18 Mar 2015 in National Assembly:
Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda. Kwanza, nashukuru kwa sababu, mimi ni mama wa kwanza kuongea katika Bunge leo. Nimesimama kuunga mkono hii Hoja. Kuna mambo mengi ambayo yamezungumuzwa. Kabla ya hayo, ningependa kusema ya kwamba, nimetumwa na watu wa Kaunti ya Ruiru. Wanasema tuendelee kuombea Bunge letu la Kumi na Moja ndiyo tusiweze kuchafuliwa na mambo yanayopita ya kamati. Mimi ni mmoja wa wahubiri ambao bado hawajateuliwa. Ningependa kuchukua jukumu la kuombea Bunge hili. Tuendelee kuomba kwa sababu uchafu ukiingia katika hii nyumba, hata ikiwa huna uchafu, utakushika. Nasema hivyo kwa sababu mimi ni mhubiri. Tukikosa kujua ni shule ...
view
18 Mar 2015 in National Assembly:
ikifanya vibaya kwenye mitihani hakuna mtu atajua. Kuna shule ambazo hazina madarasa na mambo mengi ya kufaulisha shule. Tunayo hazina ya CDF. Sisi hapa tunaruhusiwa kusaidia shule kwa kutumia pesa za CDF. Kwa hivyo wale ambao wana shule ambazo hazina vifaa katika maeneo yao wanaweza kutumia pesa ya CDF. Kuna shule ambazo zinafanya vizuri lakini siyo lazima kila mtu aende kusomea huko. Muhimu ni kwamba tujue ni mbinu gani shule hizo zinatumia kupita mitihani. Tukikosa kufanya hivyo hali ya masomo itarudi chini. Wale wanaotia bidii watasikia vibaya kwa sababu ni vizuri kujulikana kuwa umefanya vizuri. Siku ile ulishinda uchaguzi, kama ...
view
4 Mar 2015 in National Assembly:
On a point of order, hon. Temporary Deputy Speaker.
view
4 Mar 2015 in National Assembly:
Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Sijui ni kwa nini Mheshimiwa Mbadi anaona ni kama sina Hoja ya Nidhamu.
view
4 Mar 2015 in National Assembly:
Lakini nakuomba kwa heshima Mheshimiwa Mwenyekiti Mbadi ya kwamba sisi hatutaki kujua zaidi vile uenyekiti wako unaendelea. Tunataka kujua yale tunaongea siku ya leo. Tafadhali mambo yako na Mheshimiwa Ken Obura na chama yasijadiliwe hapa bali kwa chama. Ahsante.
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niongee kuhusu Hoja hii ambayo ni muhimu sana ambayo ni ya kuwatetea wananchi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Feb 2015 in National Assembly:
Tunapoongea kuhusu mambo ya wazee ambao walipigania Uhuru wetu, inaonyesha kuwa kuna mambo ambayo yanafanyika katika nchi hii yetu ya Kenya. Kuna watu muhimu sana lakini mara kwa mara, wanasahaulika. Nimetoka katika Kaunti ya Kiambu lakini sina uhakika kwamba watu wote ambao walipigania Uhuru walipata fidia. Kwa sababu hapa hatugombani, ni ukweli kuwa kuna watu wengi ambao walipigania Uhuru, lakini ni wangapi ambao walipeleka kesi kortini na wakasaidika na ile fidia kidogo ambayo ilitolewa? Kwa hivyo, tunafaa kuungana kama Wakenya bila kusema ni kabila fulani ama nyingine ambayo ilipata hiyo fidia kidogo ambayo ilipatikana. La muhimu zaidi ni kuwa hatutaki ...
view
10 Feb 2015 in National Assembly:
Thank you, hon. Speaker for giving me this opportunity to just send my condolences to the family of the late hon. Muchai, who was my colleague in Kiambu County. My worry is: What is happening in Kiambu Country surely? This is the second time we are losing an hon. Member of Parliament. The other day we lost an hon. Member, the late hon. Joseph Ngugi and now we have lost hon. Muchai. I do not want to say that maybe I am the next because I am not threatened, but I feel that maybe we should pray for Kiambu County. ...
view
11 Dec 2014 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Spika kwa kunipa hii nafasi ambayo nimengojea sana. Kwanza, ningetaka kushukuru sana kwa mwaka ambao tumekuwa nao. Nataka kukushukuru Mhe. Spika kwa sababu umekuwa na sisi na umetuelekeza kwa njia nzuri. Nataka tena kumshukuru Katibu wa chama cha ODM ambaye alichaguliwa juzi. Ashikane na Serikali ndio tuweze kulisadia na kulijenga taifa hili la Kenya. Hata Mwenyekiti naye namshukuru sana. Mhe. Spika, kuna mambo mawili au matatu ya muhimu ambayo ningependa kuyasema. Mimi niko katika Kamati ya CDF na tumejaribu sana. Wabunge ambao wako katika maeneo yao ya bunge siku hizi hawateti sana kwa sababu tumejaribu sana. Mimi ...
view
11 Nov 2014 in National Assembly:
Asante sana mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Mswada huu. Mambo ambayo yako mbele yetu ni muhimu sana kwa kila binadamu. Kama tunavyojua kwa kila mtu, maji yakitajwa anahisi kwamba ni kitu ambacho anahitaji. Tukiendelea kuangalia mambo kuhusu maji, ninajua kila mmoja katika eneo la uwakilishi Bungeni la Ruiru anaangalia aone ni kitu gani nitasema kuhusu maji. Lakini shida ya maji iko katika Kenya nzima. Ningependa kuongea kidogo kuhusu akina mama ambao wanasumbuka zaidi na jambo hili la maji. Hata kama tutakuwa tukiyashughulikia mambo haya katika kaunti, ninahuzunika zaidi ni kikumbuka kwamba ukifika katika maeneo ya ...
view