John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 81 to 90 of 2259.

  • 20 Feb 2025 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate. view
  • 20 Feb 2025 in Senate: Ningependa kuwaambia kwamba, mtie masomo mbele na muendelee na hii kazi nzuri ambayo mnafanya. Hata ingawa mnasomea matibabu, nawajulisha kwamba mnaweza kuwa viongozi kama wale walio hapa. Kama vile Naibu Spika alifanya, alitaka muwe na maono na mawazo mazuri ya kuwatibu Wakenya wote. Nawatakia mema mkiwa hapa mkiona vile mjadala unaendelea katika Seneti hii. Mkirudi nyumbani, Meru, mseme hata sisi hapa tunamuenzi na kumpenda Naibu Spika wetu. Museme pia hata sisi tumempatia mamlaka hapa na mkirudi huko mmuombee na mmpe chochote anachotaka. Asanteni sana. view
  • 20 Feb 2025 in Senate: Mr. Deputy Speaker, Sir, I beg to give Notice of the following Motion- THAT, the Senate notes the Report of the 9th Inter-Parliamentary Union (IPU) Global Conference of Young Parliamentarians held in Hanoi, Vietnam from 15th to 17th September, 2023 laid on the Table of the Senate on Tuesday, 5th March, 2024. view
  • 19 Feb 2025 in Senate: Madam Temporary Speaker, I was just concerned. Why was it difficult for Sen. Okiya Omtatah to indicate the site or source of his information? Whether the source is correct or not, it is up to the Senate to rule on that matter. He told us the site. Why were we getting concerned? We should have checked. If it is incorrect, he was supposed to be told on the spot that the site is not admissible in the Senate. view
  • 18 Feb 2025 in Senate: Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, kwa uchungu na huzuni nataka kuleta risala zangu za rambirambi kwa familia ya mwenda zake, Seneta William Cheptumo. Bw. Spika wa Muda, nikubalie kabla sijaleta risala zangu za rambirambi, nataka kuchukua fursa hii kutoa shukrani kwa Seneti pamoja na wafanyakazi wote wa Seneti na Bunge la Kitaifa. Hii ni kwa sababu juzi nilimpoteza babaangu, Seneti na wafanyakazi wa Bunge walisimama nami. Sitaki kuchukulia jambo hilo kwa mzaha. Nataka kuwashukuru kutoka pangu rohoni na niwaambie asante na asante sana. Uchungu nilionao wa kumpoteza mzazi ninauelewa vile vile uchungu wa ... view
  • 18 Feb 2025 in Senate: Bw. Spika wa Muda, jambo hili limenifanya nikakumbuka ya kwamba sio miaka mingi ambayo utaishi dunia, ni vile ambavyo utakavyofanya ukiwa duniani. Nikisoma katika Kitabu Kitakatifu cha Mungu, Bibilia yangu inaniambia ‘naye Methusela akaishi zaidi ya miaka 900 lakini hakuna kitu alifanya isipokuwa kuishi duniani.’ Yesu aliishi miaka 32 duniani na alifanya mambo mengi. Kwa hivyo, ni vile ambavyo utakavyofanya ndio itakavyo kumbukwa. Sitaki kumsahau Mhe. Malulu Injendi, Mbunge wa Malava, kwa sababu alichangia Mswada wa Wazee wa Mitaani. Nakumbuka vizuri kwa sababu hawa wazee wanasaidia sana katika uongozi kule vijijini. Ni vizuri vile Injendi aliwaslisha Mswada huo. Itakuwa vyema ... view
  • 20 Nov 2024 in Senate: Thank you, Mr. Speaker, Sir. I am concerned about funding because she has repeated about funding for a long time. She is saying that if she does not get funding, she will not do so much concerning the issue of titling. I had raised the issue of titling of Maina Village, which she is aware of. I had also mentioned about Likie. My concern is how much money the Ministry needs so that at least she can finish her work. How much has she gotten? With the amount she has, how many years then are we going to wait? I ... view
  • 22 Oct 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika. Ningepenga kupongeza Kamati yetu ya Fedha na Bajeti ya Seneti kwa kazi nzuri wanayoitekeleza. Ni jambo la kuvunja moyo kwa sababu, ukiangalia, hela ambazo Kamati hiyo ilikuwa imetenga, Mswada huo ulipoenda katika Bunge la Kitaifa, walipunguza mgao huo kwa Shilingi 46.5 bilioni. Ni kana kwamba hawaelewi mambo ya ugatuzi yanavyoendelea. Hii ni kwa sababu, hakuna hela zozote zimebaki baada ya kupuguza pesa hizi kwa kiwango hiki, za kufanya majengo ambayo yalipaswa kujengwa katika view
  • 22 Oct 2024 in Senate: zetu. Vile vile, ukitembea katika gatuzi zetu zote, barabara ziko katika hali mbovu kwa sababu mvua imeziathiri lakini Bunge la Kitaifa hawana njia ya kuangalia. Wanapunguza fedha ambazo zinaenda katika gatuzi zetu shilingi 10.5 bilioni. Kwa hivyo, ukitembea katika gatuzi zetu utapata hakuna Barabara. Vile vile, kwa sababu tunategemea fedha hizi kununua madawa, hospitali zetu hazina madawa. Watu hawajalipwa, ilhali kazi yetu kama Seneti ni kulinda na kutetea gatuzi zetu. Kwa hivyo, hatutakubaliana na mtu yeyote atakayekuwa kazi yake ni kupunguza fedha ama kuonyesha kana kwamba yeye anapigana na ugatuzi. Bw. Spika, Kamati yetu ilijitolea kuleta maendeleo katika sehemu zetu ... view
  • 22 Oct 2024 in Senate: kutengeneza hizi viwanda vidogo. Hata hivyo, pesa ambazo ziliwekwa na Kamati yetu, Shilingi 5.2 bilioni zilipunguzwa mpaka Shilingi bilioni mbili. Kwa hivyo, ile miradi ambayo ingetekelezwa kutumia fedha hizo imepungua na hata mengine haitaketekelezwa. Kwa hivyo, ningependa kusema ya kwamba, hii Kamati yetu ya Seneti ilifanya kazi nzuri lakini wenzetu wa Bunge la Kitaifa wanaonekana ya kwamba wanapinga ugatuzi usiendelee. Nafikiri pengine wanapinga ndio ili National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF) yao ifanye ile kazi ambayo ingefanywa na magavana, ila hatutakubali. Wale wasaidizi wa wauguzi pale nyanjani, wanaoitwa Community Health view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus