al Qaeda ni watu waliopitia kutoka kwa matumbo yetu sisi wanawake. Pia ningetuma risala zangu za rambirambi kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Kenya wakati huu wa msiba katika taifa letu la Kenya na kwa familia zote ambazo zilipatikana na mkasa huu na marafiki. Ningependa kuwapa moyo kutoka kifungu cha Biblia, kitabu cha Warumi, 8:36. Kifungu ... view
  • 24 Sep 2013 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus