All parliamentary appearances

Entries 41 to 50 of 112.

  • 7 Oct 2015 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Niliumwa na kitu, nikajikuna halafu watu wakaona kama ni nguo ninatoa. Sio nguo nilikua ninatoa. view
  • 7 Oct 2015 in National Assembly: Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda, ninaunga mkono. Wakati mwingi--- view
  • 7 Oct 2015 in National Assembly: Tafadhali tuachane na mambo ya nguo. Mara nyingi tunaongea mambo ya vijana lakini ikifika wakati wa kufaidika, wazee wanafaidika na vijana wanakosa. view
  • 7 Oct 2015 in National Assembly: Asante. Kama alivyosema Mheshimiwa Nakara, inafaa tuwachunge vijana. Isiwe vijana wanashughulikiwa na ikifika wakati wa kufaidika, wazee wanapata na vijana wanakosa. Kwa hivyo tusikose mwelekeo. Vijana pekee ndio wanapaswa kufaidika. Asante sana. view
  • 30 Jul 2015 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Nami pia ninataka kuchangia. Ninamshukuru Mheshimiwa kwa kuleta Ripoti hii Bungeni. Kama vile Mheshimiwa mwenzangu amesema, tumezoea kuangalia kitu kwa njia moja na sio kwa njia nyingine. Tunaangalia nani tutamchafulia jina na nani ataanguka katika njia ile ambayo anapitia lakini hatuangalii tumefaidika namna gani. Wakati mambo haya yalitokea hapa Bungeni na hata nchini mwetu, hata waheshimiwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 30 Jul 2015 in National Assembly: wenzangu wengi waliharibiwa jina. Katika maeneo yao ya uwakilishi Bungeni wanaitwa watu wa massage . Jambo hili ni mbaya kwani Mheshimiwa akitoka hapa aende ng’ambo kama ametumwa na Bunge, haendi kusimamia mambo yake bali anaenda kuwawakilisha wananchi wa Kenya na haswa anawakilisha eneo lake la uwakilishi Bungeni. Kwa hivyo hatutaki kuwafinyilia sana wale ambao waliongea na wakachafua sana majina ya wengine. Tungesema waombe msamaha kwa kuleta kibonzo ambacho kilikuwa kimechorwa watu ambao ni marafiki zetu. Naibu wa Rais amekuwa akifanya kazi nzuri. Wakati unafanya kazi nzuri, hukosi watu ambao watapigana na vile unasema na kufanya. Ukweli ni kwamba Naibu wa ... view
  • 10 Jun 2015 in National Assembly: Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Nilikua nafikiri sionekani kwa maana niko mbali. Kumbe niko karibu sana. Nataka kuunga mkono Mswada huu. Ni vizuri sana kufikiria mambo ya wafungwa. Wengine wako katika nchi za nje na wengine wako katika nchi yetu. Ni vizuri mtu akiwa na shida, awe karibu na nyumbani. Nataka kuunga mkono. Mtu akipatikana na hatia akiwa katika nchi za nje, ni vizuri arudishwe nyumbani angalau atembelewe na familia yake. Hii ni kwa sababu hapa Kenya, wengi wanatembelewa. Ni vizuri kujua ya kwamba hata mtu akiwa na makosa, anawezwa kurekebishwa. The electronic version of ... view
  • 10 Jun 2015 in National Assembly: Wale ambao wako nje waje hapa ili waweze kuhukumiwa wakiwa karibu. Ukiwa nje haujihisi ya kwamba unataka kukaa katika nchi hiyo tena. Unataka kurudi nyumbani. Kwa hivyo, yangu ni kuunga mkono Mswada huu ili tuweze kuwasaidia watu wetu ambao wako nje. Hata wakirudi, Mhe. mwenzangu amesema ya kwamba mahali pa kulala katika magereza ya huku kwetu yako katika hali mbaya. Lazima magereza yetu yawe katika hali nzuri ili kuwafaa wale ambao wanaenda huko. Pia, magereza yanaweza kuwa katika hali nzuri lakini ile tabia wanaofanyiwa huko ni mbaya zaidi. Kwa hivyo, ni lazima tuangalie pande zote ili wakiingia huko, wakae kwa ... view
  • 1 Apr 2015 in National Assembly: Ahsante, mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia mjadala ulioko mbele yetu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 1 Apr 2015 in National Assembly: Kwanza kabisa, ni vizuri kila mtu ambaye anaongea mbele ya Bunge hili ajue kwamba heshima inahitajika. Tukija hapa ni lazima tukumbuke kwamba Rais ambaye tunaongea kumhusu amechaguliwa na nchi nzima ya Jamhuri ya Kenya. Hatupaswi kumwambia vile anavyostahili kufanya. Kwa mfano, kusema kwamba Rais anafanya hivi kwa sababu kuna mgeni anakuja ni kumkosea heshima. Samahani kwa sababu naona Mbunge ambaye amesema hivyo ameondoka. Hatuwezi kusema kwamba katika nchi ya Kenya tutakuwa tukifanya kazi kwa sababu mtu fulani anakuja nchini. Kila mtu alifurahia mambo yaliyoendelea siku hiyo. Sisi tunasema kwamba hatuna shaka na Rais kuhusu yale aliyotuambia hapa Bungeni. Tuko na ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus