22 Oct 2024 in Senate:
(CHPs) kwa Kiingereza hawajalipwa. Wanasononeka wakizunguka ilhali wanafanya kazi nzuri. Seneti ilikuwa imewatengea Shilingi 5.2 bilioni ila wale wa Bunge la Kitaifa wakapunguza bila kutazama kazi nzuri ya afya wanayofanya pale nyanjani. Kumbuka hii ni sehemu kubwa iliyotengwa na hawa ndio tutakaowategemea kwa sababu kabla ya mtu kwenda hospitali, anapaswa kuonekana na hawa maofisaa wa afya wa nyanjani. Ila pesa iliyotengwa ya shilingi 5.2 bilioni imepunguzwa hadi shilingi 2.5 bilioni. Ningetaka tusimame kidete. Walio katika Kamati ya Mshikamano wa Kitaifa, fursa sawa na utangamano wa kikanda wasibanduke. Wakae vile Seneti imesema kwa sababu kazi kuu ya seneti ni kulinda na ...
view
17 Oct 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. My question goes to hon. Mutuse. Was Treetops Hotel available for acquisition? If that is so, was there any law of procurement that was breached? Secondly, what is the age of the Deputy President’s sons? Thank you.
view
15 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa ninamshukuru Seneta wa Isiolo, Sen. Fatuma Dullo, kwa swali aliuliza ili tupate mwelekeo, na tumeupata. Ninamshukuru Sen. Dullo sababu amekuwa mzoefu na amekuwa kwa Seneti hii kwa muda mrefu. Swali alilouliza ni swali nzuri kwa sababu, gavana Guyo anahitajika kuja hapa katika Seneti au Kamati ya Seneti hii na kujibu maswali. Si maswali ya Seneta, ni maswali ambayo watu wa Isiolo wanataka. Wangetaka huduma na hayo ndio maswali yanayoulizwa. Bw. Spika wa Muda, imenivunja moyo sana kusikia gavana anakuja mbele ya Kamati na hakuna jambo anafanya, ila kuleta dharau ...
view
9 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Mimi ninasumbuka kwa sababu, tayari tumejitia kitanzi kwa kutenga siku za kujadili Hoja hii. Vile vile tutakapokuwa katika Hoja ile halafu kuweko na masuala mengine nyeti, tutajipata katika ile sehemu ya kwamba, hatuna muda wa kutosha kuyaangazia masuala yale kiundani. Hatuwezi kuendelea siku ile nyingine ambayo ni Jumatano kwa sababu tayari tumeitenga kwa shughuli nyingine tofauti.Kwa hivyo kuendelea mbele, pengine tuwe tukipea muda zaidi. Hata hivyo, ninaunga mkono.
view
1 Oct 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ninaunga mkono Taarifa iliyoletwa na Seneta Onyonka kuhusu usimamizi wa shamba la ADC. Hii ni Taarifa nzuri sana kwa sababu kule sehemu za Laikipia kuna shamba kubwa sana la ADC. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
1 Oct 2024 in Senate:
Badala ya shamba lile kuleta afueni kwa ufanyi biashara wa Serikali kama kuweka ng’ombe wa nyama, unapata hilo shamba linakua donda sugu kwa wakaaji wa sehemu ile. Hii ni kwa sababu, wafugaji na wezi wanajificha kule, wakiwavizia na wakiwavamia wakaaji wa kule ambao hawana hatia yeyote.
view
1 Oct 2024 in Senate:
Vile vile, ile sehemu inatumika vibaya kwa sababu Serikali haizingatii kuweka usalama katika lile shamba kwa sababu shamba ni kubwa na wamelemewa kufanya kazi wanayopaswa kufanya. Pia, kuna wanyama wa mwituni kama ndovu wanaoishi pale na wanavamia mashamba ya wakulima kila wakati. Bw. Spika, badala ya haya mashamba ya ADC kuwa na faida, yanakua donda sugu na yanaendelea kuwasumbua wananchi. Ningependekeza kwa Kamati inayohusika iweze kuzingatia na iseme kwamba, ikiwa Serikali imeshindwa kuilinda lile shamba, igawanye hayo mashamba kwa wananchi, ili wayatumie kwa hali ambayo inafaa kutumiwa.
view
1 Oct 2024 in Senate:
On a point of order, Mr. Temporary Speaker, Sir.
view
1 Oct 2024 in Senate:
Mr. Temporary Speaker, Sir, about tribalism and him being a Chairman, is a story for another day. However, he talked about the EACC and he, first, needs to table the report of the EACC. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
19 Sep 2024 in Senate:
Asante Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, kulingana na ripoti iliyoletwa na Seneta Tobiko kuhusu watu kutekwa nyara, ningetaka kusema ya kwamba, Mkuu wa Polisi, Douglas Kanja, ameteuliwa rasmi. Anapaswa atokee kimasomaso ili aweze kupambana na haya mambo na aweze kuyakomesha. Hii ni kwa sababu, kuna sheria zinapaswa kufuatwa. Kama mtu ametenda kosa, ashikwe, apelekwe kortini na ahukumiwe. Hakuna kosa ambalo haliwezi kupewa adhabu yake. Tunapoongea hapa, mwakilishi wa Wadi ya Dela hajulikani alipo. Kwa sababu sasa tuko na askari mkuu aliyeteuliwa kirasmi, ana majukumu ambayo anapaswa awe akiangalia. Bw. Naibu wa Spika, si hiyo tu, Taarifa ...
view