All parliamentary appearances

Entries 61 to 70 of 112.

  • 11 Nov 2014 in National Assembly: Pia, tuangalie wakati tunapanga mipango hiyo, isitumie pesa nyingi hata watu wetu wakakosa maji. Sipingi Kampuni ya maji ya Nairobi, lakini nauliza kazi yao katika eneo Bunge la Ruiru ni ipi? Watu wametaabika, na kubeba maji machafu. Watu wengine wameenda kwa mashimo ya mijengo kuchota maji kwa sababu wana shida. Tafadhali, nikiunga mkono Mswada huu, nawaomba washughulikie suala hilo na wajue kwamba mwananchi wa kawaida analia usiku na mchana kwa sababu ya maji. Akina mama wameumia na migongo yao inauma kwa sababu ya kubeba maji. Tafadhali tuongee hapa Bungeni na pia tufikishe maji pale mashinani. Asante mhe. Naibu Spika wa ... view
  • 20 Aug 2014 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Kitu ambacho ni muhimu katika nchi hii ni usalama. Wakati mambo ya usalama yanachukuliwa kama mzaha, kila Mkenya anaona kwamba mambo hayaendi vizuri. Nilisikia mhe. mmoja akisema kwamba wakati mwingine unaitana na unaambiwa gari la polisi halina mafuta. Katika mwezi uliopita, kuna wakati niliuliza Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na Usalama nchini kwamba--- Wakati mwingine tunasema tuna magari mengi sana yaliyopeanwa katika kila kituo cha polisi. Lakini ninataka kuuliza jambo moja; nilimwuliza OCPD kama hayo magari yamepeanwa kama maua ama ni ya kufanya kazi. Kama magari ni ya kufanya kazi, kwa ... view
  • 20 Aug 2014 in National Assembly: Yes. view
  • 20 Aug 2014 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika, nilikuwa nimeguzwa sana kwa sababu mhe. Mbunge amesema anapoitisha gari anaambiwa hakuna mafuta. Kwa hivyo, tuangalie hilo na tena kuweka maafisa wa usalama ndio waweze kumsaidia; hili pia lifanyike katika maeneo mengine ambapo watu wanalia kama yeye. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 30 Jul 2014 in National Assembly: Thank you, hon. Deputy Speaker. I am also concerned because most of the time we talk about it and we think it is a very good thing. I am sorry to say that I am a victim. If a Member of Parliament can be a victim--- One time I had a patient and I had to take all the time to wait for the NHIF to update my card that is paid for by this Parliament. After that, I was made to pay cash for the services. If I can pay cash, what about the person who has no money ... view
  • 30 Jul 2014 in National Assembly: Thank you, hon. Deputy Speaker. I just wanted the Chair to note that. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Ahsante, mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Ninataka, kwanza, kumshukuru mhe. Millie sana kwa kuleta huu Mswada hapa. Sisi kama viongozi ambao tumechaguliwa kuja katika Bunge hili, kazi yetu ni kuwakilisha wale ambao hawawezi kufika hapa. Tunajua wakati mwingi kuna watu ambao wanateseka. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, Waheshimiwa ambao wako nyuma yangu wana mkutano mwingine. Ninakuomba uwakanye. Bi. Naibu Spika wa Muda, kuna watu tunaowawakilisha ambao wanateseka. Shida iliyoko ni kwamba hawana nafasi ya kujitetea; hawajui pa kuelekea ili kupata usaidizi. Ningependa kusema hivi: Ikiwa wewe ama mimi tutanajisiwa hakuna mtu atajua katika nchi nzima kwa sababu sisi ni wabunge. Kuna wengi ambao wamepata shida lakini wamenyamaza kwa sababu hawajui wataambia nani. Kuna visa vingi vya mama na watoto wake wasichana kunajisiwa na kuporwa mali. Hawa ni watu hawana watu wa kuwafariji na kwa hivyo wanasumbuka. Tunashukuru sana kwa ajili ya huu ... view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Tusiwachukulie polisi kana kwamba si wanadamu. Kuna visa ambapo polisi wanajeruhiwa ama wanauwa wakiwa kazini. Huu Mswada unagusia kila Mkenya. Sisemi kwamba polisi wasifanye kazi yao, lakini nao wachukuliwe kama Wakenya wanaohitaji kufanyiwa haki. Ukitembea kortini utaona waathiriwa ambao hawana watu wa kuwatambua. Utapata kwamba hawana watu wa kuwatetea na hawajui haki zao. Huwa hawana namna ya kuendelea. Tutapitisha huu mswada ndiposa tusimamie watu wetu ambao wamefinyika humu nchini. Ningependa kuwaambia watu wa Ruiru constituency, “hi”, na ninawapenda. Godbless. view
  • 2 Jul 2014 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, kama ingekuwa wakati wa siasa ningesema kwamba kuna mtu amenikanyangia. Lakini nataka kuongea kuhusu barabara ambayo imetoka Ruiru na kupitia maeneo matatu ya uwakilishi Bunge. Barabara hiyo imetuletea aibu sana sisi Wabunge watatu wa Kaunti ya Kiambu. Hii ni kwa sababu kila wakati ndizi hupandwa katika barabara hiyo kana kwamba ni shamba. Ninashukuru kwa Kshs5 milioni ambazo zimetolewa. Walakini hii ni madharau.Tunaomba barabara hiyo ambayo inatoka Ruiru hadi Githunguri na inaguza eneo la Mburu Kahangara iweze kupewa pesa yakutosha ili iweze kujengwa vizuri na watu wetu wafurahie. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus