Isaac Maigua Mwaura

Parties & Coalitions

Born

1982

Email

mwaura.isa@gmail.com

Web

www.isaacmwaura.com/

Telephone

0721864949

Telephone

0733864949

Link

@MwauraIsaac1 on Twitter

All parliamentary appearances

Entries 1651 to 1660 of 1711.

  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Kuwapatia vijana nafasi ilikuwa ni njia moja ya kuwahusisha katika siasa lakini wakaonekana kama watu mboga uongozini. Lakini siyo hivyo. Hii halmashauri ya Kitaifa ya Vijana ni kama ile Maendeleo ya Wanawake. Inawapa vijana wasia mwafaka kujionyesha kwamba wao wana demokrasia na wanaweza kuwa na viongozi ambao watazungumza kwa niaba yao kwa sababu wamechaguliwa na vijana kama wao. Bw. Spika, kipengele cha nne cha sheria ambayo imetengeneza hili baraza imesema kinaga ubaga yale mambo ambayo litafanya. Kwa mfano, inasema kwamba baraza hili litakuwa likihusika katika kushirikisha miradi na mikakati ya kitaifa kwa vijana. Hili ni jambo muhimu kwa sababu watu ... view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Pia, tumekuwa na sera ya kitaifa kuhusu vijana ama ukipenda kwa kimombo “the National Youth Policy”. Lakini hii sera, ambayo pia mimi nilikuwa mmoja wa waliohusika kuitengeneza, hatujaona ikitekelezwa na Serikali. Kwa hivyo, baraza hili lina jukumu la kueneza na kutangaza yale mapendekezo, maafikio ama ile ndoto ambayo iko katika hii sera ili tuweze kuinua kiwango cha uchumi na uwakilishaji wa vijana katika mambo ya kitaifa. Kwa hivyo, ni jambo muhimu sana kuhakikisha kwamba hili barasa limetengewa hela ndio liweze kufanya kazi yake. Baraza la Vijana la Kitaifa pia limepatiwa jukumu la kutafuta rasilimali na fedha ili kuipatia nguvu miradi ... view

  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Kama hili baraza litapatiwa nguvu, litaongeza sauti ya vijana katika mashirika ya maamuzi ya umma. Pia, itakuwa sauti nzito ambayo itasikika kuhakikisha kwamba asilimia sabini na tano ya wakenya ambao wako chini ya miaka 35 wanahusishwa katika shughuli za nchi hii. Ni muhimu kufanya vile kwa sababu kama vile takwimu zinaonyesha, kufikia mwaka wa 2017, kutakuwa na vijana zaidi ya milioni 24 ambao watakuwa chini ya miaka 35. Kama hatutaangazia sana maswala ya vijana, basi ni kama tutakuwa tumekalia bomu la muda. Ningependa kuhimiza Serikali ya Jubilee ambayo imechaguliwa kwa kusema sana kuhusu vijana na akina mama, kwamba inafaa kuchukua ... view

  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Asante sana mhe. Spika. Ningependa kuunga mkono Hoja hii ilioko mbele ya Bunge hili letu, kama kijana wa miaka 31 ambaye anajivunia kuwa kijana ambaye anahisi kudhulumiwa. Tumefanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba kuna halmashauri ya kitaifa kuhusu vijana, ambayo tulianza kuitetea tangu mwaka wa 2004 na ambayo ilipitishwa miaka minane baadaye; na haijawahi kupatiwa pesa na Serikali tukufu. Mhe. Spika, hili ni jambo la kushangaza kwa sababu ni jana tu Bunge hili liliweza kupitisha makadirio ya Serikali ya mwaka wa 2013/2014. Na hii halmashauri ni mojawapo ya taasisi za Serikali. Mhe. Spika, vijana walirauka na kupigania nafasi za uongozi kutoka ... view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Kuwapatia vijana nafasi ilikuwa ni njia moja ya kuwahusisha katika siasa lakini wakaonekana kama watu mboga uongozini. Lakini siyo hivyo. Hii halmashauri ya Kitaifa ya Vijana ni kama ile Maendeleo ya Wanawake. Inawapa vijana wasia mwafaka kujionyesha kwamba wao wana demokrasia na wanaweza kuwa na viongozi ambao watazungumza kwa niaba yao kwa sababu wamechaguliwa na vijana kama wao. Bw. Spika, kipengele cha nne cha sheria ambayo imetengeneza hili baraza imesema kinaga ubaga yale mambo ambayo litafanya. Kwa mfano, inasema kwamba baraza hili litakuwa likihusika katika kushirikisha miradi na mikakati ya kitaifa kwa vijana. Hili ni jambo muhimu kwa sababu watu ... view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Ahsante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuiunga mkono Hoja hii kuhusu wafanyikazi wa umma katika sekta ya afya, nikitathmini ya kwamba Wakenya wanaongezeka kwa idadi kubwa sana. Ripoti ya census ya mwaka wa 2009 inaonyesha kwamba Wakenya wanaongezeka kwa kiasi cha milioni moja kila mwaka. Hii inamaanisha kwamba vifaa vilivyoko kwenye mahospitali yetu haviwezi kukidhi mahitaji ya matibabu ya Wakenya. Kulikuwa na tetezi kwamba ni vizuri wauguzi wetu waende kufanya kazi katika nchi za nje kwa sababu watakuwa wanachangia kuleta fedha za kigeni na kuzisaidia jamii zao. Ningependa kusema kwamba jambo la muhimu ni kuhakikisha kwamba Wakenya wako ... view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia vizuri ni kwa nini nchi za kigeni zinahitaji watabibu wetu na sisi wenyewe hatuwezi kuwaajiri? Ingekuwa ni vyema kama wale ambao tunasema waende kufanya kazi kule nje wangekuwa zaidi ya wale ambao tunaweza kufundisha hapa. Lakini kuwa na mikakati ambayo inaonyesha kwamba vijana wetu wanakwenda shuleni, wanapata masomo ya afya na uuguzi lakini hawawezi kupata kazi, basi ni kuonyesha kwamba tunatumia pesa za umma vibaya. Kwa hivyo, ni muhimu sana kuhakikisha kwamba kuna utangamano kati ya zile hospitali na zahanati tunatengeneza kutumia zile pesa za umma kama vile CDF na watu watakaoweza kuwahudumia Wakenya ... view
  • 12 Jun 2013 in National Assembly: Ukiangalia, kwa mfano, ugonjwa wa saratani, umeongezeka kama vile miaka inavyokwenda ilihali, ugonjwa huo unaweza kutibiwa ikiwa kiwango chake hakijaweza kukidhiri. Kwa hivyo, kama hizo zahanati na hospitali zitakuwa na watabibu na wauguzi, itakuwa ni jambo la muhimu kuhakikisha kwamba magonjwa hayo yametibiwa kwa kiwango cha chini. Utakuta kwamba tangu tuanze kuzungumzia maswala ya afya katika Bunge hili la Kumi na Moja, kumekuwa na Miswada minne iliyowasilishwa na Wabunge tofauti kuhusu afya. Tulikuwa na Mswada wa hela za NHIF, wa Emergency Treatment, wa saratani na sasa huu. Hii inamaanisha kwamba sisi kama nchi tunafaa kufikiria kwa undani na kina na ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus