John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 111 to 120 of 2259.

  • 14 Aug 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika. Mimi ninaunga mkono Seneti yote ijumuishwe katika kuichanganua yale mambo yatakayoletwa katika Seneti. Hii ni ndiposa Wakenya waweze kuona mambo yamewekwa paruwaja na yaweze kuangaziwa vizuri kama vile tulivyofanya katika zile impeachments zingine. view
  • 14 Aug 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwa sababu nimekuwa katika Seneti hii, ni vizuri Maseneta wote wakijumuishwa katika hili jambo kwa sababu ikipelekwa katika Kamati, maoni watakayo yaona haitaletwa hapa katika Bunge na wale watu tutakao wachagua. Bw. Spika, sina shida yoyote na wale Maseneta waliochaguliwa kwa sababu wanaujuzi na uzoefu na wanaweza kuyaangazia yale mambo. Hata hivyo, jambo hili likifanywa katika Seneti, maneno yote yatawekwa wazi ili watu waweze kuona na itakuwa ni vizuri zaidi. Asante. view
  • 8 Aug 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Mswahili anasema kipitacho rohoni kinapaswa kuonekana usoni. Seneta Beth Syengo ameongea kuhusu Rais wa Jamhuri ya Kenya na yeye anaonyesha kwa vitendo. Hii ni kwa sababu nikimwangalia, ninaona amevalia kofia ya chama kinachoongoza. Hata mkoba wake--- view
  • 8 Aug 2024 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I am still contributing. view
  • 8 Aug 2024 in Senate: The good lady talked about what the President is doing. Therefore, I am in order to say what I was saying. view
  • 8 Aug 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika. Ninaunga mkono ile Taarifa iliyoletwa na Seneta kutoka Meru, Sen. Kathuri. Kuna mikataba kati ya gatuzi zetu na madaktari kuhusu vile ambavyo matibabu yatakua yakielekezwa. Mikataba hii ni kama haina faida ya kukamilishwa ama wale wanaandika hii mikataba hawana haja ya kukamilisha. Ndio maana kila saa unapata kuna migomo katika hospitali zetu. Wananchi wa gatuzi zetu wanafanya vile inapaswa. Unapata mtu amelipia bima ya NHIF, lakini akienda hospitali, hakuna dawa. Nikiunga Taarifa hiyo, saa zingine inafika wakati ninakisia vile wananchi wengi wa Kenya wanavyosema, kwamba ni vizuri afya ama matibabu irudishwe kwa Serikali Kuu. Gatuzi zimezembea kwa ... view
  • 8 Aug 2024 in Senate: Kuna Taarifa iliyoletwa na Sen. Asige. Nilitazama mashindano kule Paris Wakenya wakikimbia. Niliona msichana anayeitwa Yavi na aliyetoka Makueni. Nikiangalia mitandaoni, niliona Yavi akisema ya kwamba kisa na maana cha yeye kutowakilisha nchi yetu ni kuwa aliitishwa zaidi ya Kshs200,000. Hawezi pata pesa kama hizi. Lakini anaendelea kusema hata baada ya ufisadi ulio katika Wizara, alijikakamua na akaingia katika nchi ile. Bw. Spika, ninajua ya kwamba, Mhe. Kipchumba Murkomen ambaye tumekuwa na yeye hapa na mwenye kupewa hio Wizara, atawajabika. Nilitazama nikijua sisi tutafuzu sababu hizo mbio kila wakati tumekuwa tukifuzu. Lakini, niliona wakimbiaji wa Kenya wakishindwa na wakimbiaji wa ... view
  • 7 Aug 2024 in Senate: Asante sana Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Nachukua fursa hii kumpongeza Seneta wa Bungoma kwa Taarifa aliyoleta kuhusu madeni. Limekuwa donda sugu kwa sababu tumeliongea si mara moja. Hili jambo la wanakandarasi kupewa kazi na hatimaye kutolipwa inaleta sintofahamu. Ni vizuri ijulikane kwamba wakati kazi inapeanwa, inasemekana pesa ziko katika bajeti. Kwa hivyo, mtu kutolipwa pesa zake inaleta mtafaruku kwa sababu unakuta mtu alikopa pesa kwa benki halafu anakuja kupigwa mnada na mali yake kuchukuliwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, ... view
  • 7 Aug 2024 in Senate: Sen. Osotsi amesema vizuri kwamba unapata wengine wanaanguka na kufariki kwa sababu ya mshtuko wa roho, kwa kujitolea. Katiba yetu ya Kenya inasema kiwango fulani cha kazi kipewe watu fulani. Unapata wengine ni vilema na vijana ambao hawana zile pesa na wamekopa, halafu mali yao ile kidogo waliokuwa nayo inauzwa. Kama vile Seneta wa Bungoma alivyosema, ukitembelea sehemu hiyo, utapata ule Uga wa Masinde Muliro uliotengenezwa na mwanakandarasi anayejulikana kama Ruwao. Ametumia zaidi ya Kshs150 milioni na gatuzi lenyewe halijaweza kumlipa kitu chochote. Hili ni jambo ambalo si la kawaida na limekuwa mazoea. Hapa Seneti tunaongea na hakuna lolote linalofanyika. ... view
  • 1 Aug 2024 in Senate: On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus