She has established the Janet Nangabo Foundation, a community based organization specifically created to provide solutions for problems of the Trans Nzoia people.
1 Apr 2015 in National Assembly:
Pili, nataka kumshukuru Rais kwa kuongea juu ya umeme. Ni kweli tusipokuwa na umeme katika nchi yetu ya Kenya utaona kwamba hakutakuwa na kazi nyingi zakufanya katika sehemu zetu. Wengi wa watu wa jua kali, akina mama wa kuuza mboga ama vijana wale wanaendesha piki piki--- Kwa kweli ni lazima tuwe na umeme ndiposa mambo ya usalama yaende sambamba.
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
Tatu, ningependa kumshukuru Rais kwa sababu aliongea kuhusu matibabu na kuwa na kadi za NHIF, ndiposa jamii zinazotoka katika maisha ya umaskini wapate matibabu katika hospitali zinazostahili.
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
Pia namshukuru Rais kwa sababu ya hazina ya Uwezo Fund. Imewafikia akina mama kule mashinani na pia vijana wetu; hatukuwa na hizi pesa na vijana na akina mama wetu walikuwa wakiangamia. Lakini sasa ninafurahi sana kwa sababu akina mama wanaweza kufanya biashara zao, vijana wetu si kwamba ni piki piki pekee ama baiskeli peke yake, ila wana njia nyingine za kujiendeleza kimaisha.
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
Ningependa pia kumshukuru Rais kwa sababu ya pesa za wazee. Zile pesa zimeweza kuwafikia wazee kule mashinani. Kuna pesa za watoto mayatima. Hizi pesa pia zimeweza kuwafikia watoto mayatima katika sehemu tunakotoka.
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
Kile pia ningependa Rais asisitize ni mambo ya mashamba. Kweli tumekuwa na ufisadi kuhusu mambo ya mashamba kwa sababu kuna matapeli wanaojaribu kupata vyeti, ama title deeds, vya mashamba yasiyo yao. Kama hivi juzi nilikuwa Cherangany. Kuna shule moja iliyokuwa imenyakuliwa shamba lake. Halikuwa jambo zuri kwa sababu unyakuzi wa mashamba umezidi sana katika nchi yetu ya Kenya. Ningependa Rais aorodheshe majina ya wafisadi ama watu wanaojaribu kunyakua mashamba yasiyo yao. Unaona kwamba shule nyingi hazijapata title deeds, lakini ninataka kumshukuru Rais kwa sababu amesema kwamba ifikapo mwaka 2017, title deeds milioni tatu ziwe zimetolewa kwa watu wanaostahili. Ningependa hiyo ...
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
Nikimalizia, ningesema kwamba mambo ya ufisadi katika nchi yetu ya Kenya--- Ni lazima sisi Wabunge tumuunge Rais mkono ili tuhakikishe kwamba mambo ya ufisadi yanaisha. Katika hii orodha ambayo imeletwa tunaka kuona uchunguzi utakavyofanyika ndiposa tujue huyu amefanya nini na yule amefanya nini. Ninaomba kwamba sisi kama viongozi tuunge mkono Rais na naibu wake ili tuhakikishe kwamba tunapata maendeleo katika miaka mitano tuliyochaguliwa kuhudumu.
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
Ahsante sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
29 Oct 2014 in National Assembly:
Hon. Speaker, I beg to give notice of the following Motion:- THAT, aware that an increasing number of women in Kenya are moving away from traditional work burdens and entering new forms of self-and-paid employment in the private and public sectors; noting that these activities require women to work for long hours and far from home, leaving their children with inadequate care; further aware that to date no single employer in Kenya has child care services for its women employees at the place of work; deeply concerned that there is no regulatory system for child handlers and existing child care ...
view
29 Oct 2014 in National Assembly:
child care workers and ensure that passage of bad behaviour to young children is curbed.
view
27 Aug 2014 in National Assembly:
Hon. Speaker, I also want to support the Petition which was presented by our colleague here. It is true that the project, or that house, has been there for the last 15 years and it was not in use. As hon. Pukose has said, that house was purchased in March at Kshs46 million. After two months, he sold it at Kshs185 million. We want to see that transparency and accountability are observed in Trans Nzoia.
view