John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 101 to 110 of 2259.

  • 18 Sep 2024 in Senate: Thank you, Madam Temporary Speaker. I thought I heard the Cabinet Secretary say that he was laying a foundation so that he could answer the Question. I was following. Can we get it generally because all Questions are related? That is what I heard him say. view
  • 18 Sep 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono kubadilisha kwa tarehe ya kuwa na kikao katika Kaunti ya Busia. Hii inapatia Seneti fursa ya kutembea mashinani ili kuchangamkia mambo yanayowahusu watu katika ile kaunti. Haijapotea kwangu kwamba Seneti hii imetembea katika kaunti nyingi. Tumetembea Kaunti ya Kitui ambapo tuliona kwamba Gavana alikuwa ametengeneza kiwanda cha kutengeneza nguo wakati ule. Tulienda Uasin Gishu tukaona wakulima wamejawa na ghadhabu wakati ule wakisema kwamba wanataka bei yao ya mahindi iangaliwe. Nakumbuka Mhe. Murkomen aliambiwa “wacha Kiingereza. Una Kiingereza kizuri lakini leo ongea mahindi.” Tukienda mashinani tunaweza kupata haya mambo ... view
  • 20 Aug 2024 in Senate: Bw. Spika, asante sana kwa kunipa fursa hii. Mwanzo, nampongeza Bw. Douglas Kanja kwa kuteuliwa kuwa generali mkuu wa polisi. Ni vizuri ijulikane wazi, Kanja anapokuja, aje akijua kwamba kazi kuu ya Serikali yoyote ni kulinda mali na maisha ya wananchi. Bw. Spika, ukitembea sehemu nyingi za Bonde la Ufa, hasa Laikipia County, utapata wakati mwingi watu wanaishi kwa maisha ya kukimbizwa na kuibiwa na wezi wa mifugo. Ningependa kumuuliza Generali wa Polisi atakapoingia, azingatie na kukubalia tuongeze askari wetu wa ziada, kwa Kingereza wanaitwa National Police Reservists (NPR). Hii ni kwa sababu hawa ndio askari walio na uzoefu na ... view

  • 20 Aug 2024 in Senate: Kwa mambo ya maandamano yaliyokuwa yakifanyika katika nchi ya Kenya, sisi tulitoa mwongozo hapa na tukapitisha vile ambavyo Serikali inapaswa kufanya. Kwa hivyo, hatuna haja ya kujisumbua kumuuliza huyu afisa. Anapaswa kufuata mambo ambayo tulielekeza katika Bunge hili. Tulisema ya kwamba, wale waliouawa wanafaa kufidiwa na Serikali. Vile vile, tulisema walioko kwa hospitali pia wanapaswa kufidiwa. Ningependa kusema nampongeza huyu afisa. Tukiangalia historia yake, ni mtu aliye na uzoefu, sina shaka. Namtakia kila la heri katika jukumu mpya alilopewa la kuongoza askari wetu. Tunajua ya kwamba, baada yamuda aliopewa, tutaona kazi atakayaokuwa ameifanya. view

  • 20 Aug 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Shahidi mheshimiwa Mawira, sijui ni kuamini leo ama ule wakati mwingine ulikuja hapa. Hii ni kwa sababu Bibilia inasema unapaswa utumiwe kama chombo. Sijui kama wewe ni chombo? Unasema ulishurutishwa na ulitishwa wakati ule mwingine. Leo ulipokuwa ukiongea, ulisema ya kwamba huwezi kutaja majina fulani kwa sababu unahofia maisha yako. Sijui nitakuamini leo ama wakati ule mwingine. Nina ugumu na ninakanganyikiwa. view
  • 20 Aug 2024 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I stand here to support the Motion. Everybody has listened to what has been presented to this House and it is up to this House to make their decision. Today, we sit here as judges. We have listened to the evidence that has been placed to this Senate. It is up to us to make an informed decision whether to support this Motion or otherwise. Mr. Speaker, Sir, I support and second this Motion. view
  • 19 Aug 2024 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda. Katika kanda za video ambazo--- view
  • 19 Aug 2024 in Senate: Bw. Spika wa Muda, katika kanda za video ambazo tumeonyeshwa hapa, tulimwona Gavana Kawira akisema kuwa kuna pesa ambazo zimechangwa. Hii ilinikanganya kidogo kwa sababu alipokuwa akinena kwa lugha ya Kimeru alisema kuwa pesa zilizokusanywa ni shilingi milioni 87. Lakini alipozungumza kwa lugha ya Kiswahili alisema pesa zilizokusanywa ni shilingi millioni 60 na akasema zinaweza tumika kumjengea nyumba ya ghorofa yule mjane na vilevile anunuliwe gari. Bw. Spika wa Muda, katika kanda nyingine ya video, nilimsikia MCA akisema kuwa Gavana wa Meru County ni wazimu. Lakini, baadaye alipokuwa akiulizwa kuhusu swala lile alisema kuwa alinukuliwa vibaya. Mimi nashindwa kama ni ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus